Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumanne, 29 Oktoba 2019

MAAMBUKIZI YA VVU NCHINI YASHUKA KWA ASILIMIA 2.3

 Na WAMJW- DSM

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa maambukizi ya VVU yamepungua kutoka asilimia 7 mwaka 2003/4 hadi asilimia 4.7 mwaka 2016/17 .

Waziri Ummy ameyasema hayo leo wakati wa mkutano wa kujadili maendeleo ya utekelezaji wa sera ya pamoja ya ushirikiano na Serikali ya Marekani kupitia PEPFAR cop 19 kuhusiana na VVU na UKIMWI uliofanyika jijini Dar Es Salaam.

“Kuanzia huduma za UKIMWI zianze kutolewa nchini tumeshuhudia mafanikio makubwa kwa upande wa kupunguza maambukizi kutoka asilimia 7 mwaka 2003/4 hadi asilimia 4.7 mwaka 2016/17" alisema Waziri Ummy.

Aliendelea kusema  kuwa Serikali imefanikiwa kutoa huduma za utambuzi na matibabu na sasa dhana ya kwamba UKIMWI ni ugonjwa wa kifo imeisha na kuwa ni ugonjwa unaoweza kudhibitiwa

Aidha,Waziri Ummy amesema kuwa Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo PEPFAR inaendelea kupanga mikakati mbalimbali ya kudhibiti maambukizi ya UKIMWI, kutoa huduma na matibabu kwa watu wanaoishi na virusi.

Mbali  na hayo Waziri Ummy amedai kuwa Serikali imefanikiwa kutoa huduma za utambuzi na matibabu, huku akisisitiza kuwa dhana ya kwamba UKIMWI ni ugonjwa wa kifo imeisha baina ya wananchi

Hata hivyo, Waziri  Ummy amesema, kufikia mwezi Septemba mwaka 2019 idadi ya watu waliopima na kujua afya zao imefikia asilimia 77.2 na kati yao asilimia 98 wanaendelea na huduma za VVU pamoja na matumizi ya ARV.

Hata hivyo Waziri Ummy hakusita kulishukuru shirika la PEPFAR kwa kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI kwa kudhamini, kuweka malengo na kutoa miongozo katika huduma za VVU nchini.

Kwa upande wake Balozi wa Marekani nchini Dr. Inmi Patterson amesema Serikali ya Marekani itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ugonjwa wa UKIMWI na ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa jitihada kubwa inazofanya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kudhibiti maambukizi na kutoa huduma bora za VVU kwa watu waliogundulika na maambukizi.

Mkutano huo ulijumuisha wadau mbalimbali akiwemo mwakilishi wa Shirika la Afya duniani nchini Tanzania Dkt. Tigest Ketsela pamoja na wataalam kutoka Wizara ya Afya wakiongozwa na Mkurugenzi wa kinga Dkt. Leonard Subi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Tume ya kudhibiti na kupambana na UKIMWI (TACAIDS) pamoja na Shirika la PEPFAR Tanzania.

Mwisho.

0 on: "MAAMBUKIZI YA VVU NCHINI YASHUKA KWA ASILIMIA 2.3"