Serikili kupitia Wizara ya Afya imefanikiwa kupunguza maambukizi ya malaria kwa takribani asilimia 50% kutoka 14.8% mwaka 2015 mpaka kufikia 7.3% mwaka 2017.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wakiongozana na Mawaziri kutoka nchi za SADC ziarani Mkoa wa Pwani, Kibaha walipotembelea Kiwanda cha Viuadudu wa kibaiolojia cha TBPL.
Waziri Ummy Mwalimu amesema, mafanikio haya ni kutokana na kuwekeza rasilimali fedha, utashi wa viongozi, wadau mbalimbali na jamii kwa ujumla katika kutekeleza mikakati ya udhibiti wa malaria.
Mojawapo ya afua zilizochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kudhibiti ugonjwa wa malaria ni kujenga kiwanda cha viuadudu vya kibailojia kwa ajili ya kuua mazalia, alibainisha Waziri Ummy.
Aliendelea kusisitiza kuwa matumizi ya viuadudu hivyo vya kibailojia ni kwa ajili ya kuangamiza viluilui vya mbu wanavyoeneza magonjwa mbalimbali yakiwemo; malaria, homa ya dengue, zika, homa ya manjano, matende, giri-majihoma ya bonde la ufa na chikungunya.
Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa ili kuendeleza mafanikio na hatimae kutokomeza kabisa malaria katika nchi zote za SADC tunahitaji kuongeza wigo na kuhakikisha nchi wanachama wanaongeza rasilimali fedha ili kutekeleza afua mbalimbali za udhibti wa malaria, alisema.
Aidha, Waziri Ummy akiongozana na Mawaziri wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi Kusini mwa Afrika (SADC) alifanya ziara katika Bohari ya Dawa MSD, huku kwa kiasi kikubwa kuonekana kuridhishwa na hali ya utendaji kazi wa Bohari ya Dawa nchini (MSD), kutokana na mfumo mzuri wa manunuzi na usambazaji wa dawa, vifaa, vifaatiba na vitendanishi.
Waziri Ummy ambae pia ni, Mwenyekiti wa baraza hilo la Mawaziri amesema wameridhishwa na utendaji kazi wa bohari hiyo na kwamba sasa wanasubiri hatua za mwisho zikamilike manunuzi yaanze.
“Wameshuhudia MSD wana uwezo, utaalamu, vifaa kwa hiyo mawaziri wameridhika na hali waliyoikuta hapa na tunaamini kwa kununua dawa kwa pamoja kama nchi za Sadc bei pia itashuka,” amesema Ummy Mwalimu.
Mbali na hayo, Waziri Ummy amesema kuwa, MSD ina uwezo na utaalamu unaokidhi viwango katika manunuzi na usambazaji wa dawa, hali iliyopelekea kushinda zabuni ya usambazaji wa dawa kwa nchi wanachama wa SADC.
#SADC
#TunaboreshaAfya
Ijumaa, 8 Novemba 2019
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 on: "TANZANIA YAPUNGUZA MAAMBUKIZI YA MALARIA KWA ASILIMIA 50"