Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Matukio. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Matukio. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 29 Novemba 2019

VIONGOZI WA DINI WASAINI MAAZIMIO YA MAPAMBANO DHIDI YA KIFUA KIKUU

- Hakuna maoni
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongea viongozi wa dini (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa viongozi wa dini wa Taifa na wa kanda ya ziwa ambapo viongozi hao walitia saini maazimio ya mapambano dhidi ya kifua kikuu jijini Mwanza

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee naWatoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea wakati wa mkutano wa viongozi wa dini ambapo alisema wanayo imani na viongozi wa dini kwani wanawafikia wananchi wengi.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akiwakaribisha viongozi mbali mbali wa Serikali Wakitaifa, Viongozi wa Dini na Viongozi wa Taasisi zisizo Zakiserikali na wageni wengine katika Mkoa wa Mwanza.

 Meneja Mpango wa Taifa wa kudhibiti Kifua Kikuu (TB) na Ukoma nchini Dkt. Beatrice Mutayoba.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akibadilishana mawazo na Naibu Waziri wa OR-TAMISEMI Josephat Kandege kwenye mkutano wa viongozi wa dini katika vita dhidi ya Kifua Kikuu.

 Viongozi mbalimbali wa dini wakifuatilia mkutano huo ambao umefanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.

 Baadhi ya viongozi wa dini wakimsikiliza mgeni rasmi wakati wa mkutano huo.

Picha ikionesha kuendelea kwa Mkutano wa viongozi wa dini wa Taifa na wa kanda ya ziwa ambapo viongozi hao walitia saini maazimio ya mapambano dhidi ya kifua kikuu jijini Mwanza.

Viongozi wa dini wakisaini maazimio ya kushiriki  mapambano ya kutokomeza  kifua kikuu.Mkutano huo umeandaliwa na Bunge kupitia mtandao wa wabunge wa kupambana na kifua kikuu.

Picha ya Pamoja ikiongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, akiambatana na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda pamoja na Viongozi wengine Wakitaifa na Viongozi wa Dini.


VIONGOZI WA DINI WASAINI MAAZIMIO YA MAPAMBANO DHIDI YA KIFUA KIKUU

Na. Catherine Sungura, wamjw - MWANZA

Serikali ya Tanzania inatenga mabilioni mengi katika kushughulikia masuala ya afya nchini hususani kwenye upande wa tiba ambapo gharama za matibabu zinakuwa kubwa sana.

Hayo yamesemwa leo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai wakati kusaini tamko la maazimio ya viongozi wa dini lililobeba ajenda ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Kifua kikuu (TB) nchini  jijini hapa .

“Wananchi wanadhani kuwa wizara ya afya inasimamia tu tiba, hapana tusisahau kinga ni muhimu sana  dhidi ya magonjwa nchini, tutakaposimamia kinga  serikali itakua inaokoa gharama kubwa kwenye matibabu na pia kupunguza mzigo mkubwa wa kugharamia matibabu kama nchi”Alisisitiza Mhe. Ndugai

Aidha, amewashuru viongozi hao wa dini kwa ahadi pamoja na kusaini azimio  la kusimamia na kusemea kwa waumini  wao suala zima la TB hivyo anayo Imani watalibeba na kulitekeleza na kuwafanya wananchi wengi kupata uelewa juu ya ugonjwa huo na kujitokeza  mapema kwenda kupima afya zao na hivyo kuanza dawa  na  kutoambukiza watu wengine.

Awali akiongea na viongozi hao Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  amesema kuwa Wizara yake  inaendelea kubuni mikakati ya kutokomeza  Tb nchini kama  mikakati Madhubuti yaliyowekwa   kwa mara ya kwanza na baraza kuu la umoja wa mataifa lililokutana Septemba mwaka 2018 na kuweka maazimio na malengo ya  kuongeza kasi ya  kutokomeza TB  ifikapo mwaka 2030.

“Maambukizi mapya ya Tb nchini yamepungua kwa asilimia 18 kulinganisha  na hali ya mwaka 2015 na hivyo kufanya Tanzania  kuwa miongoni  mwa nchi saba  Duniani ambazo zipo katika mwelekeo sahihi wa kufikia malengo ya mpango mkakati wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ya kutokomeza TB kwa hatua ya kwanza ya mwaka 2020.

