Wakurugenzi mbalimbali
kutoka wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
wakimsikiliza Waziri wa wizara hiyo Mhe. Ummy Mwalimu (Hayupo Pichani) katika mkutano
wa mwaka wa wadau wa sekta ya afya wa kujadilia njia zitakazowezesha kufikia
malengo na vipaumbele vya kisera vya mwaka 2019/2020 uliofanyika jijini Dodoma.
WADAU WA SEKTA
YA AFYA KUENDELEA KUBORESHA UTOAJI WA HUDUMA NCHINI
NA
WAJMW-DODOMA
Serikali kupitia
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inaendelea
kuboresha huduma afya nchini kwa kukarabati vituo vya afya vipatavyo 350 ili utoaji wa huduma za afya ya mama na mtoto
hususani huduma za dharura wakati wa
kujifungua.
Hayo yamesemwa
leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wa mwaka wa
wadau wa sekta ya afya wa kujadilia njia zitakazowezesha kufikia malengo na
vipaumbele vya kisera vya mwaka 2019/2020 uliofanyika mapema jijini Dodoma.
“Sekta ya
afya tunaona inaendelea kupiga hatua kubwa sana katika maeneo mbalimbali
ikiwemo suala la kuimarisha miundombinu ambapo vituo vya Afya takribani 350
vimekarabatiwa kwa kuongeza miundombinu
kwa ajili ya kutoa huduma za afya za dharura ikiwemo huduma za kumtoa mtoto
tumboni”.
Waziri Ummy
amesema serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo duniani inahakikisha
sekta ya afya inapata mafanikio kwa kuboresha huduma nchini ikiwemo na kufikia
asilimia zaidi ya 90 ya dawa zinapatikana katika sehemu zote za kutoa huduma.
Aidha,
Waziri Ummy amesema mkutano huo ulikua na lengo la kukubaliana kutekeleza
vipaumbele nane (8) ambavyo serikali pamoja na wadau wa maendeleo itahakikisha
vinatekelezwa ipasavyo katika mwaka 2019/2020.
Maeneo hayo
ni pamoja na Kuimarisha huduma za afya ya uzazi ,mama na mtoto ikiwa ni pamoja
na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi, kwa kuweka miundombinu ya huduma za
uzazi wa dharura na watoto wachanga kwani kwa takribani hivi sasa watoto
wachanga wapatao elfu tisini hufariki ndani ya siku ishirini na nane (28) za
mwanzo. Kuongeza huduma za uzazi salama sambamba na uzazi wa mpango, kupunguza
maambukizi ya UKIMWI kutoka mama kwenda kwa mtoto.
Eneo la pili
linahusu Afya za wasichana na wavulana walio katika umri wa kubalehe ikiwa ni
pamoja na kutoa elimu ya kuepuka ngono katika umri mdogo na mimba
zisizotarajiwa.
Alitaja eneo
jingine ni kuongeza nguvu kazi katika
sekata ya afya ikiwa ni pamoja na kuajiri watumishi wa afya katika ngazi zote,
kuongeza ujuzi kwa kutoa nafasi za kusomesha watumishi ili kukidhi vigezo
vilivyoweka na shirika la afya duniani (WHO).
Kipaumbele cha
Nne, ni kuimarisha ubora wa huduma za afya utakaoenda sambamba na uboreshaji wa
miundombinu ya sehemu za kutolea huduma za afya za serikali pamoja na kuongeza
rasilimali fedha kwa ajili ya kutatua changamoto za afya kwa kuongeza ya bajeti ya afya kutoka
kutoka Bilioni 31 hadi Bilioni 270 mwaka 2018/2019.
Naye Naibu
katibu Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia afya dkt.Zainabu Chaula amesema kwamba
wao kama sehemu ya utekelezaji wamejipanga kutekeleza maboresho ya afya ngazi
ya msingi kuanzia vijijini hadi Taifa kupitia sera ya afya hivyo wamejipanga
kuongeza kutoa elimu ya afya kwa umma kuanzia zahanati kwa kupanga mipango endelevu ili iende
sambamba kuanzia ngazi husika kwa kutumia kamati za afya kwenye vituo vya
kutolea huduma za afya nchini.
|
0 on: "WADAU WA SEKTA YA AFYA KUENDELEA KUBORESHA UTOAJI WA HUDUMA NCHINI"