Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumapili, 19 Aprili 2020

TUACHE MZAHA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA CORONA

- Hakuna maoni
Wafanya biashara ndogo ndogo katika kituo cha mabasi Makumbusho wakipata mafunzo juu ya namna yakunawa mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka wakati,   elimu ya kujikinga dhidi ya Corona ilipokuwa ikitolewa kituoni hapo.

Mkuu wa Kitengo cha maji na usafi wa mazingira kutoka Wizara ya Afya, Ndg. Anyitike Mwakitalima akiwaelekeza madereva bajaji namna ya kunawa  kwa kufuata taratibu za unawaji mikono kwa sabuni na maji safi yanayotiririka kwa usahihi kulingana na miongozo ya Wizara.

Mkuu wa Kitengo cha maji na usafi wa mazingira kutoka Wizara ya Afya, Ndg. Anyitike Mwakitalima akielekeza  jambo wakati wa kampeni ya uhamasishaji kwa Jamii juu ya namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona.

Balozi wa kampeni ya Mikoni safi, Tanzania salama, Msanii Mrisho Mpoto (Mjomba), akisisitiza jambo kwa wafanyabiashara katika eneo la Coco Beach Dar es salaam juu ya umuhimu wa kuchukua tahadhari wakati wote ili kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Balozi wa kampeni ya Mikoni safi, Tanzania salama, Msanii Mrisho Mpoto (Mjomba) akisisitiza kukaa umbali wa mita moja au zaidi ili kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona pindi watu wanapoongea au mtu anapopiga chafya au kukohoa.


TUACHE MZAHA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA CORONA

Na WAMJW- DSM

Mkuu wa Kitengo cha maji na usafi wa mazingira, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ndg. Anyitike Mwakitalima ametoa wito kwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kuacha mzaha na kufuata taratibu kutoka kwa Wataalamu wa Afya ili kujikinga dhidi ya virusi vya Corona.

Ameyasema hayo leo, wakati akitoa elimu kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kuhusu kuchukua tahadhari za kujikinga dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona

"Watanzania tusifanye mzaha, huu ugonjwa sio wakufanyiwa mzaha, wenzetu wa nchi zilizoendelea pamoja na uchumi wao kuwa mkubwa na sayansi yao kubwa, lakini wamefika mahali wameshindwa, hizi tahadhari za msingi ambazo tunaelekeza ni muhimu kuzizingatia " alisema.

Alisema kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Afya, inaendelea kutoa elimu ya Corona kwa jamii kupitia vyombo vya habari, lakini pia kuwafuata wananchi walipo ili kuwapa elimu hiyo na kujibu maswali yanayowatatiza, hali itayosaidia watu kufahamu njia zote za kujikinga na kuepuka kupata maambukizi ya virusi hivyo.

"Tunafahamu kwamba , bado suala la elimu halijaweza kufika kwa Jamii vyakutosha, kwahiyo tunatumia njia mbali mbali, tunatumia vyombo vya habari kama tv na redio, lakini tumeona tunakila sababu yakushuka na kwenda ambako Jamii hipo ili tuweze kuzungumza nao, na kujibu maswali ya msingi yanayowatatiza" alisema.

Aidha, alisema kuwa, kwa sehemu kubwa Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wanachukua tahadhari, kwa kuweka vifaa vya kunawia mikono na sabuni, na kusafisha mikono ya abiria kabla yakupenda usafiri.

"Kwa sehemu kubwa tumeona wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wanachukua tahadhari, ikiwemo kutengeneza jiki kwaajili yakutakasa chombo chake cha usafiri, lakini katika sehemu za biashara watu wameweka vyombo vya kunawia mikono na wanaelekezwa kunawa kabla ya kufanya manunuzi" alisema

Nae Balozi wa kampeni ya Mikoni safi, Tanzania salama, Msanii Mrisho Mpoto (Mjomba) amewaasa wananchi kunawa mikono mara kwa mara kwa kufuata hatua tano muhimu, kama ifuatavyo moja ni kulowanisha mikono, pili kupakaa sabuni kwenye mikono ili kuua virusi vyote, tatu ni sugua mikono yako kwenye kucha, viganja, vidole na sehemu zote, nne ni kusuuza mikono kwa maji yanayotiririka, na hatua ya tano ni kufuta mikono kwa kitambaa safi.

