Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo CORONA VIRUS THREAT. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo CORONA VIRUS THREAT. Onyesha machapisho yote

Alhamisi, 7 Mei 2020

DKT. NDUGULILE AIAGIZA NIMR KUFANYA UTAFITI KUHUSU UGONJWA WA CORONA

- Hakuna maoni

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza katika mkutano na watafiti wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR juu ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona.
Waziri wa Afya, Dkt. Ndugulile akifafanua jambo baada ya kumalizika kwa mkutano kujadili jinsi ya kupambana na Covid-19 nchini. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Prof. Yunus Mgaya.






Dkt. Ndugulile akijadiliana jambo pamoja na watafiti wa taasisi hiyo mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo.

WAMJW- Dar es Salaam                                                                           

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeitaka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kufanya utafiti kuhusu ugonjwa wa Corona (Covid-19) kwa kuwa kuna tofauti kubwa ya dalili zilizojitokeza kwa wagonjwa hapa nchini ukilinganisha na wagonjwa waliopo nje ya  nchi.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipokutana na watafiti wa taasisi hiyo wakati  wakijadili maambukizi ya ugonjwa wa Corona na aina ya matibabu ambayo wagonjwa wanatakiwa kupatiwa hasa baada ya kubainika kuwa dalili za ugonjwa huo zinatofautiana na dalili za wagonjwa wa mataifa mengine.

“Kuna mambo mengi ambayo tunapaswa kuyafanyia utafiti wa kisanyansi, moja ni uelewa wa jamii, tunataka kujua wagonjwa wanaougua Corona ni wagonjwa wa namna gani, wana magonjwa ya aina gani, dalili zinazowapata wagonjwa ni za aina gani.  Hapa tunataka tupate uwelewa,” amesema Dkt. Ndugulile.

Pia, amesema kupitia utafiti huo wanataka kujua aina za matibabu ambayo wagonjwa wanatakiwa kupatiwa ili kuhakikisha ugonjwa wa Covid-19 unadhibitiwa hapa nchini.

“Kutokana na muitikio mkubwa wa tiba asili na tiba mbadala, kupitia kikao hiki nawaelekeza wataalamu wetu wajipange kufanya utafiti na kutoa majibu ya tiba ya maambukizi ya virusi vya Corona,” amesema Dkt. Ndugulile.

Amesema wamekubaliana na watafiti hao kufanyia kazi maagizo hayo ndani ya muda mfupi na kutoa majibu sahihi ambayo yatasaidia katika mapambano ya ugonjwa wa Corona.

Naye Mkurugenzi Mkuu  wa NIMR, Prof. Yunus Mgaya amesema mapambano dhidi ya ugonjwa Covid-19  ni vita ambayo inapaswa kufanyiwa utafiti ambao utasaidia kupatikana kwa njia sahihi za kukabiliana na maambukizi ya ugponjwa huo.

“Tunafahamu kwamba jamii za kiafrika zina utaalamu katika miti shamba. Katika hili kuna tafiti mbalimbali zinaendelea ili kuchunguza uwezo wa miti shamba kwa lengo la kupunguza makali ya Covid-19.

Mwisho

Jumatano, 29 Aprili 2020

WAGONJWA WAPYA WA CORONA 196 WAONGEZEKA NCHINI

- Hakuna maoni
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akihutubia Wabunge na Wageni mbalimbali waliofika katika hafla ya ugawaji wa magari ya kubebea wagonjwa  50 yaliyotolewa na Wizara ya Afya kwa Mikoa mbalimbali nchini iliyofanyika katika ofisi ya Waziri Mkuu Mlimwa Jijini Dodoma. Kushoto ni Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu

Baadhi ya Wabunge wakiwa kwenye magari ya majimbo yao waliyotolewa na Wizara ya Afya na kukabidhiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi funguo za Magari ya kubebea wagonjwa Mbunge wa Urambo Bi. Magreth Sitta kwa niaba ya wabunge wengine.

Waziri Mkuu Kassim majaliwa akiongeza na Mbunge wa Ulanga Mhe. Goodluck Mlinga wakati wa hafla ya makabidhiano ya magari ya kubebea wagonjwa iliyofanyika ofisini kwa waziri mkuu jijini Dodoma. Katikati ni Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu.

