TAASISI YA MIFUPA (MOI) YATAKIWA
KUWASILIANA NA WATEJA KWA KWA NJIA YA SIMU
Na.WAMJW,Dar
es Salaam
Taasisi ya mifupa (MOI) imetakiwa kuanzia leo
kuwasiliana na wateja wao kwa njia ya simu pale panapotokea mabadiliko ya watoa
huduma kutokuwepo mahali pa kazi ilikuepusha usumbufu wa kukaa hospitalini muda
mrefu.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati alipofanya
ziara katika taasisi hiyo na kukuta wagonjwa wakisubiri kwa muda mrefu kupata matibabu
pamoja na vipimo.
Dkt. Mpoki alisema alichokiona kwenye taasisi
hiyo ni mawasiliano ambayo inasababisha wagonjwa wengi kutokupata taarifa za kutokuwepo
kwa madaktari wao hivyo kufanya wagonjwa kusubiri kwa muda mrefu.
“kuanzia leo taasisi hii itawasiliana nanyi kila
inapotokea changamoto inayofanya mabadiliko ya mida yenu na madaktari, mtapigiwa
simu sasa wewe utafanya maamuzi yakuja au kusubiri hadi muda ulioambiwa ili uonane
na daktari wako muda utakaombiwa”. Alisema Dkt. Mpoki.
Aidha, aliwataka madaktari na wauguzi wawe wanawajulisha
wagonjwa mapema wao kwa wale wenye simu kwani kwenye kila jarida la mgonjwa huwa
wanaandika namba za simu za wateja wao.
Hata hivyo Dkt. Mpoki alisema hii ni kutokana
na mkakati wa Serikali wakutatua changamoto za wananchi wanaofika kupata matibabu
kwenye taasisi zake na hivyo kuboresha huduma kwa wahitaji kadri ya uwezo unavyopatikana.
Katibu Mkuu huyo alifanya ziara katika taasisi
hiyo kwa kutembelea idara ya Mionzi, wagonjwa wa nje pamoja na kuongea na wagonjwa
waliofika kupata matibabu katika hospitali hiyo.
-Mwisho-
0 on: "TAASISI YA MIFUPA (MOI) YATAKIWA KUWASILIANA NA WATEJA KWA NJIA YA SIMU"