Na WAMJWW
Barozi wa Japan
nchini Tanzania Mh.Masaham Yoshida mapema leo amefanya mazungumzo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es
salaam, lengo likiwa ni kuimarisha ushirikiano wa nchi hizo mbili hususani
katika masuala za huduma ya Afya.
Mh.Masaham Yoshida ameahidi kuisaidia Sekta ya Afya kupitia mradi
wa “SUMITOMO CHEMICAL PROJECT” wenye lengo la kuangamiza mazalia ya mbu kwa
kutumia Viuwadudu, mradi huo umeanza kufanya kazi katika maeneo ya Nyanja ya
juu Kusini katika Mkoa wa Mbeya. Hata hivyo Mh.Masaham Yoshida ameahidi
kuendeleza ushirikiano huo na Serikali ya Tanzania.
Nae Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu ameshukuru ugeni
huo kutoka Japan ulio na tija kwa taifa la Tanzania katika Sekta ya Afya huku akisisitiza na
kuweka mkazo katika ushirikiano huo ili kusukuma gurudumu la maendeleo ya
Sekta ya Afya nchini.
0 on: "BAROZI WA JAPAN NCHINI AFANYA MAZUNGUMZO NA MH. UMMY MWALIMU (MB)."