Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Ushirikiano Sekta ya Afya. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Ushirikiano Sekta ya Afya. Onyesha machapisho yote

Alhamisi, 12 Desemba 2019

SERIKALI YAAGIZA HOSPITALI ZOTE NCHINI KUANZISHA MFUKO WA FEDHA ZA DAWA.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akieleza jambo wakati wa kikao cha kuzindua Bodi ya ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sekou-Toure.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akiteta  jambo na Mwenyekiti mpya wa Bodi ya ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sekou-Toure  Prof. Abel Makubi wakati wa kikao cha kuzindua Bodi hiyo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akikata  utepe ikiwa kama ishara ya uzinduzi wa Bodi mpya ya ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sekou-Toure, Kulia kwake ni Mwenyekiti mpya wa Bodi Prof. Abel Makubi, kushoto kwake ni Kaimu RMO Mkoa Mwanza Dkt. Silas Wambura.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu na Mwenyekiti mpya wa Bodi ya ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sekou-Toure wakiwa wamebeba kitabu cha mwongozo wa Bodi ya ushauri,  wakati wa kikao cha kuzindua Bodi hiyo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akimkabidhi mwongozo mmoja kati  ya wajumbe wa Bodi mpya ya ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou-Toure, katikati ni Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Silas Wambura.

Baadhi ya Watumishi wa Hospitali  ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou-Toure waliofika kushuhudia uzinduzi wa Bodi mpya ya ushauri ya Hospitali hiyo, uliofanywa na Waziri wa Afya Mhe.@umwalimu katika ukumbi wa RMO Mkoa wa Mwanza.

Baadhi ya Watumishi wa Hospitali  ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou-Toure na Wajumbe wa Bodi ya zamani  ya ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou-Toure, waliofika kushuhudia uzinduzi wa Bodi mpya ya ushauri ya Hospitali hiyo, uliofanywa na Waziri wa Afya Mhe.@umwalimu katika ukumbi wa RMO Mkoa wa Mwanza.

Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya Mhe.@umwalimu, akiwa na wajumbe wa Bodi mpya ya ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou-Toure baada ya uzinduzi wa Bodi hiyo.


SERIKALI YAAGIZA HOSPITALI ZOTE NCHINI KUANZISHA MFUKO WA FEDHA ZA DAWA.

Na Rayson Mwaisemba, WAMJW- MWANZA

Serikali kupitia Wizara ya Afya imeagiza Waganga Wakuu wa Vituo vya Afya na Hospitali zote nchini kuanzisha mfuko wa fedha za Dawa kupitia makusanyo ya fedha za ndani, ili kuweza kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa dawa nchini endapo itatokea.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu katika kikao cha uzinduzi wa Bodi mpya ya ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza.

"Kuanzia Vituo vya Afya, Hospitali zote za Halmashauri, za Mikoa , kuanzisha mfuko wa fedha za dawa, na vyanzo vikuu vya mifuko hii ni mapato yatokanayo na mauzo ya dawa, huduma za Maabara, huduma za mionzi" alisema Waziri @umwalimu.

Amesema, Bodi hiyo ya ushauri lengo lake kubwa ni kuhakikisha inaboresha huduma za kinga na tiba katika Hospitali, huku ikihakikisha huduma hizo zinaifikia wananchi kwa ubora na gharama nafua.

Aliendelea kusema, Sera ya Afya nchini inawataka Wananchi kuchangia huduma kwa gharama nafuu isipokuwa kwa makundi yote ya msamaha, wakiwemo Wazee, Watoto walio chini ya miaka mitano na mama wajawazito, hivyo kuwataka kuweka mifumo mizuri ili kurahisisha utoaji huduma.

Mbali na hayo, Waziri Ummy ameiagiza Bodi hiyo kuhakikisha inaboresha huduma za dharura na ajali, ili kuokoa vifo vitokanavyo weza kuepukika kupitia huduma za dharura, keisha kuwashauri kujenga jengo jipya la wagonjwa wa nje (OPD) ili kuboresha huduma kwa wananchi.

"Watu wengi wanakufa wakiwa getini Mwa Hospitali, wakati utaalamu upo, kwamba mkiboresha huduma za dharura na ajari, tunaweza kuokoa maisha ya watu wengi " alisema Waziri @umwalimu.

Aidha, Waziri Ummy ameeleza majukumu ya Bodi hiyo ni kushauri, kutengeneza, kusimamia na kupitisha miongozo, malengo na mipango mikakati ya Hospitali kulingana na Sera na miongozo ya Serikali.

