Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatano, 24 Julai 2019

BALOZI WA UFARANSA AFURAHISHWA NA HUDUMA ZA CHUO KIKUU CHA AFYA NA SAYANSI MUHIMBILI

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Mikrobiolojia na Immunolojia chuo cha  MUHAS Prof. Said Aboud, wakati alipofanya ziara katika chuo hicho ili kujionea maendeleo ya shughuli zakitafiti katika chuo hicho, Kulia kwa Waziri Ummy ni Balozi wa Ufaransa Tanzania Frederic Clavier na wamwisho ni  Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Andrea Pembe.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akiambatana na Balozi wa Ufaransa Tanzania Frederic Clavier na Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Andrea Pembe, wakwanza  kushoto ni Mtaalamu wa Mikrobiolojia na Immunolojia chuo cha  MUHAS Prof. Said Aboud.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akipokea maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Mikrobiolojia na Immunolojia chuo cha  MUHAS wwakati alipofanya ziara katika chuo hicho ili kujionea Maendeleo ya shughuli zakitafiti katika chuo hicho, Kulia kwake ni Balozi wa Ufaransa Tanzania Frederic Clavier.

Wataalamu mbali mbali wa masuala ya tafiti pamoja na Watumishi wa Sekta ya Afya, wakifuatilia hotuba kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu wakati alipofanya ziara katika chuo cha MUHAS ili kujionea Maendeleo ya shughuli zakitafiti

Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu pamoja na Balozi wa Ufaransa Tanzania Frederic Clavier na Wataalamu mbali mbali wa masuala ya tafiti pamoja na Watumishi wa Sekta ya Afya baada ya ziara ya kujionea Maendeleo ya shughuli zakitafiti katika chuo cha MUHAS.


BALOZI WA UFARANSA AFURAHISHWA NA HUDUMA ZA CHUO KIKUU CHA AFYA NA SAYANSI MUHIMBILI

NA WAJMW-DSM

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Bw. Frederic Clavier amefurahishwa na huduma zinazotolewa katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi cha Muhimbili.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu mapema leo wakati wa kukagua na kufuatilia maendeleo ya ushirikiano kati ya nchi ya Ufaransa na Tanzania katika masuala ya utafiti mafunzo na utoaji wa huduma za Afya katika chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Muhimbili.

Kwa kiasi kikubwa Waziri Ummy pamoja na Balozi huyo wameridhishwa kwa kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Wataalamu katika chuo hicho ikiwemo utafiti, mafunzo na utoaji wa huduma za afya.

“Binafsi tumeridhishwa na kazi kubwa na nzuri zinazofanywa na wataalamu wetu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi cha Muhimbili, katika masuala ya utafiti tumeona kazi kubwa inayofanyika katika utafiti juu ya dawa za kuua wadudu”. Amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema hakuna sheria nzuri za udhibiti wa dawa hizi nchini hivyo Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Muhimbili na Serikali ya Ufaransa itaendelea kufanya utafiti na kuona jinsi gani itapunguza madhara ya utumiaji wa dawa za kuua wadudu kwa binadamu.

Pamoja na hayo, Waziri Ummy amefurahi kuona ushirikiano ambao Serikali ya Ufaransa inaendelea kuutoa katika huduma za watu wenye tatizo la Seli nundu “Sickle Cell".

“kwa Mujibu wa Tafiti tuna jumla ya watu 200,000 nchini ambao wana tatizo la seli nundu na watoto ambao wanazaliwa ni 11,000 kwahiyo tumejadiliana na Serikali ya Ufaransa kuona ni jinsi gani tunaweza kuboresha huduma za ugunduzi ili tuweze kuwatambua mapema watoto pale wanapozaliwa na tatizo hili na kuhakikisha huduma za matibabu zinapatikana ikiwepo dawa ya kupunguza maumivu inapatikana”. Amesema Waziri Ummy.

Kufuatia hatua hiyo Waziri Ummy amemuomba Balozi Frederic kushawishi makampuni makubwa ya  kutengeneza dawa kutoka Ufaransa yaweze kusaidia katika kuzalisha dawa ya kupunguza maumivu ya Seli nundu inapatikana kwa Watanzania wengi.

Mwisho

0 on: "BALOZI WA UFARANSA AFURAHISHWA NA HUDUMA ZA CHUO KIKUU CHA AFYA NA SAYANSI MUHIMBILI"