Jengo la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Zainab Chaula (kulia) akizungumza na watendaji wake alipotembelea ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara.
Na.WAMJW
Hospitali ya rufaa ya mkoa wa mara inatarajiwa kukamilika ujenzi wake na kuanza kutoa huduma za afya mwezi agosti 2020
Hayo yamesemwa na na Katibu Mkuu
Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula wakati akihitimisha ziara yake mkoani Mara kwa kutembelea ujenzi wa Hospitali hiyo (Kwanga) na kuona maendeleo ya ujenzi ambao ulikua ukisuasua kutokana na sababu mbalimbali.
Dkt. Chaula alisema kuwa wametoa zaidi ya bilioni 4 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi huo hivyo na kumtaka mkandarasi mkuu Shirika la nyumba nchini (NHC) kuhakikisha mradi huo unakamilika mwezi Agosti mwaka 2020.
"Tunahitaji huduma zianze kutolewa mapema kwani Hospitali hiyo itakua ni mkombozi kwa wananchi wa Musoma na maeneo jirani wanaopata rufaa za kwenda Bugando".Alisema Dkt. Chaula
Katika ziara hiyo.Dkt. Chaula alitembelea Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Musoma na kuona hali halisi ya utoaji wa huduma za afya Hospitalini hapo kisha kuongea na watumishi.
Aidha, Dkt. Chaula amehitimisha ziara yake mkoani Mara kwa kutembelea Hospitali ya Wilaya ya Butiama na kuridhishwa na majengo mapya ya huduma za mama na mtoto na kisha kutembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa na kuweka shada kwenye kaburi lake.
0 on: "HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA MARA KUKAMILIKA 2020"