|
Picha ya Juu ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Picha ya Chini ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo wakizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa wa Kitaifa wa Upuliziaji wa dawa za kuua wadudu dhurifu wakiwemo Mbu ili kupunguza Magonjwa ya Malaria na Dengue pamoja na magonjwa Mengine. Uzinduzi huu umefanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar Es Salaam. |
|
Baadhi wa Mabwana Afya kutoka Manispaa mbalimbali za jiji la Dar Es Salaam wakipita mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu kumuonesha zana zinazotumika katika kupuliza dawa za kuangamiza wadudu dhurifu katika hafla ya uzinduzi wa mkakati wa kupuliza dawa ili kutokomeza wadudu dhurifu. |
|
Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa wa Kitaifa wa Upuliziaji wa dawa za kuua wadudu dhurifu wakiwemo Mbu ili kupunguza Magonjwa ya Malaria na Dengue pamoja na magonjwa Mengine. |
|
Baadhi ya mashine za kupulizia dawa za kuua mbu na wadudu dhurifu kwa binadamu zikiwa katika magari tayari kwa ajili ya ufunguzi wa mkakati wa taifa wa kudhibiti wadudu dhurifu. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu mapema leo. |
|
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kushoto) akizindua rasmi mkakati wa upuliziaji dawa kwa ajili ya kutokomeza wadudu dhurifu ikiwemo mbu. Wa pili kulia ni Waziri wa TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo. |
|
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) akiwa na Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo (katikati) mapema leo wakizindua mashine za kupuliza dawa ya kuua mbu na wadudu dhurifu zitakazosambazwa badae kwenye baadhi ya mikoa ikiwemo Tanga na Dar Es Salaam. |
|
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Waziri wa TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo Jafo wakijaribu moja ya mashine za FOG maalumu kwa ajili ya upuliziaji wa dawa za kuua wadudu wadhurifu katika maeneo mbalimbali nchini. |
|
Katibu tawala wa mkoa wa Dar Es Salaam Bw. Abubakar Kinenge (kushoto) akikabidhiwa moja ya mashine za kupuliza dawa za kuua wadudu dharifu na Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo (Kulia) wakati wa uzinduzi wa kitaifa wa mkakati wa kupuliza dawa za kuua wadudu dhurifu wakiwemo mbu na wengineo nchi nzima. |
|
Picha ya Pamoja kati ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa OR-TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo wakiwa na Wakurugenzi na viongozi mbalimbali toka Wizara ya Afya na Serikali ya Mkoa wa Dar Es Salaam wakati wa uzinduzi wa mkakati wa taifa wa kutokomeza wadudu dhurifu uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar Es Salaam.
|
Na.WAMJW-DSM
Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi mahiri wa Mhe. Dkt.John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewekeza vya kutosha katika kudhibiti mbu anayesababisha malaria hali ambayo imepelekea kupungua kwa kiwango cha ugonjwa wa Malaria nchini.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akizindua mkakati wa Taifa wa kudhibiti mbu na wadudu wadhurifu jijini hapa.
“Kiwango cha Malaria nchini kimepungua kutoka asilimia 18.1 mwaka 2008 hadi asilimia 7.3 ya sasa. Hatahivyo, juhudi zinahitajika zaidi kutokomeza ugonjwa huu".Alisema Waziri Ummy Mwalimu
Aidha, alisema takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) linakadiria kuwa asilimia 17 ya magonjwa ya kuambukiza husambazwa na wadudu na kusababisha zaidi ya vifo millioni moja kila mwaka." Kwa mfano, malaria peke yake inakadiriwa kusababisha vifo 400,000 kila mwaka na wengi wanaofariki ni watoto chini ya miaka 5"Aliongeza Waziri Ummy Mwalimu
Kwa upande wa ugonjwa wa homa ya Dengue Waziri huyo alisema Mwaka huu ugonjwa wa Dengue umethibitishwa kuwepo hapa nchini hususani katika jiji la Dar es Salaam,Tanga na mikoa mingine. Kuanzia Januari 2019 hadi kufikia tarehe 21 Julai 2019 jumla ya wagonjwa waliothibitishwa kuwa na homa ya dengue hapa nchini ni 6588 na vifo 6 .
Alitaja mikoa hiyo ni Mkoa wa Dar es Salaam umeongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi ( 6,170 na vifo 4), Tanga (316 na kifo kimoja), Pwani ( 57), Morogoro (22), Lindi (8), Arusha (5), Dodoma (3 na kifo kimoja), Kagera (2), Singida (2),Ruvuma (2) na Kilimanjaro.
Hata hivyo Waziri Ummy alisema kutokana na kuendelea kujitokeza kwa magonjwa yaenezwayo na wadudu na,kusababisha madhara kwenye jamii,wizara yake imeandaa mkakati huo wa kudhibiti mbu na wadudu wengine wadhurifu wa mwaka 2019-2024 ikiwa na lengo la kuhakikisha wanadhibiti mbu na wadudu wengine wadhurifu kwa njia ya utengamano na kuhakikisha jamii inashiriki kikamilifu.
Katika kuimarisha udhibiti huo wizara imeagiza zenye uwezo mkubwa wa kupulizia zipatazo 8 na zinapelekwa katika mkoa wa Dar es Salaam,Tanga na Dodoma.
Kwa upande wake Waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo amemshukuru Waziri Ummy kwa kuzindua mkakati huo huku akionesha nia ya dhati ya kuendeleza mkakati huo katika Mikoa yote nchini huku akiwataka Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuhakikisha wanatenga bajeti ya kununua mashine ili kuweza kufikia malengo ya kutokomeza kabisa Malaria, Dengue na magonjwa mengine yanayosababishwa na wadudu dhurifu.
MWISHO
0 on: "MKAKATI WA KUZUIA MBU NA WADUDU DHURIFU NCHINI WAZINDULIWA LEO "