Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (aliyevaa buti) akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema pamoja na Mbunge wa Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu, wakiwa katika zoezi la upuliziaji wa viuadudu katika mazalia ya mbu, eneo la Mchikichini Manispaa ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (aliyevaa buti) akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema pamoja na Mbunge wa Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu, wakielekea katika zoezi la upuliziaji wa viuadudu katika mazalia ya mbu, eneo la Mchikichini Manispaa ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam.
Iliyobebwa ni moja kati ya mashine mpya 14 za kupuliza dawa (motorised sprayers) zilizonunuliwa na Manispaa ya Ilala ikiwa ni moja ya jitihada yakupambana dhidi ya ugonjwa wa homa ya Dengue katika Manispaa hiyo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongoza zoezi la upuliziaji wa viuadudu katika mazalia ya mbu, katika eneo la Mchikichini Manispaa ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (aliyevaa buti) akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema pamoja na Mbunge wa Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu, wakinyunyiza dawa katika mazalia ya mbu, eneo la Mchikichini Manispaa ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam.
Baadhi ya mtaro katika eneo la Ilala Mchikichini Jijini Dar es salaam, ambao ni moja ya sababu ya mazalia ya mbu wanaosababisha ugonjwa wa homa ya Dengue
Na WAMJW- DSM
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. @ummymwalimu leo amefanya ziara katika eneo la Mchikichini Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam kukagua utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa kwa Mikoa/Halmashauri ya kupambana dhidi ya ugonjwa wa Dengue.
Kwa kiasi kikubwa Waziri @ummymwalimu ameridhishwa na hatua walizochukua na Manispaa ya Ilala ikiwemo kununua mashine mpya 14 za kupuliza dawa (motorised sprayers), kununua Viuadudu kutoka kiwandani Kibaha lita 3,980 (shs 53m) na kununua lita 210 za kuua mbu wapevu. Huku upuliziaji ukiendelea ktk kata 25.
Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa, Matokeo ya jitihada hizi yanaoneka, huku Idadi ya wagonjwa wa Dengue Wilaya ya Ilala ikipungua kutoka wagonjwa 527 mwezi Mei 2019 hadi wagonjwa 207 mwezi June 2019.
Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa, katika Jiji zima la Dar es Salaam wagonjwa wa homa ya Dengue wamepungua kutoka 2,759 mwezi Mei 2019 hadi wagonjwa 790 mwezi June.
Mbali na hayo, Waziri Ummy amewataka wananchi kushiriki kikamilifu ktk kutokomeza mazalia ya mbu, kwa kufanya usafi katika maeneo yanayowazunguka, kupulizia dawa maeneo yote yenye mazalia ya mbu, pia kutumia chandarua chenye dawa wakati wote.
Mwisho.
0 on: "SERIKALI YAJIIMARISHA KUIMALIZA DENGUE"