Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumanne, 16 Julai 2019

RAIS MAGUFULI AMWAGIZA WAZIRI UMMY KUFUATILIA MALIPO YOTE YA SERIKALI KWA WAGONJWA WA NJE YA NCHI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuonesha ishara ya uzinduzi rasmi wa miradi 7 yenye jumla ya shilingi Bilion 15 katika Hospitali ya Rufaa ya kanda ya ziwa Bugando. Kulia kwake ni Baba Askofu Mhashamu Askofu Renatus Nkwande huku kushoto kwake ni Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu akifuatiwa na Waziri wa Nishati Medard Kalemani na mwisho ni Naibu  Waziri wa Ardhi Mhe. Angelina Mabula

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimpa mkono Baba Askofu Mhashamu Askofu Renatus Nkwande baada ya kuzindua mradi wa NHIF ikiwa ni moja kati ya miradi 7 iliyozinduliwa yenye jumla ya shilingi Bilion 15 katika Hospitali ya Rufaa ya kanda ya ziwa Bugando.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akieleza jambo wakati wa uzinduzi rasmi wa miradi 7 yenye jumla ya shilingi Bilion 15 katika Hospitali ya Rufaa ya kanda ya ziwa Bugando.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa taarifa ya Wizara ya utekelezaji mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo kwenye picha) wakati wa uzinduzi rasmi wa miradi 7 yenye jumla ya shilingi Bilion 15 katika Hospitali ya Rufaa ya kanda ya ziwa Bugando.

Baadhi ya viongozi wa Serikali wakifuatilia Maelekezo kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo kwenye picha) wakati wa uzinduzi rasmi wa miradi 7 yenye jumla ya shilingi Bilion 15 katika Hospitali ya Rufaa ya kanda ya ziwa Bugando.

Wananchi waliojitokeza kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wwakati wa uzinduzi wa miradi 7 yenye jumla ya shilingi Bilion 15 katika Hospitali ya Rufaa ya kanda ya ziwa Bugando.


Na WAMJW-MWANZA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli amemwagiza Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kufuatilia malipo yote ya Wagonjwa wanoenda kutibiwa nje ya nchi ili kubaini ubadilifu unaofanywa na baadhi ya watu wasiowaaminifu.

Rais Magufuli ameagiza hilo leo wakati akizindua miradi Saba ya huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Ziwa Bugando yenye thamani ya shilingi Bilion15, jambo litalosaidia kurahisisha upatikanaji wa huduma bora kwa ukaribu pamoja na kuokoa kiasi cha fedha miongoni mwa wanaohitaji huduma. 

"Na kwasababu Waziri wa Afya yupo hapa, akafuatilie malipo yote ambayo tunatakiwa kulipa, kule nje , akikuta kunamalipo yakulipa mtu ambae hakuwa mgonjwa aliyejihifadhi huko, akazilipe mwenyewe " alisema Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli 

Rais Magufuli amesema kuwa baadhiya Watendaji waliona kupeleka Wagonjwa nje ya nchi kwaajili ya matibabu ni fursa yakujipatia kipato, jambo lililokuwa linapelekea hasara kubwa kwa nchi ya Tanzania kutokana na malipo kwa baadhiya watu wasiostaholi.

" Hata kupeleka kwa wagonjwa nje kwa Watanzania ilikuwa ni dili, ilikuwa ni fursa kwa Watendaji, wapo watu waliokuwa wanapewa vibali kwenda kutibiwa India lakini anaumwa mafia, ilikusudi apate safari na msindikizaji, bill zote zinaletwa kwa Serikali " alisema Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli 

Dkt. Magufuli aliendelea kusema kuwa ni lazima tujenge nidhamu katika nchi, huku akisisitiza kuwa Serikali haijakataza kupeleka wagonjwa nje ya nchi, huku akisisitiza kuwa wagonjwa wanaostahili kupelekwa kwa matibabu nje ya nchi ni wale walioshindikana ndani ya nchi.

Aidha, Waziri Ummy ameagiza kuboresha uzalishaji wa oksijeni ili kuhakikisha zinazalishwa kwa wingi jambo litalosaidia kuokoa kiwango kikubwa cha mapato kinachopotea kwa kuagiza nje ya nchi, pia itasaidia kuongeza ajira kwa wananchi wa Tanzania. 

"Ninawaomba ndugu zangu, tengenezeni oksijeni nyingi, panueni uzalishaji ili Wizara ya Afya iagize hapa hapa Bugando ili vijana wanaomaliza famasi hapa hapa Bugando wapate ajira hapa yakutengeneza Oksijeni " alisema Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli 

Nae, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu amesema kuwa hadi kufikia juni 30, 2019 Serikali ina jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya vya umma 5756 (71%),Taasisi za Dini 923 (11%) na vituo vya watu binafsi ni 1440 (18%). 

Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa, pia Serikali, ina Jumla ya Vituo vya Afya vya Mashirika ya Dini ikiwemo Hospitali Teule za Wilaya vipatavyo 43, ambazo zinapata ruzuku (OC) kiasi cha shilingi 30,704,000/= kwa mwezi na mishahara kiasi cha Tshs.1.8 bilioni kwa mwezi kwa ajili ya watumishi 2600. 

Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amesema kuwa Serikali imepunguza malalamiko ya upatikanaji wa dawa kwa Wananchi na katika hospitali ya rufaa ya Bugando hii ni kufuatia ongezeko la bajeti ya dawa hadi kufikia Tshs.270 bilioni, huku Serikali ikitoa kiasi cha Tshs. milioni 100 kila mwezi kwa ajili ya kununulia dawa, huku Mwaka 2015/16 walikuwa wanapata Tshs.534 milioni na Mwaka 2018/19 wanapata Tshs.1.5 bilioni.

Naye, Mkurugenzi wa Hospitali ya kanda ya Bugando Prof. Abel Makubi akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, amesema  kwa  kipindi cha miaka minne wamefanikiwa kuboresha huduma za afya na kukamilisha miradi saba ambayo ni  kitengo cha  saratani, mahututi, upasuaji, oksijeni na viwanda vidogo ambavyo vitakuwa vinazalisha dawa kwa ajili ya wagonjwa.

Ameongeza kuwa asilimia 70 ya wagonjwa wa saratani ambao walikuwa wanakwenda katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam walikuwa wanatoka Kanda ya Ziwa, hivyo imewapunguzia gharama na usumbufu wa kusafiri kutafuta huduma hiyo.

#tunaboreshaafya

0 on: "RAIS MAGUFULI AMWAGIZA WAZIRI UMMY KUFUATILIA MALIPO YOTE YA SERIKALI KWA WAGONJWA WA NJE YA NCHI"