Aidha, Waziri Ummy amesema  kuwa vifo vitokanavyo na Tb peke yake vimepungua kutoka 30,000 mwaka 2015 hadi 22,000 mwaka 2018 na hii ni sawa na punguzo la asilimia 27,“licha ya mafanikio, nchi bado ina vifo vingi vinavyosababishwa na Tb ambapo kwa sasa takribani watu sitini  hufariki   kila siku hapa nchini”, alisema .

Hata hivyo Waziri huyo wa afya amesema kuwa hadi kufikia mwaka huu serikali ina vituo 103 vinavyotoa huduma za wagonjwa wenye Tb sugu ukilinganishwa na kituo kimoja mwaka 2015  pamoja na uboreshaji wa mifumo ya  uchunguzi  na ugunduzi wa TB kwenye vituo vya  huduma za afya,upanuzi wa matumizi ya hadumini za kisasa za LED na kuongezeka kwa mashine za kisasa zinazopima vimelea vya TB kwa njia ya vina saba za GenXpert zipatazo 238 ambazo kwa sasa zinapatikana kwenye mikoa yote nchini.

MWISHO

Jumanne, 26 Novemba 2019

DKT. CHAULA AFUMUA MFUMO WA UONGOZI WA VYUO VYA MAFUNZO VYA AFYA

- Hakuna maoni
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akifungua Mkutano wa wakuu wa vyuo vya Afya 37 vilivyo chini ya wizara hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mtumba, Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Deodata Makani akifuatilia busara za Katibu Mkuu Wizara ya Afya (Hayupo kwenye picha) wakati wa mkutano wa wakuu wa vyuo vya Afya 37 vilivyo chini ya wizara hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mtumba, Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Grace Magembe akifuatilia, ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa vyuo vya Afya 37 vilivyo chini ya wizara hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mtumba, Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Mafunzo na Rasilimali watu Dkt. Saitore Laizer akiwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango Edward Mbanga katika mkutano wa wakuu wa vyuo vya Afya 37 vilivyo chini ya wizara hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mtumba, Jijini Dodoma.

Prof. Andrea Pembe, wakwanza kushoto akiwa na baadhi ya Wakuu wa vyuo vya Afya na baadhi ya Viongozi katika Sekta ya Afya wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa vyuo vya Afya 37 vilivyo chini ya Wizara ya Afya, uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mtumba, Jijini Dodoma.

Baadhi ya Wakuu wa vyuo vya Afya vilivyo chini ya wizara wakifuatilia maelekezo kutoka kwa Katibu mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula (hayupo kwenye picha)wakati wa ufunguzi wa  mkutano wa wakuu wa vyuo vya Afya 37 vilivyo chini ya wizara ya Afya.

Wakuu wa Vyuo vya Afya 37 pamoja na baadhi ya viongozi katika Sekta ya Afya, wakifuatilia taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya,  wakati wa mkutano wa wakuu wa vyuo vya Afya uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mtumba, Jijini Dodoma.

DKT. CHAULA AFUMUA MFUMO WA UONGOZI WA VYUO VYA MAFUNZO VYA AFYA

Na WAMJW-DOM

Katibu mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula amefumua mfumo  wa uongozi katika vyuo vya Afya nchini na kuunganisha  vyuo vyote vilivyokaribu na hivyo kufanya vyuo kupungua idadi kutoka vyuo 37 hadi kufikia vyuo 9, hali itayosaidia matumizi mazuri ya rasilimali chache zilizopo katika kuzalisha rasilimali watu.

Hayo yamejiri wakati wa mkutano wa wakuu wa vyuo vya Afya 37 vilivyo chini ya wizara hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mtumba, Jijini Dodoma.

“Wizara imeona ili kuboresha utoaji taaluma katika vyuo vyake ni vyema kubadilisha mfumo uliopo wa kuendesha vyuo vidogovidogo na kutengeneza mazingira ya kuwa na vyuo vikubwa vichache vyenye mfumo mzuri wa kiuongozi ili kuzalisha Wataalamu sahihi”, alisema.

Dkt. Chaula amesema kuwa, lengo la mkutano huo ni kupanga jinsi ya  kuboresha taaluma ndani ya vyuo vya Afya nchini ili kutoa Watumishi bora zaidi jambo litakalosaidia kupunguza vifo visivyokuwa vya lazima kwa kiasi kikubwa.

