Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile jana Novemba 22,
2018 ameanza ziara yake ya kikazi kwa Mkoa wa Kilimanjaro.
Akiwa mkoani kilimanjaro jana
alifika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na kupokelewa na mwenyeji
wake Bi.Anna Mghwira Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro
ambapo alipata taarifa ya Mkoa huku sekta ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto na kisha kuendelea na ziara yake katika Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi pamoja na Hospitali ya Rufaa na Kanda ya Kaskazini
ya KCMC. yafuatayo ni matukio katika picha kama yalivyojiri.
Dkt, Ndugulile (kushoto) akisalimiana na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bi. Anna Mghwira (kulia)
Dkt, Ndugulile (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kippi Warioba kati kati ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bi. Anna Mghwira
Dkt. Ngugulile (aliyesimama) akizungumza na waganga wakuu wa wilaya pamoja na wakurugenzi katika zoezi la ugawaji vyeti vya ubora kwa kwa Hospitali na Vituo vya afya vilivyopo Mkoani Kilimanjaro.
Dkt. Ndugulile (Kushoto) akitoa cheti cha ubora kwa Hospitali ya Mt. Joseph iliyotunukiwa hadhi ya nyota nne.
Dkt. Ndugulile (Kushoto) akitoa cheti cha ubora kwa Kituo cha afya cha Moshes kilichotunukiwa hadhi ya nyota nne.
Dkt. Ndugulile (Kushoto) akitoa zawadi ya ngao kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha Bw. Valerian Juwal kwa kuongoza Mkoani Kilimanjaro kuwa na Vituo bora vya afya.
Dkt. Ndugulile (kushoto) akiwa ameshika vipeperushi vya elimu ya afya kwa umma vilivyokuwa vimewekwa sehemu isiyo rasmi na kuuagiza uongozi wa Hospitali ya Mawenzi kuhakikisha ndani ya wiki moja vipeperushi hivyo vitolewe kwa wananchi kwa lengo la kuelimishwa, aliye kulia ni Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro- Mawenzi dkt. Japhet Boniphace.
Dkt. Ndugulile akikagua jokofu linalotunza dawa za Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro, Mawenzi.
Dkt. Ndugulile(kushoto) akikagua nyaraka za kitengo cha maabara ambapo amewaagiza watumishi wote hospitalini hapo kuandika rekodi muhimu zote za wagonjwa wakiwa hospitalini.
Ukaguzi ukiendelea....
Dkt Ndugulile (aliyesimama kulia) akizungumza na wananchi waliofika katika Hospitali ya Mawenzi kupata huduma za matibabu.
Dkt. Ndugulile akifurahi mara baada ya kukutana na Mzee franley Mnzava mwenye umri wa Miaka 98 aliyefika Hospitali ya Mawenzi kupata matibabu. Licha ya umri mkubwa alionao Mzee Mnzava bado yu mwenye nguvu na mcheshi muda wote ambapo amewasihi vijana kutunza miili yao ili kuishi miaka mingi.
Dkt, Ndugulile akikagua ramani ya jengo la kituo cmaalum cha uangalizi wa magonjwa ya mlipuko kinachojengwa pembeni ya Hospitali ya mawenzi kinachotarajiwa kukamilika mwezi Machi 2019.
Dkt. Ndugulile akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro.
Dkt. Ndugulile akipokelewa na mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini Dkt. Gileard Masenga.
Dkt.
Faustine Ndugulile (kushoto) akihojiana na Bw. Longini Mtalo, Mteknolojia
kutoka kituo cha utengenezaji wa viungo bandia katika Hospitali ya Rufaa ya
Kanda ya Kaskazini KCMC huku akiwa ameshika sampuli ya kiungo bandia
kilichotengenezwa na kituo hicho.
wanafunzi wakiwa katika mafunzo ya vitendo kwenye Kituo cha utengenezaji wa viungo bandia katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini.
Mafuta Maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi yanayotengenezwa na Kituo cha Kilimanjaro Sunscreen Production Unit ndani ya Hospitali ya KCMC, mafuta haya huwaliwa walemavu wa ngozi dhidi ya jua kali linalodhuru ngozi ya miili yao.
Dkt. Ndugulile akizungumza jambo huku akiwa amebeba mafuta maalum kwa ajili ya wenye ulemavu wa ngozi yanayotumika kuwakinga dhidi ya jua kali.
0 on: "MATUKIO KATIKA PICHA, ZIARA YA DKT. NDUGULILE MKOANI KILIMANJARO."