JAMHURI YA MUUNGANO
WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA
WATOTO
TANZANIA
KUWA MNUNUZI MKUU WA DAWA NA VIFAA TIBA UKANDA WA SADC
Mawaziri
wa Afya wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Africa
(SADC) kwa kauli moja wamepitisha uteuzi wa nchi ya Tanzania kupitia Bohari ya
Dawa (MSD) kuwa Mnunuzi Mkuu wa Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara
kwa ajili ya nchi hizo kupitia mfumo wa Ununuzi Shirikishi (Pooled Procurement Services (SPPS).
Uteuzi
huo wa nchi ya Tanzania umepita bila kipingamizi mwishoni mwa wiki kwenye
Mkutano wa Mkutano wa Mawaziri wa Afya wa nchi za SADC uliowakutanisha Mawaziri
wa Afya na Mawaziri wanaohusika na
masuala ya UKIMWI uliofanyika mjini Polokwane, Limpopo – Afrika Kusini.
Hatua
ya uteuzi wa Tanzania kuwa mnunuzi mkuu wa Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya
Maabara umetokana na juhudi za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. John Pombe Magufuli kuimarisha hali ya upatikanaji wa dawa MSD ambapo sasa
inatekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa .
Aidha,umahiri
na uzoefu wa Bohari ya Dawa (MSD) katika masuala ya ununuzi, utunzaji na
usambazaji Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara (yaani mnyororo wa
ugavi) unaeleweka na kuaminika vizuri hata na nchi nyingine zilizowahi
kututembelea kujifunza na kubadilishana uzoefu.
Kwa
hatua hiyo MSD itakuwa na dhamana na majukumu yafuatayo:
·
Kununua
Dawa na Vifaa Tiba kwa ajili ya nchi za SADC
·
Usimamizi wa taarifa na takwimu za Dawa na
Vifaa Tiba vitakavyohitajika
·
Usimamizi
wa kanzidata (Database) ya dawa za nchi wananchama wa SADC na usimamizi wa bei
elekezi ya Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara
·
Kusimamia manunuzi ya Dawa, Vifaa Tiba na
Vitendanishi vya Maabara kwa ajili ya Ukanda wa SADC na kusimamia mnyororo wa
ugavi
·
Kutoa
huduma za kitaalamu na kupanga bei elekezi na
·
Kutoa
huduma za ushauri wa kitaalam katika masuala ya dawa na vifaa tiba.
Hatua hii itapunguza kwa kiasi kikubwa bei
ya dawa na vifaa tiba kwa ajili ya matumizi ya nchi wananchama wa SADC. Jambo
ambalo limeipatia heshima na sifa kubwa Tanzania, kwani imeaminiwa kufanya
ununuzi wa dawa kwa niaba ya nchi nyingine kumi na tano (15) ambazo ni
wanachama wa SADC.
Tanzania
kupewa jukumu hilo ni jambo la kujivunia sana tena inaonyesha dhahiri tumetambulika
tuko vizuri kwenye masuala mazima ya mnyororo wa ugavi kwa nchi wanachama wa
SADC.
Faida zitakazopatikana
kwa Tanzania kuwa Mwenyeji wa huduma hii ni kama zifuatazo:
·
Heshima
kwa nchi yetu kwa kuaminiwa na nchi wanachama wa SADC baada ya kukidhi vigezo
vya kitaalam
·
Viwanda
vyetu vya ndani vitaweza kuuza dawa zao kwa nchi za SADC, kwani wajumbe wa
mkutano tumekubaliana kuwa na kituo kimoja kitakachoshughulikia udhibiti ubora
na ukaguzi
·
Bei ya dawa itapungua zaidi maana sasa
tutaweza kwenda moja kwa moja kwa wazalishaji sio kama nchi (Tanzania), lakini
kama Ukanda unaoshughulikia nchi 15
·
Itaongeza
ajira na kuijengea uwezo Bohari ya dawa(MSD)
Imetolewa
na:
Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini-Afya
16/11/2017
0 on: "TANZANIA KUWA MNUNUZI MKUU WA DAWA NA VIFAA TIBA UKANDA WA SADC"