Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatano, 30 Oktoba 2019

SARATANI YA MATITI YAWEZA KUSHIKA NAMBA MOJA




Mkurugenzi wa huduma za Kinga ya Saratani  katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) Dkt. Crispian Kahesa

SARATANI YA MATITI YAWEZA KUSHIKA NAMBA MOJA

Na. Catherine Sungura, WAMJW-DSM

Endapo hatua zisipochukuliwa za  saratani ya matiti inaweza kushika namba moja kwa kuwa na idadi  kubwa ya wagonjwa  nchini.

Hayo yanesemwa na Mkurugenzi wa huduma za Kinga ya Saratani  katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) Dkt. Crispian Kahesa  alipozungumza na waandishi wa habari  kuhusu mwezi wa uhamasishaji , uelimishaji na uchunguzi wa saratani ambao huadhimishwa kila mwezi oktoba kila mwaka.

“Idadi ya saratani ya matiti  inaonekana kuongezeka nchini ambapo hivi sasa wanawake wenye umri  kuanzia miaka 20 na kuendelea nao wanagundulika  kuugua ugonjwa huu”. Alisema Dkt. Kahesa.

Alisema kuwa endapo hatua zisipochukuliwa  saratani hiyo itazidi kuwa tishio zaidi na kwamba  idadi kubwa ya wagonjwa wanaofika  hospitalini hapo wanatoka katika maeneo ya mjini ambapo mkoa wa Dar es salaam unaonekana kuongoza.

“Tathimini  ya miaka 10 iliyopita saratani hii ilikua inashika nafasi ya tano ,hivi sasa ni ya pili kwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa,zamani tulikua tunawaona wagonjwa kuanzia miaka 55 ukashuka hadi miaka 50 na sasa tunaona hadi wenye umri wa miaka 20”.

Dkt. Kahesa alisema kuwa kwa mwaka huu pekee wameweza kuona wanawake 1443 ambapo kati ya 342 wamekutwa na uvimbe 170 walikuwa na dalili za awali za saratani.

Kwa upande wa saratani kwa wanaume Dkt. Kahesa alisema kuwa saratani hiyo huathiri asilimia moja kwa wanaume hata hivyo kwa upande wao ni hatari  zaidi na endapo isipogundulika huweza kuathiri mapafu yao kwa haraka.

“Saratani hii huathiri wanawake zaidi  kuliko wanaume kwa asilimia 99 na wanaume ni asilimia 1 tu,ambapo dalili kwa wanaume  ni tofauti  kidogo na wanawake,hivyo kwa mwanaume ni rahisi kugundua kuliko mwanamke kwa kuwa kifua chake kina mafuta mengi.

Aliongeza kuwa kati ya wanawake 170 waliofanyiwa vipimo  zaidi ya 68 waligundulika na vivimbe ambavyo ni ugonjwa wa saratani.

Hapa nchini saratani ya shingo ya kizazi inaongoza ikifuatiwa  na saratani ya matiti,saratani  ya njia ya chakula,saratani ya tezi dume na saratani  nyingine ni zile zinazoathiri  mfumo wa kinga.

Mwisho

0 on: "SARATANI YA MATITI YAWEZA KUSHIKA NAMBA MOJA"