Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee hma Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya Madaktari wa Afya ya kinywa na meno (hawapo kwenye picha) wakati akifungua mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Baadhi ya Madaktari na Wadau wa Afya ya kinywa na meno wakifuatilia kwa umakini hotuba ya mgeni rasmi, Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya (hayupo kwenye picha) wakati wa mkutano wa mwaka wa madaktari wa Afya ya kinywa na meno uliofanyika mkoa wa Mara.
Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa Madaktari wa Afya ya kinywa na meno uliofanyika mkoa wa Mara.
Na WAMJW - MARA.
WAZIRI wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amemwagiza Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya kuhakikisha kuwa kabla ya Machi 30, 2019
Hospitali zote za Mikoa kutoa Huduma za matibabu ya kinywa.
Ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa
Madaktari wa Kinywa wenye lengo la kujadili njia bora za kuboresha huduma za
Afya ya kinywa na meno na namna ya kuikuza kada hiyo, tukio lililofanyika
katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Waziri Ummy alisema kuwa "hatuwezi kusema kuwa afya ya
kinywa na meno ni muhimu alafu leo ni hospitali za rufaa za Mikoa 10 kati ya 28 ndio zinavitendea kazi"
alisema Waziri Ummy.
Pia Waziri Ummy aliwahasa Wananchi kupambana dhidi ya
magonjwa ya kinywa na meno kwa kujiepusha matumizi ya sigara, tumbaku, unywaji
wa pombe kupita kiasi, ulaji wa vyakula na vinywaji vyenye sukari.
"Magonjwa ya kinywa na meno yana visababishi vyake
ikiwemo uvutaji wa sigara,sigara, tumbaku, unywaji wa pombe kupita kiasi, ulaji
wa vyakula na vinywaji vyenye Sukari" alisema Waziri Ummy
Kwa upande mwingine Mhe. Ummy amewataka madaktari wa kinywa
na meno kuwahamasisha wananchi ili kufahamu umuhimu wa kupiga mswaki japo mara
mbili kwa siku ili kujiepusha katika hatari yakupata magonjwa ya kinywa na
meno.
"Mnatuambia kwamba angalau tupige mswaki mara mbili kwa
siku, hapo mnakazi kubwa sana ya kutushawishi, hivyo niwaombe tushirikiane nasi
ili kuhakikisha kwamba tunaongeza elimu na hamasa kwa jamii katika suala
hiki" alisema Waziri Ummy.
Akiwasilisha taarifa mbele ya mgeni rasmi, Rais wa chama cha
Madaktari wa kinywa na meno Tanzania Dkt. Mwakitobe amesema kuwa idadi ya
Wataalamu wa Afya ya kinywa na meno bado ni ndogo sana ukilinganisha uwiano wa
watoa huduma na wagonjwa hali inayopunguza ufanisi kutokana na kufanya kazi kwa
muda mrefu bila kupumzika.
"Idadi ya Wataalamu wa Afya ya kinywa na meno bado ni
ndogo sana ukilinganisha uwiano wa watoa huduma na wagonjwa. Wataalamu hao no
pamoja na dental therapist, Madaktari wasaidizi wa kinywa na Meno, Wataalamu wa
maabara wa kinywa na meno, mafundi wa vifaa na vifaa tiba vya kinywa na meno,
Madaktari wa kinywa na meno na Wabobezi kwenye maeneo hayo ya kinywa na
meno" alisema Dkt. Mwakitobe.
Dkt. Mwakitobe aliendelea kusema kuwa tafiti za hivi karibuni zinonesha uhusiano mkubwa wa magonjwa ya kinywa na meno na magonja yasiyo yakuambukiza kama vile kisukari, ugonjwa wa moyo Saratani na hata magonjwa ya HIV/AIDS.
Kwa upande mwingine Dkt. Mwakitobe alisema kuwa Huduma za
msingi za kinywa na meno zinahitaji ushiriki mkubwa wa kila mtaalamu wa fani
hiyo ya kinywa na meno, pamoja na kundi la wauguzi wa kinywa na meno, ambapo
kwa sasa nchi yetu haina chuo kinachotoa mafunzo ya fani ya kinywa na meno.
Aidha, Dkt. Mwakitobe alisema kuwa idadi ya Madaktari bingwa
wa kinywa na meno bado no chache na licha ya uhaba uliopo bado hawapati
kipaumbele cha kujiendeleza.
"Katika kipindi cha masomo cha mwaka 2018/2019
kipaumbele hakikutolewa kwa waombaji wanaodahiliwa katika fani za uzamili
kwenye masomo ya Afya ya kinywa na meno kwani kada hiyo ni muhimu na inasaidia
wananchi kama kada nyingine za Afya" alesema Dkt. Mwakitobe.
Mwisho.
0 on: "WAZIRI UMMY AAGIZA HOSPITALI ZOTE ZA RUFAA ZA MIKOA KUTOA MATIBABU YA KINYWA NA MENO. "