Na WAJMW-Dodoma

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ametangaza ongezeko la wagonjwa wa Corona 196 nchini huku Tanzania Bara ikiwa na Wagonjwa 174 na Zanzibar wagonjwa 22 ambao walitolewa taarifa na Waziri wa Afya Wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid na kufanya idadi ya wagonjwa wa Corona nchini kufikia 480.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema hayo wakati akigawa magari 50 ya kubebea wagonjwa kwa wabunge wa majimbo mbalimbali tukio lililofanyika leo katika ofisi ya Waziri Mkuu iliyopo Mlimwa jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema jumla ya wagonjwa waliopona imeongezeka kutoka 48 hadi kufikia 197, huku Zanzibar waliopona wakiwa 36 na Tanzania bara 83. Pia Waziri Mkuu amesema kumekuwa na ongezeko la vifo vya watu sita (6) na kufanya kuwa na vifo vilivyotoka na Corona nchini kufikia 16.

Kati ya wenye maambukizi 297 waliobaki, 283 wanaendelea vizuri na tiba na kusubiri ufuatiliaji wa afya zao na wengine 14 wako chini ya uangalizi maalumu wa madaktari ambao wanahitaji oksjeni  (Oxygen) ya kuwasaidia kupumua pamoja na wale wenye magonjwa mengine ambayo yamejitokeza kwenye wodi.

Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kuwaondoa washukiwa waliokua karantini ambao walishatimiza siku 14 baada ya uchunguzi wa kiafya kuonekana hawana maambukizi na kuruhusiwa kurudi nyumbani.

Hadi kufikia jana tarehe 28 Aprili, watu 644 wameruhusiwa kutoka karantini katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Arusha, Zanzibar, Kilimanjaro, Mwanza, kagera, Songwe, Kigoma na Dodoma.

Hata hivyo Waziri Mkuu amekemea tabia ya upotoshaji na utoaji wa takwimu ambazo sio rasmi na kuzua taharuki kwa jamii kwamba kila kifo kimetokana na Corona kuwa sio sahihi na kusisitiza kuwa kuna magonjwa mengine ambayo yanaua pia.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zote zinazotolewa na wataalamu wa afya huku Serikali ikiendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuweza kupambana na vita hii ya ugonjwa wa Corona.

Katika makabidhiano hayo ya magari, Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya  imetoa magari 50 nchiniyenye Tsh. Bilioni 6 ili yaweze kuwezesha rufaa za akinamama Wajawazito na kuepusha vifo vitokanavyo na uzazi pamoja na kukabiliana na magonjwa ya milipuko kama Corona.

Magari 18 yamepekwa katika Hospitali za Rufaa za Mikoa, magari 32 yatatumika kwa ajili ya vituo vya afya na Hospitali za Wilaya.

Aidha, Waziri Ummy amemshukuru Waziri Mkuu kwa kutoa ushirikiano mkubwa unaoutoa kwa Wizara ya Afya kwa kuwezesha mambo mbalimbali lengo likiwa ni kufikisha huduma bora za afya kwa wananchi wote.



Ijumaa, 24 Aprili 2020

WAGONJWA 37 WA CORONA WAPONA NA KURUHUSIWA HUKU 71 WAKISUBIRI VIPIMO VYA MWISHO

- Hakuna maoni


Na.WAMJW-Dar es Salaam

Wagonjwa 37 waliokuwa wameambukizwa virusi vya Corona (COVID-19) wamepona na kuruhusiwa kurejea nyumbani baada ya vipimo vya mwisho kuthibitisha kwamba hawana maambukizi ya COVID-19.

Hayo yamesemwa leo  na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akipokea msaada wa sabuni na fedha kutoka kampuni ya Azania group ya jijini hapa

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa wagonjwa hao 37 ni kati ya wagonjwa 108 waliothibitika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona lakini hivi sasa hawana dalili zozote za ugonjwa kama homa, mafua na kikohozi.

“Watu hawa 108 hawana dalili zozote za ugonjwa kama vile homa au mwili kuchoka isipokuwa wapo katika vituo vya matibabu kusubiri vipimo vya mwisho ili kuthibika kwamba hawana virusi vya corona kabla ya kuruhusiwa kutoka vituoni, hivyo wamepona na wameruhusiwa kurejea nyumbani,” amesema Waziri wa Afya.

Waziri Ummy Mwalimu amewataka watu waliopona ugonjwa huo kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya ili kujikinga na maambukizi mapya ya COVID-19 kwani zipo tafiti zilizofanyika nchi mbalimbali ikiwamo China zimeonyesha kuwa watu wanaweza kupata  maambukizi mapya kama asilimia 14.

“Tunapenda kuwahimiza watu waliopona watoe elimu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona (COVID-19) kwa jamii. Pia, Nitumie fursa hii kwa niaba ya Serikali  kutoa shukrani zetu za thati kwa watumishi wa afya kwa kuendelea kutoa huduma kwa watu wenye maambukizi ya COVID-19. Asanteni sana watumishi wa afya,” amesema Waziri.

