Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongoza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Mhe. Anthony Mtaka na Watumishi wengine wa Serikali wakati alipofanya ziara ya
kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la
upasuaji na jengo la naabara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akifuatilia kwa makini ramani ya
ujenzi wa jengo la wazazi na jengo la
upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu kutoka kwa Mhandisi kutoka
Wizara ya Afya Bw. Mbuya (Wakulia kwa Waziri Ummy). Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka
(wakwanza kulia) na Watumishi wengine wa Serikali wakati alipofanya ziara ya
kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la
upasuaji na jengo la maabara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu
Moja kati ya mradi wa ujenzi wa jengo
la maabara na jengo la upasuaji ikiwa na gharama ya shilingi Bilion 5.7 ikiwa
katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu
Na WAMJW- SIMIYU
Serikali kupitia Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto yatoa kiasi cha shilingi Bilion 5.7
kwaajili ya ujenzi wa jengo la maabara na jengo la upasuaji ikiwa ni awamu ya
pili, baada yakuzinduliwa kwa awamu ya kwanza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli, Mwezi Agasti 2018.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipofanya
ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la maabara na jengo la upasuaji
katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.
Waziri Ummy amesema kuwa, uwekezaji
huu umeweka alama kubwa kwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Rais
Dkt.John Pombe Magufuli kwa kuwasogezea huduma bora zakibingwa kwa Wananchi wa
Simiyu jambo litalosaidia kuondoa usumbufu katika kutafuta huduma hizo.
"Kipekee kabisa nimshukuru Mhe.
Rais katika mwaka huu 2018/2019 ameipatia Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu
kiasi cha shilingi Bilion 5.7 kwaajili ya ujenzi wa jengo la maabara na jengo
la upasuaji lakini pia litakuwa na huduma za mionzi" alisema Waziri Ummy.
Aidha, Waziri Ummy ameongeza kuwa
Serikali tayari umeshapata kiasi cha shilingi Bilion 2.2 kwaajili ya ujenzi wa
jengo la mama na mtoto ili huduma za kulaza Wagonjwa zianze kutolewa katika
Hospitali hiyo.
"Tuna pesa nyingine kiasi cha
shilingi Bilion 2.2 ukiacha zile Bilion 5.7 tutaanza kujenga jengo la mama na
mtoto ili sasa tuanze kulaza wagonjwa, kwasababu ukiangalia wagonjwa wengi ni
Wanawake na Watoto, lakini hili kingine la wodi nyingine nalibeba pia"
alisema Waziri Ummy.
Mbali na hayo, Waziri Ummy amewaagiza
Watumishi wa Sekta ya Afya kuzingatia maadili na weledi wa kazi zao ikiwemo
matumizi mazuri ya lugha kwa wagonjwa pindi wakiwa kupata huduma za Afya.
"Niinawataka tena Wauguzi
kuzingatia maadili na weledi wa kazi zao ,ikiwemo kutumia lugha nzuri, lugha
yenye busara na lugha yenye upendo kwa wagonjwa, asili ya muuguzi ni upendo na
heshima na kumthamini mtu ambae unampa huduma " amesema Waziri Ummy.
Hata hivyo, Waziri Ummy aliendelea
kusema kuwa Serikali haitokuwa na msamaha na Mtumishi yeyote ambae atabainika
ametoa lugha chafu kwa wagonjwa ikiwemo kujihusisha na masuala ya Rushwa kwa
kuwachukulia hatua kali ikiwemo kufuta reseni zao.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.
Anthony Mtaka amesema kuwa changamoto kubwa ambayo itakuwepo katika ujenzi wa
Hospitali hiyo ni uwepo wa wodi, hivyo amemwomba Waziri Ummy kuharakisha ujenzi
wa wodi ili huduma zianze mara moja.
"Wakati wote tunapokuwa tunakuja
changamoto kubwa ilikuwa ni wodi, na hata wagonjwa wanaokuja wanaulizia kuhusu
wodi za kulala wagonjwa " amesema Mhe. Mtaka.
#tunaboreshaafya
Mwisho .
0 on: "SERIKALI YATOA BILION 5.7 UJENZI WA MAABARA NA JENGO LA UPASUAJI - SIMIYU"