Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Ijumaa, 22 Novemba 2019

“TUNAZO FEDHA ZA KUKAMILISHA HOSPITALI YA UHURU” - RAIS MAGUFULI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi (hawapo pichani) mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Hospitali ya Uhuru inayojengwa Wilayani Chamwino, Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu  akimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Hospitali ya Uhuru inayojengwa wilayani Chamwino, Dodoma.

Na Englibert Kayombo, WAMJW – Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewahakikishia wananchi kuwa Serikali inayo fedha za kutosha kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Uhuru.

Rais Magufuli amesema hayo leo alipokuwa akizungumza na wananchi mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali hiyo inayojengwa wilayani Chamwino, Dodoma.
“Fedha ya ujenzi wa hospitali ipo, tunayo Billioni 3.4” amesema Rais Magufuli ambaye ameonyesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa Hospitali hiyo.

Mafundi ujenzi wakiendelea na kazi ya ujenzi wa Hospitali ya Uhuru Wilayani Chamwino, Dodoma.

Rais Magufuli amesema kuwa mwanzoni TBA ilipewa kazi ya ujenzi wa hospitali hiyo lakini hawakusimamia vizuri ujenzi kupelea Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo kuchukua maamuzi ya kukabidhi kazi kwa Jeshi la Kujenga Taifa ili kazi hiyo ikamilike kwa wakati.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitizama ramani ya mchoro sanifu wa kengo la Hospitali ya Uhuru inayojengwa Wilayani Chamwino, Dodoma.

Naye Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Brigedia Jenarali Charles Mbuge aliyepewa jukumu la kusimamia ujenzi wa Hospitali hiyo amesema kuwa Jeshi lake linauwezo wa kufanya kazi hiyo na kuikamilisha ndani ya muda uliopangwa.

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Brigedia General Charles Mbuge akifafanua jambo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Bombe Magufuli mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali ya Uhuru wilayani Chamwino, Dodoma.

“Mheshimiwa Amiri Jeshi Mkuu, Jeshi letu lina nguvu ya kutosha na tutamaliza kwa muda kazi hii, sina mipango mingine ni kumaliza tuu” amesema Brigedia Jenerali Mbuge.

Mnamo tarehe 9 Desemba, 2018, Rais Magufuli alitoa maagizo ya fedha zilizotengwa kugharamia sherehe za uhuru kiasi cha Shilingi Milioni 995 kutumika kujenga hospitali katika Mkoa wa Dodoma. Kukamilika kwa hopitali hiyo kutatatua kero waliyokuwa wanaipata wananchi ya umbali wa kufuata huduma za afya.


Picha ya Mchoro sanifu wa jengo la Hospitali ya Uhuru inayojengwa Wilayani Chamwino, Dodoma.

Mwisho

0 on: "“TUNAZO FEDHA ZA KUKAMILISHA HOSPITALI YA UHURU” - RAIS MAGUFULI"