Jumamosi, 19 Oktoba 2019
KATIBU MKUU DKT. CHAULA AHITIMISHA ZIARA YAKE MKOANI MWANZA
Picha mbalimbali zikimuonesha Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula alipotembelea Hospitali ya Rufaa ya Sekou Toure kukagua ujenzi wa jengo la ghorofa litakalotoa huduma mbalimbali kisha kutembelea baadhi ya maeneo ya utoaji wa huduma za afya, kuongea na wagonjwa waliofika Hospitalini hapo ili kupata huduma lengo likiwa ni kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi kisha amehitisha kwa kuongea na watumishi na kutatua baadhi ya kero alizoziona.
Baada ya hapo Dkt. Chaula ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Bugando na kuzungumza na Menejimenti ya Hospitali hiyo na kuridhishwa na mafanikio yaliyopatikana ndani ya kipindi cha miaka miwili na kuwezesha hospitali kutoa huduma bora na kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bugando Prof. Abel Makubi amepongezwa kutokana na ubunifu wake uliowezesha hospitali kuboresha miundombinu na mapato ya ndani.
Dkt. Chaula pamoja na timu aliyoambatana nayo akiwemo Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Grace Maghembe imeishauri Hospitali ya Bugando kuendelea kuzijengea hospitali za Mikoa na Wilaya katika kuzalisha maji tiba kwa wagonjwa. Asilimia 50 ya infusion zinazotumika Bugando zinazalishwa na hospitali.
Prof. Kabudi ameishukuru serikali kupitia wizara ya afya kwa kusaidia kuanzishwa huduma za wagonjwa wa saratani kupitia ujenzi wa jengo la huduma hizo. Pia aliendelea kushukuru kwa hospitali hiyo kuingizwa kwenye mpango wa kupata mashine ya MRI.
Dkt. Chaula na timu nzima anayoongozana nayo imeondoka jijini Mwanza kuelekea Chato na Geita kuendelea na ziara yake katika mikoa ya kanda ya ziwa.
About Wizara ya Afya
Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 on: "KATIBU MKUU DKT. CHAULA AHITIMISHA ZIARA YAKE MKOANI MWANZA"