Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa
kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98 leo jijini Dar es salaam.
Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kulia akipokea moja ya vifaa vya uchunguzi wa saratani
ya kizazi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia
Zoungran kushoto wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kuchunguza saratani ya
kizazi leo jijini Dar es salaam.
Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kulia akipokea moja ya nyenzo za kufundishia juu ya uchunguzi wa saratani ya
kizazi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia
Zoungran kushoto wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kuchunguza saratani ya
kizazi leo jijini Dar es salaam katikati ni Afisa Afya kutoka USAID Bi. Ananth
Thambinyga.
Mkurugenzi
Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran akiongea na waandishi wa
habari hawapo pichani wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye
thamani ya shilingi milioni 98 leo
jijini Dar es salaa.
Waziri Wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akiwa
kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Wizara ya afya,Jhpiego na USAID wakati wa
kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98 leo jijini Dar es salaam, wa tatu kushoto ni Mkurugenzi
Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran na aliyevaa nguo ya
pundamilia ni Afisa Afya kutoka USAID Bi. Ananth Thambinygan.
WAZIRI Wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amewaelekeza
waganga wakuu wa mikoa wote nchini kuanzisha zoezi la wazi la uchunguzi wa
saratani ya kizazi angalau mara moja katika mwezi ili kusaidia kutokomeza
tatizo kwa wanawake hilo nchini.
Hayo amesema
wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratan vyenye thamani ya shilingi
milioni 98 ambavyo vimetolewa na Taasisi
isiyo ya Kiserikali ya JHPIEGO kwa kushirikiana na USAID ili kusaidia kupambana
na tatizo hilo nchini.
“Angalau
ifikapo Desemba 2018 nataka vituo vya
Afya vya Serikali 524 viwe vinatoa huduma ya matibabu ya awali ya
Saratani ya mlango wa kizazi na kufikia
wanawake milioni 3 watakaopata huduma hii ili kuokoa wanawake wa
vijijini kwani mpaka sasa hivi tunavyo
vituo vya afya 265 vinavyotoa huduma hii
” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri
Ummy amesema kuwa uchunguzi na kutoa chanjo ya Saratani ya mlango wa kikazi kwa wasichana kuanzia miaka 9 mpaka 14 ili
kuweza kupunguza vifo vitokanavyo na tatizo hilo kwani katika kila wanawake 100
vifo vinavyotokana na ugonjwa huo ni 32.
Mbali na hayo
Waziri Ummy amesema kuwa katika kuongeza jitihada za kupambana na ugonjwa huo Serikali imeongeza
vituo vya afya 100 kutoka 343 hadi
kufikia 443 mwaka huu ili kutokomeza tatizo hilo nchini.
Kwa upande
wake Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran amesema
kuwa walianzisha mpango wa kupambana na tatizo hilo na kufanikiwa kuwafikia
wanawake elfu 75 kwa mikoa 4 tangu mwaka 2009.
“Mbali na
mikoa hiyo 4 bado tunalengo la kuongeza mikoa mingine 7 ili kuweza kutoa huduma
hiyo kwa ajili ya kuunga mkono Juhudi za Serikali katika kupambana na Saratani
ya mlango wa kizazi ili kuweza kuokoa wanawake wengi zaidi nchini” alisema Bw.
Zoungran.
0 on: "WAZIRI UMMY AWATAKA WAGANGA WAKUU WA MIKOA KUANZISHA ZOEZI LA WAZI UCHUNGUZI WA SARATANI YA KIZAZI KWA WANAWAKE."