Nae Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sekou-Toure Dkt. Dkt. Graham Mtui ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kuendelea kuboresha huduma za Afya katika Hospitali hiyo kwa kuleta mashine ya uchunguzi wa figo na ini, mashine ya kusafisha figo ambazo zinatarajia kuanza kutoa huduma Januari 2020.

Kwa upande mwingine amesema, Hospitali inatarajia kupokea mashine sita ikiwemo CT Scan, X- ray yakidigitali, vifaa vya mifupa na mashine zinazosaidia kupumulia kutoka MSD.

Hata hivyo, amesema kuwa, idadi ya Wagonjwa wanaofika kupata huduma, kutoka wastani wa wagonjwa 350 kwa siku kwa mwaka 2015 hadi kufikia wagonjwa kati ya 500 mpaka 700 kwa Mwaka huu 2019, huku akiweka wazi kupunguza Rufaa za kwenda Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Bugando kwa asilimia 50.

"Kutokana na mafanikio hayo, idadi ya wagonjwa wanaopata huduma katika Hospitali imeongezeka, kutoka wastani wa wagonjwa 350 kwa siku ambayo ilikuwa mwaka 2015, na kufikia wastani wa wagonjwa kati ya 500 hadi 700 kwa mwaka huu 2019", alisema Dkt. Graham Mtui.

Mwisho.

Jumapili, 1 Desemba 2019

MAAMBUKIZI YA VVU YASHUKA NCHINI

Logo ya Siku ya UKIMWI.

Hadi sasa Watanzania milioni.1.4 wanaoishi na VVU ambapo kiwango cha maambukizi kikiwa ni asilimia 4.7 ikilinganishwa na asilimia 7.0 ya mwaka 2014.

Hayo yamesemwa leo na Mgeni rasmi wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya UKIMWI duniani  na Waziri wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemevu Mhe. Jenista Mhagama jijini Mwanza.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu.
Waziri Mhagama amesema kuwa maambukizi mapya na vifo  vitokanavyo na UKIMWI pia vimepungua.
 "Tumeweza kupata mafanikio haya kufuatia kuboreshwa kwa huduma.za ART na afua za kinga kama vile utahiri wa kitabibu wa wanaume na kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto"Alisema Waziri Mhagama.

Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Jenister.

Aidha, amesema kiwango  cha watu wanaoishi na VVU walioko kwenye mpango wa ARV kimeongezeka kutoka asilimia 22 mwaka 2009 hadi kufikia asilimia 57 ya mwaka 2017.

Naye Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema mpaka kufikia mwezi Septemba 2019 takribani watu 1,252,205 kati ya wananchi 1,600,000 wanaokadiriwa kuishi na VVU nchini walikuwa wamepima na kufahamu hali zao za maambukizi ya VVU. 
"Hii ni sawa na asilimia 78.3 ya lengo la 90 ya kwanza.
Miongoni mwao wanaume walikuwa 413,985 sawa na asilimia 33, na wanawake walikuwa 838,220 sawa na asilimia 77".

Mhe. Jenister akiwa na Mhe. Ummy Mwalimu.
Kwa upande wa vijana Waziri Ummy amesema kuwa Vijana balehe (umri wa miaka 10 – 19) walikuwa 57,167 sawa na asilimia 4.6, na vijana (umri wa miaka 15 – 24) walikuwa 96,006 sawa na asilimia 7.7.

Aidha, amesema kati ya waliopima na kutambua afya zao watu 1,221,799 sawa na asilimia 97.6 wanatumia ARV. 

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella.

 Hata hivyo alisema Lengo la 90 ya pili ambalo ni asilimia ya kuwa watu waliopimwa na kugundulika kuwa wana maambukizi ya VVU wanatumia dawa za kupunguza makali ya VVU (yaani ARV’s), tayari tumefikia takriban asilimia 98 wanatumia zawa za kupunguza makali ya VVU yaani ARV.

"Lengo la 90 ya tatu, ambalo ni kuhakikisha kuwa asilimia 90 ya wanaotumia ARV’s wamefanikiwa kupunguza wingi wa VVU mwilini Waziri huyo alisema wamefanya vizuri sana,"ni kuwa tumekuwa tukifuatilia kwa karibu hali za watu wanaotumia dawa za kupunguza makali ya VVU".Alisema 

Mhe. Jenister Mhagama akiwa na Mhe. Ummy Mwalimu, wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa TACAIDS Leonard Maboko.

