Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Bakar Kambi akisisitiza jambo wakati
wa Semina ya uhamasishaji wa wahariri na wakuu wa Idara ya Afya juu ya magonjwa
yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ilofanyika mapema leo katika ofisi za Wizara ya
Afya jijini Dar es salaam, pembeni yake ni
Dkt. Janeth Mgamba.
Mkurugenzi msaidizi
ufuatiliaji wa magonjwa ya milipuko Dkt. Janeth Mgamba akitoa taarifa fupi
mbele ya wahariri na wakuu wa Idara ya Afya katika semina ya uhamasishaji
kuhusu magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
Watumishi wa Idara ya Afya wakifuatilia kwa makini Semina ya
uhamasishaji wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele iliyofunguliwa na
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Bakar Kambi mapema leo katika ofisi za Wizara ya
Afya jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Blog ya Full Shangwe wa Bahati Bukuku akitoa mchango
katika Semina ya uhamasishaji juu ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele
mbele ya wahariri na wakuu wa Idara ya Afya.
Meneja mpango wa kupambana na magonjwa yaliyokuwa hayapewi
kipaumbele Dkt. Upendo Mwingira akiwasilisha mada mbele ya wahariri na wakuu wa
Idara ya Afya katika semina ya uhamasishaji wa magonjwa ambayo yalikuwa
hayapewi kipaumbele.
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto
imefanikiwa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa asilimia
90 kupitia mpango wa kudhibiti magonjwa hayo hapa nchini NTD.
Hayo yamezungumzwa na Mganga Mkuu wa
Serikali Prof. Bakari Kambi wakati
alipofungua semina ya uhamasishaji wa kupambana na magonjwa hayo kwa wahariri
wa vyombo vya habari na Wakuu wa idara mbalimbali wa Wizara ya Afya leo jijini
Dar es salaam.
“Tumepata mafanikio kwani mpaka
kufikia Oktoba 2017 huu tumefanikiwa kupunguza ugonjwa wa matende na mabusha katika wilaya 95
sawa na asilimia 77 kati ya wilaya 120 na hivyo tumesitisha kutoa dawa katika
wilaya hizo” alisema Prof. Kambi.
Aidha Prof. Kambi amesema kuwa katika
mafanikio hayo pia Serikali imefanikiwa kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa
Vikope (Trakoma) katika wilaya 58 sawa na asilimia 82 kati ya wilaya 71 hapa
nchini.
Kwa mujibu wa Prof. Kambi amesema kuwa
kwa maeneo ya nyanda za juu hususan katika maeneo ya Rungwe,Kyela,ileje na Busekeleo
wamefanikiwa kupima wananchi na kuonyesha kuwa maambukizi yamepungua na hivyo
kuendelea katika wilaya zilizobaki.
Kwa upande wake Mratibu wa Kitaifa wa Mpango wa kupambana na Magonjwa yaliyokuwa
hayapewi kipaumbele Dkt. Upendo mwingira amesema kuwa wanajamii wanatakiwa
wajitokeze katika kupata dawa za kujikinga na magonjwa hayo kwani muitikio ni mdogo na inaweza
kusababisha madhara makubwa siku za usoni.
Aidha Dkt. Mwingira amesema kuwa
Semina hiyo imelenga kuwaelimisha wahariri wa vyombo vya habari ili watoe
kipaumbele katika kuhamasisha wananchi juu ya matumizi ya dawa za kukinga
magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ambayo ni Matende na Mabusha, Usubi,Minyoo
na Trakoma ili kuweza kutokomeza kabisa ugonjwa huo hapa nchini.
0 on: "SERIKALI YAPIGA HATUA KATIKA KUDHIBITI MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE."