Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Alhamisi, 14 Novemba 2019

WAZIRI MKUU AWAASA WANANCHI KUJENGA UTAMADUNI WA KUFANYA MAZOEZI.


WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewaasa Wananchi kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi kwa dakika 30 angalau mara tatu kwa wiki.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo, wakati akizindua Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza katika viwanja vya Jamhuri, Jijini Dodoma.

"Tujenge utamaduni wa kufanya mazoezi angalau dakika 30 mara tatu kwa kila wiki, niweke msisitizo kwa sekretarieti ya Mkoa na mamlaka ya Serikali za mitaa, kuendeleza utaratibu wa mazoezi uliowekwa na mama yetu Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ", amesema Waziri Mkuu. 


Mbali na hayo, Waziri Mkuu, amesisitiza juu ya kupunguza matumizi ya vilevi, kama vile Pombe na sigara pamoja na kinywaji vyenye sukari, ambavyo kwa kiasi kikubwa uchangia magonjwa kama vile kisukari na Kansa jambo linalopelekea mzigo wa matibabu kwa wananchi.

"Tujitahidi sana kupunguza matumizi ya vilevi, hususan Pombe na Sigara, pamoja na vinywaji vilivyo na sukari  kama vile soda, juisi na chokoreti, tunajua wengi tunakunywa, basi wewe kama ni mshiriki mzuri basi pata kwa kiasi". Amesema Mhe. Kassim Majaliwa.



Ameendelea, kusisitiza kwa kuwaagiza viongozi wa maeneo mbali mbali kuhamasisha wananchi wa maeneo yao kufanya mazoezi angalau kila Jumamosi, na kuwataka kupunguza matumizi ya magari kila mara.

Aidha, Mhe. Majaliwa ameagiza viongozi kuendelea kuhamasisha wananchi kujiunga katika vikundi vya kufanya mazoezi, na kusisitiza kuvifufua vikundi vyote vya mazoezi vilivyo kufa, huku akieleza umuhimu wa kutoa taarifa kwa wananchi ili washiriki katika mazoezi.  



Amesema Halmashauri zote zihakikishe zinatenga na kuyaendeleza maeneo ya wazi katika kila kata au mitaa ili pamoja na shughuli nyingine wananchi pia watumie maeneo hayo kwa ajili ya kufanya mazoezi.

Waziri Mkuu amesema  wanafunzi kuanzia sasa kabla ya kuingia darasani wawe wanakimbia mchakamchaka ili waweze kujiimarisha kiafya jambo ambalo litawaepusha na magonjwa yasiyoambukiza. 


Kwa upande wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa, katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita Tanzania ilishuhudia ongezeko la idadi ya watu waliopatiwa huduma za magonjwa yasiyoambukiza kutoka wagonjwa milioni 3.4 kwaka 2016 hadi wagonjwa milioni 4.2 mwaka 2018, ilkiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 24.

Hata hivyo, Waziri Ummy ameyataja magonjwa hayo ni kama vile, pumu, shinikizo la juu la damu, kisukari, saratani, siko seli, magonjwa ya akili, ajali, magonjwa mengi ya macho, kinywa, masikio, pua na koo, huku akidai kuwa magonjwa haya yamekuwa yakiongezeka duniani kote na kuathiri nyanja zote za kimaisha.

Picha ya Pamoja ikiongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akiwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu, pamoja na viongozi wengine wa Kitaifa katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.

#TunaboreshaAfya.

0 on: "WAZIRI MKUU AWAASA WANANCHI KUJENGA UTAMADUNI WA KUFANYA MAZOEZI."