Na WAMJWW
Bodi
ya Shirika la kimataifa la HelpAge yaahidi kushirikiana na Serikali ya Tanzania
kupitia Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutatua
changamoto mbali mbali zinazowakabili wazee wa Tanzania ikiwemo ukatili dhidi
ya vikongwe.
Hayo
yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mh.
Arun Maira wakati alipokutana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu mapema leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini
Dar es salaam.
Mh. Arun Maira ameipongeza Serikali ya awamu ya tano chini ya Raisi Dkt. John Magufuli kwa jitihada kubwa anayofanya katika kusimamia ustawi na maendeleo ya Wazee
hususani katika masuala ya huduma ya Afya.
Aidha
Mh. Arun Maira aliahidi kuimarisha ushirikiano na Serikali ya Tanzania kupitia
Wizara ya Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto kwa kusaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa
wazee kupitia utekelezaji wa mkakati wa kutokomeza mauaji ya Wazee mara tu
utakapokamilika.
Mh. Arun
Maira aliendelea kusisitiza kwamba changamoto hizi za Wazee ikiwemo suala la
ukatili wataliweka kama moja ya vipaumbele katika mpango kazi wao ili kuwezesha utekelezaji huo.
Nae
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu
aliwashukuru wajumbe hao wa bodi ya Shirika la kimataifa la HelpAge kwa kutatua
changamoto mbali mbali zinazowahusu wazee
wa Tanzania hususani katika
kusaidia kampeni ya “Mzee kwanza”.
Mwisho
Mh. Ummy aliiomba bodi hiyo kuweka nguvu zaidi katika suala la ulinzi wa wazee
hususani katika utekelezaji wa mkakati
wa kuzuia mauaji na ukatili wa vikongwe kupitia mkakati wa kutokomeza mauaji ya
wazee.
0 on: "SHIRIKA LA KIMATAIFA LA HELPAGE LAAHIDI KUWASAIDIA WAZEE WA TANZANIA"