Na WAMJW-DSM
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeendelea
kutoa mafunzo kwa timu za Usimamizi wa uendeshaji wa huduma za afya katika
Halmashauri (CHMTs) juu ya tathmini ya uhakiki wa ubora wa huduma za
zinazotolewa katika eneo husika.
Mafunzo hayo yaliyofunguliwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar
Es Salaam Dkt. Yudas Ndugile siku ya Jumanne yameendelea kwa wiki moja lengo
likiwa ni kuwaelimisha watoa huduma za afya kuzingatia misingi ya utoaji wa
huduma bora za afya ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa miundombinu.
Akiongelea mafunzo hayo Mratibu na mkufunzI kutoka Wizara ya
Afya Dkt. Talhiya Yahya amesema Lengo la
kutoa nyota ni kuongeza chachu ya utoaji wa huduma za afya nchini ikiwa
sambamba na uboreshaji wa miundombinu na watumishi wa afya kufuata kanuni na
taratibu zilizowekwa mahala pa kazi.
“Lengo la mafunzo haya ni kutoa elimu kwa CHMT kuhusu
kutumia nyezo ya kielektroniki kufuatilia utekelezaji wa mipango ya uboreshaji
wa vituo kutegemea na mapungufu yaliyopatikana katika vituo kipindi cha kufanya
tathmini ya kutoa nyota kutokana na ubora wa kituo”. Amesema Dkt. Talhiya.
Dkt. amesema baada ya mafunzo hayo anategemea kuona maboresho yakifanyika
na tathmini ijayo ya kuhakiki ubora (Star Rating) vituo vingi vitakua na nyota
tatu au zaidi.
Wakati huo huo, Wizara imetoa mafunzo kwa watumishi wa afya wa
Hospitali mbalimbali za Jiji la Dar Es Salaam namna ya kufuata miongozo na
taratibu za kukinga na kudhibiti maambukizi (IPC Standards).
Mafunzo hayo ya siku tano yamehitimishwa leo katika ukumbi
wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam tawi la Kijitonyama ambapo mratibu wa mafunzo
hayo Dkt. Chrisogone German amesema lengo ni kuwajengea uwezo watumishi hao kufuata
miongozo ya utoaji wa huduma katika maeneo yao ya kazi.
Dkt. Chrisogone amesema muongozo wa mpya wa kukinga na
kudhibiti maambukizi (IPC Guideline) wa mwaka 2018 ambao umefuata vigezo vya
Shirika la afya Duniani (WHO) utaanza kutekelezwa katika vituo vya kutolea huduma
za afya katika mkoa wa Dar Es Salaam ikiwemo washiriki kujengewa uwezo wa
utayari wa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola.
Mafunzo hayo yamejumuisha washiriki kutoka Hospitali ya
Taifa Muhimbili, Mloganzila, Agha Khan, TMJ, Sali International, Hindu Mandal,
BOCHI na Rabininsia.
0 on: "ELIMU YA TATHMINI YA UHAKIKI UBORA WA HUDUMA ZA AFYA YAZIDI KUTOLEWA"