Na WAMJWW.
WAZIRI wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameendelea kusisitiza kuwa wananchi hawapaswi
kununua damu kwani huduma hiyo ni bure kwa watanzania wote katika hospitali
zote.
Hayo amezungumza leo
jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa Benki ya damu iliyodhaminiwa na
Ubalozi wa Kuwait katika Taasisi ya Mifupa MOI ambapo uliuzuliwa na Balozi wa
Kuwait nchini Tanzania.
“Watanzania
wanahoitaji huduma ya kuongezewa damu wapewe bure marufuku kwa watoa huduma za
vituo vya afya pamoja na hospitali zote kuuza damu hiyo kwani inatoka kwa
wananchi wenyewe” alisisitiza Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy
amesema kuwa wananchi wanatakiwa kujitokeza katika kuchangia damu ili kuweza
kuwa na hifadhi ya kutosha na kufanya kazi kwa wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo
kwa wakati sahihi bila ya usumbufu wowote katika kuokoa maisha ya watanzania.
Mbali na hayo Waziri
Ummy amesema kuwa anayo furaha kutimiza
miaka miwili tangu kuingia kwa Serikali ya awamu ya tano kwa kupiga hatua
katika sekta ya afya hasa katika kupunguza rufaa za nje na kuwa na utaalamu wa
matibabu ya kibingwa kama vile upandikizaji wa figo, vifaa vya usikivu( Coclea
Impant) na kutibu magonjwa ya moyo.
Kwa upande wake Balozi
wa Kuwait Nchini Tanzania Bw. Jasem Ibrahim Al-Najem amesema kuwa wameamua kuchangia kiasi cha fedha cha
shilingi Milioni 200 katika kutengeneza Benki hiyo ya damu MOI ili kuweza
kusaidia kuboresha sekta ya afya nchini.
“Mbali na kiasi hicho cha
fedha pia tumetoa Dola za Kimarekani 500 ili kuweza kusaidia walemavu mbalimbali katika kulejesha hali zao
za kawaida hapa nchini” alisema Bw. Al-Najem.
Aidha katika uzinduzi
huo wa Benki ya damu Balozi Al-Najem alijitolea damu unit moja ili kuweza kuchangia
benki hiyo ya taasisi ya Mifupa MOI ili kuweza kuhamasisjha na wananchi wengine
waweze kuchangia damu kwa msaada wa wagonjwa wengine.
Kwa upande wake
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Lwezimula alisema kuwa katika
kuhakikisha Matibabu ya kibingwa yanapiga hatua nchini waliamu kuanzisha kambi
za matibabu kuanzia mwaka 2000 na kufanya taasisi zingine za afya kuiga mfano
huo.
“Tunataka kuhamasisha
matibabu ya kibingwa kufanyika nchini pamoja na uchangiaji damu kwani damu hiyo
haitatumika MOI peke yake bali hata kwenye Taasisi zingne na vituo vya Afya
nchini kote” alisema Dkt. Lwezimula.
Sambamba na tukio hilo
Kikundi cha Kutayarisha Madereva wa Magari Makubwa Wanawake (WOW) Afrika Mashariki walijitolea
kuchangia damu ili kuweza kusapoti benki hiyo kwa ajili ya wagonjwa wanaohitaji
huduma hiyo ya damu.
“Tumehamasika kuja
kuchangia damu ili kuweza kutoa mfano kwa wanachi wengie waweze kujitolea
katika uchangiaji huu wa damu ili kujenga taifa lenye watu wenye afya bora”
alisema Mkurugenzi wa WOW Bw. Martin Gabone.
0 on: "WAZIRI UMMY ASEMA WANANCHI WASIUZIWE DAMU "