Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufika kwenye hospitali ya
Magonjwa ya kuambukiza Kibong'oto Mkoani Kilimanjaro,kushoto ni Mkuu wa
Mkoa huo Mhe.Anna Mghirwa
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Anna mghirwa akiongea wakati wa
ufunguzi wa kiyuo hicho ambacho kitakuwa kikihudumia wachimbaji wa
madini na familia zao kutokana na kifua kikuu na kudhurika na magonjwa
ya mfumo wa hewa.
Baadhi ya wachimbaji wa madini kutoka Mererani ambao walishiriki ufunguzi wa kituo hicho
Baadhi ya watumishi wa Hospitali ya Kibong'oto wakimsikiliza Waziri Ummy
Mwalimu(hayupo pichani)wakati akihutubi ambapo alisema kituo hicho ni
miongoni mwa vituo 11 vilivyojengwa katika nchi 10 za SADC
Waziri wa Afya pamoja na viongozi wa Mkoa,Mbunge pamoja na wadau wa madini wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa kituo hicho.
Waziri Ummy Mwalimu(wa kwanza kushoto),Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro
Mhe.Anna Mghirwa(kulia) walikagua chumba chenye mashine ya Uchunguzi
(Xray) iliyofungwa kwenye kituo hicho.
Waziri wa Afya (katikati)akimsikiliza kwa makini bw.Athumani
Abdalah(hayupo pichani)wakati akitoa ushuhuda wake kama mchimbaji mdogo
mdogo,kishoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Anna Mghirwa na kulia
kwake ni Mbunge wa Jimbo la Siha Dkt.Godwin Mollel
Na.WAMJW,Siha
Shughuli
za uchimbaji madini duniani kote zinatambulika kama ni shughuli
hatarishi kwa afya ya binadamu kutokana na urahisi wa kudhurika pia
athari kwenye afya ya mapafu kutokana na vumbi zito
Hayo
yamesemwa na jana na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto Ummy Mwalimu wakati wa ufunguzi wa kituo cha kisasa cha kutoa
huduma za Kifua Kikuu,UKIMWI na Magonwa yatokanayo na shughuli za
uchimbaji madini katika hospitali ya magonjwa ya kuambukiza Kibong'oto
iliyopo Mkoani Kilimanjaro
Waziri
Ummy amesema shughuli za uchimbaji humuweka mchimbaji kwenye hatari
zaidi ya kupata kwa urahisi ugonjwa wa Kifua Kikuu na Magonjwa mengine
sugu ya mfumo wa njia ya hewa,vile vile shughuli za kijamii,kiuchumi na
kiutamaduni katika maeneo ya migodi zimekua zikichochea kasi ya
maambukizi ya Ukimwi katika maeneo hayo.
"Kutokana
na changamoto hizi na ili tupunguze tatizo LA Kifua Kikuu na UKIMWI
katika sekta ya madini,mwaka 2015 nchi kumi za SADC kwa pamoja ziliomba
fedha katika mfuko wa Dunia wa Kudhibiti magonjwa ya UKIMWI,Kifua Kikuu
na Malaria(Global fund ATM) ili kukabiliana na tatizo hili katika sekta
ya madini"(TB in the Mining Sector(TIMS)
Aidha,alisema
tangu kuanza kutekelezwa kwa mradi huo Januari,2016,tayari matokeo ya
utafiti zilizofanyika maeneo ya migodi yameonesha kuwepo kwa kiwango
kidogo cha ufahamu na uelewa wa masuala ya Kifua Kikuu,UKIMWI na
magonjwa yatokanayo na shughuli za uchimbaji miongoni kwa wachimbaji na
jamii inayowazunguka.
"
wachimbaji wadogo wadogo wameendelea kuathirikanna vumbi LA silika
kutokana na kutumia dhana duni za uchimbaji usiozingatia masharti ya
udhibiti wa vumbi,licha ya sekta hii kuchangia kwa kiasi kikubwa pato LA
Taifa,hali a upatikanaji wa huduma za afya kwenye migodi si ya
kuridhisha"
Kituo hicho
cha kisasa ambacho ni cha kwanza nchini kitakua mfano na kitasaidia
kuokoa maisha na ulemavu utokanao na shughuli za uchimbaji kutokana
sehemu zingine nchini,kimefungwa vifaa vya uchunguzi ikiwepo xray na
kupatiwa daktari bingwa na wataalamu wa maabara na mionzi
0 on: "WACHIMBAJI WADODO WADOGO WA MADINI WAPATA AHUENI KWENYE AFYA"