Waziri pia ametoa wito kwa watumishi wa afya kuendelea kutoa huduma za afya kwa watu wote wanaohitaji huduma za matibabu wakiwamo wenye dalili za ugonjwa wa Corona.

“Tumeona kumeanza tabia ambayo ni kinyume na taratibu za afya, hatutakiwi kuwakataa wagonjwa wenye dalili za maambukizi ya virusi vya Corona. Nasisitiza kwamba watumishi wa afya wanakumbushwa kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia nwongozo wa Taifa wa kudhibiti maambukizi (National Infection Prevention and Control Guidelines for Health care Services in Tanzania) wa Juni, 2018 pamoja na mwongozo wa Menejimenti ya Matibabu ya Ugonjwa wa COVID-19 wa Januari, 2020 ili kujikinga na maambukizi wakati wa utoaji wa huduma kwa wagonjwa,” amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Wakati huo  Waziri Ummy Mwalimu ameishukuru kampuni ya Azania group kwa msaada wa sabuni 300 na fedha shilingi milioni 50 kwa ajili ya mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Msaada huo utatumika kwa chakula cha wagonjwa na usafi kwenye vituo vya tiba cha Temeke,Amana na Kisoka-Mloganzila.

Jumatano, 4 Machi 2020

WAZIRI UMMY ATOA MASAA KWA HALMASHAURI ZOTE KUTENGA SEHEMU ZA KUWEKA WASHUKIWA WA CORONA

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akiongea wakati akifungua mafunzo ya jinsi ya kuepuka maambukizi ya Virusi vya Corona kwa viongozi wa dini mbalimbali waliojitokeza katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa Maafa kutoka Wizara ya Afya Dkt. Elias Kwezi akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa viongozi wa dini kuhusiana na jinsi ya kuepuka maambukizi ya ugonjwa wa Corona usiingie nchini.
Mwakilishi mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Tigest Katisela akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa viongozi wa dini kuhusiana na jinsi ya kuepuka maambukizi ya ugonjwa wa Corona usiingie nchini.



Baadhi ya viongozi wa dini waliofika katika mafunzo ya jinsi ya kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa Corona unaoendelea kusambaa duniani. Mafunzo hayo yameandaliwa na Wizara ya Afya na kushirikisha viongozi wa dini mbalimbali nchini.
Picha ya pamoja ya Waziri Ummy Mwalimu akiwa na viongozi wa dini na wadau mbalimbali wa maendeleo waliofika katika mafunzo ya namna ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona yanayofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar Es Salaam.
Na Emmanuel Malegi-DSM

Waziri Ummy Mwalimu ametoa masaa 5 kwa kila Halmashauri kutenga sehemu maalum kwaajili ya kumuweka mshukiwa wa ugonjwa wa Corona na kufanya utaratibu wa uchunguzi na kutoa taarifa haraka Wizara ya Afya.

Waziri Ummy ametoa kauli hiyo wakati akifungua mafunzo kwa viongozi wa dini nchini jinsi ya kuepuka maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo vinazidi kusambaa katika nchi mbalimbali duniani.

 "Ninatoa muda mpaka saa 10 jioni vituo vyote vya afya vya umma nchini viwe vimetenga sehemu maalum ya kuweka mshukiwa wa Virusi vya Corona na kuripoti haraka iwezekanavyo katika Wizara ya Afya kwa ajili ya kuchukua hatua stahiki". Amesema Mhe. Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy amesema mpaka sasa nchi yetu ni salama, hakuna mshukiwa wa COVID19 lakini Serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kudhibiti ugonjwa huu usiingie nchini ikiwa ni pamoja na kushirikisha taasisi mbalimbali za dini.

"Tunawaomba viongozi wa dini muende mkatoe elimu kwa waumini wenu kuchukua tahadhari kwa kuzingatia kanuni za usafi na pia kukaa mbali na mtu mwenye dalili za mafua ambaye ana historia ya kusafiri nje ya nchi". Mhe. Ummy.

Aidha, Waziri Ummy ametoa maelekezo kwa taasisi za dini, taasisi za umma, maofisi na mashule ya Serikali na binafsi kuweka sehemu maalum ya kunawa mikono kwa maji yenye dawa ya kuua bakteria (hand sanitizers) ili kuepuka maambukizi yatokanayo na bakteria.

-MWISHO-

Ijumaa, 31 Januari 2020

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA UNAOSABABISHWA NA KIRUSI CHA CORONA (Novel Corona Virus 2019-nCoV) ULIOIKUMBA NCHI YA CHINA NA MATAIFA MENGINE DUNIANI.


                      Bofya hapa kupata kiunganishi cha Tamko kuhusu Virusi vya Corona