Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya
,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya akimjulia
hali Mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji Mkubwa wa Mgongo , kulia kwake ni Daktari bingwa
wa Upasuaji wa Ubongo na Mgongo Dkt Nicephorus Rutabansibwa akitoa maelekezo juu ya maendeleo ya mgonjwa huyo, wa mwisho ni Mganga mkuu wa Serikali Prof.
Muhamad Kambi.
.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya
,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya akikagua
mashine mojawapo katika benki ya damua ya MOI.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya
,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya pamoja na
Mganga Mkuu wa Serikali akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa Maabara Bwana
Mbuta Jackson ya namna benki mpya ya
damu inavyfanya kazi kwa kushirikiana na damu salama.
Katibu Mkuu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,
Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya akitoa maelekezo mbele ya menejimenti ya MOI wakati akikagua miundombinu, mapema leo wakati wa ziara yake katika taasisi hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya
,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya akizungumza
na menejimenti ya MOI katika ukumbi wa Mikutano MOI
Menejimenti ya MOI wakifuatilia hotuba
ya katibu Mkuu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,
Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya katika ukumbi wa Mikutano MOI
Picha ya pamoja ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya
,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya na
Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Muhamad Kambi wakiwa na menejimenti ya MOI wakati alipofanya ziara katika taasisi hiyo mapema leo.
Na WAMJWW-DSM
Taasisi
ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Ubongo ,Mgongo na Mishipa ya Fahamu (MOI)
imeokoa zaidi ya shilingi Bilioni 5 ambazo zingetumika kusafirisha wagonjwa nje
nchi kufuataia kuanzisha huduma za kibingwa ambazo awali zilikua hazipatikani
hapa nchini.
Hayo
yamebainishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee
na watoto Dkt Mpoki Ulisubisya alipofanya ziara katika taasisi hiyo na kukagua
hali ya utoaji wa huduma, miundombinu na kuwajulia hali wagonjwa.
Akizungumza
na menejimenti ya MOI Dkt Ulisubisya amepongeza kazi nzuri na kubwa inayofanywa
ambayo imepelekea watanzania kupata huduma bora za kibingwa ambazo wangepaswa
kuzifuata nje ya nchi.
“Mnafanya
kazi nzuri sana , jambo ambalo linatupa faraja kubwa sisi viongozi wenu, naomba
muongeze ubunifu zaidi. Hamtakiwi kuifikiria MOI kwenye ukanda huu wa Afrika
pekee bali duniani. Hii ni changamoto kwetu sote kuifikisha hapo”. Dkt
Ulisubisya
Aidha,
Dkt Ulisubisya amebaini kuwa MOI imepunguza rufaa za kwenda nje ya nchi kwa
asilimia 95% na inaweza kulimaliza kabisa tatizo hilo ili pasiwepo mgonjwa wa
kwenda nje.
Pia,
amewaelekeza viongozi wa MOI kwa kushirikiana na Wizara mama kutafuta namna ya
kufuta rufaa kwa kutoa mapendekezo na ushauri kwa wizara
“Azma
ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mh .Dkt John Pombe Magufuli ni kuhakikisha
huduma zote za Afya zinapatikana hapa nchini na vyema sote tukamuunga mkono”
Dkt Ulisubisya
Kwa
upande wake Mganga mkuu wa Serikali Profesa Muhamad Kambi ameupongeza uongozi
wa MOI kwa kuwa na maono ya mbali ya kuifanya MOI kuwa Taasisi bora barani
Afrika na duniani:
“Nimefurahi
kwamba MOI mna maono ya mbali , mnafikiria kuitoa Taasisi hii hapa ilipo na
kuifikisha sehemu ya juu zaidi, dira yenu ni kuwa Taasisi bora Afrika kufikia
2022 fanyeni kazi kwa bidii kufikia lengo hilo .” Prof Muhamad Kambi
Awali
akiwasilisha taarifa ya Utendaji, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt Respicious
Boniface amesema toka Taasisi hiyo ianzishwe, imefanikiwa kuanzisha huduma za
kibingwa za Upasuaji wa Nyonga, Magoti, Ubongo, Mgongo, Vibiongo, Usingizi
ambazo zimesaidia kupunguza rufaa za nje ya nchi.
“Mh
Katibu Mkuu ,baada ya kuanzisha huduma hizi za Kibingwa tumefanikiwa kuokoa
shilingi Bilioni 5 ambazo zingetumika kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi,
tumepunguza rufaa kwa asilimia kubwa
naomba nikuhakikishie hata hizi asilimia 5% zilizobaki tutashirikiana na
Serikali na naamini zitakwisha kabisa” Dkt Respicious Boniface.
0 on: "MOI YAOKOA BILIONI 5 KWA KUPUNGUZA RUFAA ZA NJE YA NCHI."