Mbali na hayo Dkt. Chaula amesema kuwa, mfumo bora wa utawala vyuoni  ni muhimili mkubwa na wa msingi katika kuhakikisha mafunzo bora yanatolewa katika vyuo vyetu na wahitimu wanaozalishwa kutoka vyuo hivyo wana umahiri unaokusudiwa katika kutoa huduma za Afya kwa wananchi.

Aliendelea kusema, Wizara imekiri kupokea changamoto za uendeshaji wa mafunzo vyuoni, ikiwemo uchache wa watumishi vyuoni, vifaa vya kufundishia, viwango vya ubora wa wahitimu kushuka, huku akisisitiza mabadiliko ya mfumo wa uongozi yatakuwa chachu ya utatuzi wa changamoto hizo.

Mbali na hayo, Dkt. Chaula amewaasa Viongozi wapya kushughulikia changamoto ya malalamiko kutoka kwa wazazi na wanafunzi wanaosoma vyuoni ikiwemo kukosa kwa baadhi ya haki zao, hali iliyopelekea kwa baadhi ya vyuo kupoteza uaminifu kwa wanafunzi na wazazi.

Nae, Mkurugenzi wa Mafunzo na Rasiliamali  Watu Dkt. Saitore Laizer ametoa wito kwa Wakuu wapya wa vyuo hivyo kufanya kazi kwa ushirikiano baina yao, jambo litalosaidia matumizi mazuri ya rasilimali chache zilizopo katika kuzalisha rasilimali watu.

MWISHO.

Jumatano, 3 Julai 2019

SERIKALI YAJIIMARISHA KUIMALIZA DENGUE

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (aliyevaa buti) akiambatana na Mkuu  wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia  Mjema pamoja na Mbunge wa Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu, wakiwa katika  zoezi la upuliziaji wa viuadudu katika mazalia ya mbu, eneo la Mchikichini Manispaa ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (aliyevaa buti) akiongozana na Mkuu  wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia  Mjema pamoja na Mbunge wa Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu, wakielekea katika  zoezi la upuliziaji wa viuadudu katika mazalia ya mbu, eneo la Mchikichini Manispaa ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam.

Iliyobebwa ni moja kati ya mashine mpya 14 za kupuliza dawa (motorised sprayers) zilizonunuliwa na Manispaa ya Ilala ikiwa ni moja ya jitihada yakupambana dhidi ya ugonjwa wa homa ya Dengue katika Manispaa hiyo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongoza zoezi la upuliziaji wa viuadudu katika mazalia ya mbu, katika eneo la Mchikichini Manispaa ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (aliyevaa buti) akiambatana na Mkuu  wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia  Mjema pamoja na Mbunge wa Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu, wakinyunyiza dawa katika mazalia ya mbu, eneo la Mchikichini Manispaa ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam.

Baadhi ya mtaro katika eneo la Ilala Mchikichini Jijini Dar es salaam, ambao ni moja ya sababu ya mazalia ya mbu wanaosababisha ugonjwa wa homa ya Dengue


Na WAMJW- DSM 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. @ummymwalimu leo amefanya ziara katika eneo la Mchikichini Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam kukagua utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa kwa Mikoa/Halmashauri ya kupambana dhidi ya ugonjwa  wa Dengue.

Kwa kiasi kikubwa Waziri @ummymwalimu ameridhishwa na hatua walizochukua na Manispaa ya Ilala ikiwemo kununua mashine mpya 14 za kupuliza dawa (motorised sprayers), kununua Viuadudu kutoka kiwandani Kibaha lita 3,980 (shs 53m) na kununua lita 210 za kuua mbu wapevu. Huku upuliziaji ukiendelea ktk kata 25.

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa, Matokeo ya jitihada hizi yanaoneka, huku Idadi ya wagonjwa wa Dengue Wilaya ya Ilala ikipungua kutoka wagonjwa 527 mwezi Mei 2019  hadi wagonjwa 207 mwezi June 2019. 

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa, katika Jiji zima la Dar es Salaam wagonjwa wa homa  ya Dengue wamepungua kutoka 2,759 mwezi Mei 2019 hadi wagonjwa 790 mwezi June.

Mbali na hayo, Waziri Ummy amewataka wananchi kushiriki kikamilifu ktk kutokomeza mazalia  ya mbu, kwa kufanya usafi katika maeneo yanayowazunguka, kupulizia dawa maeneo yote yenye mazalia ya mbu,  pia kutumia chandarua chenye dawa wakati wote.

Mwisho.