Waziri Ummy alitaja mafanikio mengine ya kujikinga dhidi ya maambukizi ni tohara kwa wanaume ambapo kuanzia mwaka 2009 hadi Agosti 2019 jumla ya wanaume 4,456,511 wamefanyiwa tohara kupitia njia za mkoba na huduma katika vituo vya huduma.

Takwimu zinaonesha kwamba watu 953,973 sawa na asilimia 89 ya watu 1,072,650 waliopimwa wingi wa VVU wamefanikiwa kupunguza wingi wa VVU mwilini jambo ambalo ni muhimu katika kinga dhidi ya UKIMWI.Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni "Jamii ni chachu ya mabadiliko,tuungane kupunguza maambukizi mapya ya VVU"

Wananchi waliojitokeza katika viwanja vya Rock City Mall leo, kushuhudia Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani, mgeni rasmi akiwa Waziri Jenister Mhagama, aliyemwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Kassim Majaliwa.

Picha ya Pamoja ikiongozwa na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Jenister Mhagama, aliyemwakilisha Mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Mhe. Kassim Majaliwa.


#TunaboreshaAfya.
#WAMJW









Jumatano, 27 Novemba 2019

SERA MPYA YA AFYA KUJIKITA ZAIDI KWENYE KINGA.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. @umwalimu akifungua Kongamano la 6 la mwaka la Afya lenye lengo la kuwaleta pamoja Wadau mbali mbali katika Sekta ya Afya, ili kujadili maendeleo na changamoto ambazo nchi inakabiliana nazo.

Wadau mbali mbali wa Sekta ya Afya wakifuatilia kwa makini ufunguzi wa Kongamano la 6 la mwaka la Afya lenye lengo la kuwaleta pamoja Wadau mbali mbali katika Sekta ya Afya, ili kujadili maendeleo na changamoto ambazo nchi inakabiliana nazo, lenye kauli mbiu ya "ufanisi na matokeo " katika utoaji huduma za Afya.

Wadau mbali mbali wa Sekta ya Afya wakifuatilia kwa makini ufunguzi wa Kongamano la 6 la mwaka la Afya lenye lengo la kuwaleta pamoja Wadau mbali mbali katika Sekta ya Afya, kauli mbiu ya "ufanisi na matokeo " katika utoaji huduma za Afya.

Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa @umwalimu akiwa na Wadau wa masuala ya Afya kutoka Sekta mbali mbali za Kiserikali na Binafsi wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 6 la mwaka la Afya lenye kauli mbiu ya "ufanisi na matokeo " katika utoaji huduma za Afya.


SERA MPYA YA  AFYA KUJIKITA ZAIDI KWENYE KINGA.

Na Rayson Mwisemba, WAMJW- DOM

Sera Mpya ya Afya ya Mwaka  2019 - 2020 itajikita katika Kinga ili kukabiliana na mzigo wa gharama za matibabu ambazo zinawatesa Wananchi katika ngazi ya Jamii na nchi kwa ujumla.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu jiji hapa wakati akifungua kongamano la 6 la mwaka la Afya lenye lengo la kuwaleta pamoja Wadau mbali mbali katika Sekta ya Afya, ili kujadili maendeleo na changamoto ambazo nchi inakabiliana nazo, lenye kauli mbiu ya "ufanisi na matokeo " katika utoaji huduma za Afya.

"Ukiangalia Sera ya Afya ya Mwaka 2007, tulijikita zaidi kwenye mambo ya Tiba, sio kinga, kwahiyo Sera hii mpya ya Afya ya mwaka 2019 - 2020 itajiwekeza zaidi katika masuala ya Kinga sio Tiba, kwa sababu wote tunaamini Kinga ni bora kuliko tiba" alisema Waziri Ummy.

Hata hivyo alisema Sera hiyo inapendekeza kwamba, Serikali kwa kushirikiana na Wadau iweke miundombinu ya kutoa huduma za Afya kwa kuzingatia vigezo vya jografia ya eneo husika, idadi ya watu waliopo katika eneo, na kuangalia mzigo wa magonjwa katika eneo hilo.

"Serikali kwa kushirikiana na Wadau tutaweka miundombinu ya kutoa huduma za Afya kwa kuzingatia vigezo vitatu, vigezo vya kijografia ya eneo husika, vigezo vya idadi ya watu waliopo katika eneo, na vigezo cha tatu tutaangalia mzigo wa magonjwa katika eneo hilo ili kumpatia mwananchi huduma stahiki na kwa wakati kulingana na vigezo hivi" Alisema.