Ijumaa, 23 Novemba 2018

MATUKIO KATIKA PICHA, ZIARA YA DKT. NDUGULILE MKOANI KILIMANJARO.

- Hakuna maoni
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile jana Novemba 22, 2018 ameanza ziara yake ya kikazi kwa Mkoa wa Kilimanjaro.

Akiwa mkoani kilimanjaro jana alifika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na kupokelewa na mwenyeji wake Bi.Anna Mghwira  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ambapo alipata taarifa ya Mkoa huku sekta ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na kisha kuendelea na ziara yake katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi pamoja na Hospitali ya Rufaa na Kanda ya Kaskazini ya KCMC. yafuatayo ni matukio katika picha kama yalivyojiri.




Dkt, Ndugulile (kushoto) akisalimiana na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bi. Anna Mghwira (kulia)
Dkt, Ndugulile (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kippi Warioba kati kati ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bi. Anna  Mghwira


Dkt. Ngugulile (aliyesimama) akizungumza na waganga wakuu wa wilaya pamoja na wakurugenzi katika zoezi la ugawaji vyeti vya ubora kwa kwa Hospitali na Vituo vya afya vilivyopo Mkoani Kilimanjaro.



Dkt. Ndugulile (Kushoto) akitoa cheti cha ubora kwa Hospitali ya Mt. Joseph iliyotunukiwa hadhi ya nyota nne.



Dkt. Ndugulile (Kushoto) akitoa cheti cha ubora kwa Kituo cha afya cha Moshes kilichotunukiwa hadhi ya nyota nne.

Dkt. Ndugulile (Kushoto) akitoa zawadi ya ngao kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha Bw. Valerian Juwal kwa kuongoza Mkoani Kilimanjaro kuwa na Vituo bora vya afya.

Dkt. Ndugulile (kushoto) akiwa ameshika vipeperushi vya elimu ya afya kwa umma vilivyokuwa vimewekwa sehemu isiyo rasmi na kuuagiza uongozi wa Hospitali ya Mawenzi kuhakikisha ndani ya wiki moja vipeperushi hivyo vitolewe kwa wananchi kwa lengo la kuelimishwa, aliye kulia ni Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro- Mawenzi dkt. Japhet Boniphace.

Dkt. Ndugulile akikagua jokofu linalotunza dawa za Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro, Mawenzi.

Dkt. Ndugulile(kushoto) akikagua nyaraka za kitengo cha maabara ambapo amewaagiza watumishi wote hospitalini hapo kuandika rekodi muhimu zote za wagonjwa wakiwa hospitalini.

Ukaguzi ukiendelea....

Dkt Ndugulile (aliyesimama kulia) akizungumza na wananchi waliofika katika Hospitali ya Mawenzi kupata huduma za matibabu.

Dkt. Ndugulile akifurahi mara baada ya kukutana na Mzee franley Mnzava mwenye umri wa Miaka 98 aliyefika Hospitali ya Mawenzi kupata matibabu. Licha ya umri mkubwa alionao Mzee Mnzava bado yu mwenye nguvu na mcheshi muda wote ambapo amewasihi vijana kutunza miili yao ili kuishi miaka mingi.

Dkt, Ndugulile akikagua ramani ya jengo la kituo cmaalum cha uangalizi wa magonjwa ya mlipuko kinachojengwa pembeni ya Hospitali ya mawenzi kinachotarajiwa kukamilika mwezi Machi 2019.

Dkt. Ndugulile akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro.

Dkt. Ndugulile akipokelewa na mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini Dkt. Gileard Masenga.

Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akihojiana na Bw. Longini Mtalo, Mteknolojia kutoka kituo cha utengenezaji wa viungo bandia katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC  huku akiwa ameshika sampuli ya kiungo bandia kilichotengenezwa na kituo hicho.
wanafunzi wakiwa katika mafunzo ya vitendo kwenye Kituo cha utengenezaji wa viungo bandia katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini.


Mafuta Maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi yanayotengenezwa na Kituo cha Kilimanjaro Sunscreen Production Unit ndani ya Hospitali ya KCMC, mafuta haya huwaliwa walemavu wa ngozi dhidi ya jua kali linalodhuru ngozi ya miili yao.

Dkt. Ndugulile akizungumza jambo huku akiwa amebeba mafuta maalum kwa ajili ya wenye ulemavu wa ngozi yanayotumika kuwakinga dhidi ya jua kali.