Aidha , amesema Sera hiyo mpya inayotarajia kuanza kutumika mwaka huu wa fedha , Serikali itaendelea kutambua mchango wa Sekta Binafsi katika utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi, jambo litalosaidia kupunguza mzigo wa utoaji huduma.

Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Kongamano la Afya Omary Nchili amesema kuwa, lengo la Mkutano huo, ni kujadili changamoto na matokeo chanya katika Sekta ya Afya, ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi.

"Tumekutana hapa Wadau mbali mbali kuweza kujadili, changamoto pamoja na matokeo chanya katika Sekta ya Afya, kwa ufanisi, hivyo tutakuwa hapa kwa siku mbili ambazo tutapembua kwa undani kuhusu upatikanaji wa huduma kwa gharama ndogo na upatikanaji wa huduma kwa ujumla " alisema.

Kongamano hilo la siku mbili limeandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Wizara ya Afya Zanzibar, Tume ya huduma ya Kijamii ya Kikristo, Bakwata na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Tindwa Medical Services inayofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete .

Mwisho.

Jumatatu, 9 Septemba 2019

TANZANIA NA CUBA KUENDELEZA USHIRIKIAKO KWENYE SEKTA YA AFYA

Picha ya Pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile pamoja na mgeni wake Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa Cuba Mhe. Marcelino Medina Gonzalez

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa Cuba Mhe. Marcelino Medina Gonzalez (hayupo pichani) katika kikao kujadili mahusiano baina ya nchi mbili kwenye Sekya ya Afya.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa Cuba Mhe. Marcelino Medina Gonzalez akifafanua jambo kwenye kikao kujadili mahusiano baina ya nchi mbili kwenye Sekya ya Afya.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akiagana na mbeni wake Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa Cuba Mhe. Marcelino Medina Gonzalez (kushoto) mara baada ya kumaliza kikao kujadili mahusiano baina ya nchi mbili kwenye Sekya ya Afya.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Dkt. Faustine Ndugulile leo amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba Mhe. Marcelino Medina Gonzalez Jijini Dodoma.

Katika mazungumzo yao, Dkt. Ndugulile ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Watu wa Cuba kwa kuendelea kusaidia Sekta ya Afya nchini kwa kutoa madaktari bigwa kufanya kazi kwenye hospitali hapa nchini Tanzania.

Dkt. Ndugulile ametaka mahusiano hayo chanya yaendelee kuimarika ili Watanzania wengi wanufaike kwa kuweza kupata huduma bora za matibabu ya kibingwa. 

“Nchi ya Cuba imepiga hatua kubwa kwenye Sekta ya Afya na wana madaktari bingwa wengi ambao tunaweza kuwatumia kuja hapa nchini kuhudumia Watanzania wengi zaidi ndani ya muda mfupi kuliko kupeleka wagonjwa nje” amesema Dkt.Ndugulile na kuendelea kusema kuwa pindi Madaktari hao wa kigeni wanapokuja hapa nchini, madaktari wa Kitanzania wanapata fursa ya kujifunza kwa vitendo na kutibu hapa hapa nchini kwa kutumia miundombinu iliyokuwepo hivyo kupunguza gharama kwa Serikali kusafirisha wagonjwa kwenda nje ya nchi.

Kwa upande wake Mhe. Marcelino Gonzalez ameipongeza Tanzania kwa juhudi kubwa inazozifanya kuwekeza kwenye Sekta ya Afya na kuhakikisha Madaktari wanapata utaalamu wa kutosha ili kutoa huduma bora kwa wananchi.

Amesema kuwa nchi ya Cuba iko tayari kutoa nafasi za masomo kusomea fani ya udaktari ili kuja kutibu Watanzania.

Nchi ya Cuba imekuwa na mahusiano ya karibu na Tanzania  kwa  kipindi kirefu. Mnamo Mwaka 1964 ubalozi wa Cuba ulifunguliwa rasmi nchini Tanzania na miaka 10 baadaye  mwaka 1974 Rais Fidel Castrol, alifika Tanzania kumtembelea Mwl.Julius Nyerere.Nchi ya Cuba na Tanzania Imekuwa na Mahusiano kwenye mambo mengi ikiwemo ushirikiano katika kutoa huduma za Afya.