Aliendelea kusisitiza kuwa, kulingana na miongozo kutoka kwa Wataalamu wa Afya, hairuhusiwi kufuta mikono kwenye nguo baada ya kunawa mikono kwenye hatua tano, kwani kufanya hivyo hupelekea kurudisha maambukizi mikononi endapo vitakuwepo katika nguo hizo.

Uhamasishaji huu unafanywa kupitia kampeni hii ya “Mikono safi, Tanzania salama” inaratibiwa na Wizara ya Afya, kwa kushirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la Project CLEAR kwa kushirikiana na Msanii Mrisho Mpoto (Mjomba) kutoka Mjomba Theatre Gallery unaendelea katika Jiji la Dar es Salaam.

Mwisho

Jumatano, 15 Aprili 2020

TUEPUKE MSONGAMANO KATIKA MAENEO YETU YA KAZI

- Hakuna maoni
 Mkuu wa Mkoa wa Songwe Breg. Jen. Nicodemus Mwengela akisisitiza jambo wakati akiongea na wahamasishaji kutoka Wizara ya Afya, Shirika lisilo Lakiserikali la Project CLEAR na Mjomba Theatre Gallery katika ofisi zake Vywawa Mkoa wa Songwe. 

Mkuu wa Kitengo cha maji na usafi, Wizara ya Afya Ndg. Anyitike Mwakitalima akieleza jambo kuhusu ugonjwa wa Corona mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe Breg. Jen. Nicodemus Mwengela wakati walipoenda kukabidhi vifaa vya kunawa mikono na vitakasa mikono kwaajili ya Mkoa huo.

Msanii Mrisho Mpoto (Mjomba) kutoka Mjomba Theatre Gallery akifafanua jambo mbele ya mkuu wa Mkoa wa Songwe Breg. Jen. Nicodemus Mwengela (hayupo kwenye picha).

Waratibu wa kampeni ya "Mikono safi, Tanzania salama" kutoka Wizara ya Afya Shirika lisilo Lakiserikali Project CLEAR na Mpoto Gallery wakifuatilia neno kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Breg. Jen. Nicodemus Mwengela juu ya namna Mkoa unavopambana na ugonjwa wa Corona. 

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Breg. Jen. Nicodemus Mwengela akinawa mikono kwa sabuni na maji safi yanayotiririka, ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo kutoka Wizara ya Afya na washirika wake, pembeni yake ni Katibu tawala wa Mkoa huo.

Mwenyekiti wa Machifu Mkoa wa Songwe akinawa mikono yake kwa sabuni na maji safi yanayotiririka ikiwa ni moja ya njia ya kupambana dhidi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona.

Mwananchi wa Ichenjezya Vywawa Songwe akinawa mikono yake kwa sabuni na maji safi yanayotiririka ikiwa ni moja ya njia ya kupambana dhidi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona.

Msanii Mrisho Mpoto (Mjomba) kutoka Mjomba Theatre Gallery akikabidhi vitakasa mikono na vifaa vingine vya kupambana dhidi ya ugonjwa wa Corona kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Breg. Jen. Nicodemus Mwengela, kulia ni Mkuu wa Kitengo cha maji na usafi, Wizara ya Afya Ndg. Anyitike Mwakitalima.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Breg. Jen. Nicodemus Mwengela katika picha ya pamoja na Waratibu wa kampeni ya "Mikono safi, Tanzania salama" kutoka Wizara ya Afya Shirika lisilo Lakiserikali Project CLEAR na Mpoto Gallery baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo kwaajili ya kupambana dhidi ya ugonjwa wa Corona Mkoani Songwe.

Afisa kutoka makao makuu jeshi la polisi kitengo cha ushirikishaji Stafu Sajenti Valentino Ngowi akihamasisha wananchi katika kituo cha mabasi Vwawa juu ya umuhimu wa kukaa zaidi ya mita moja kati ya mtu mmoja hadi mwingine ikiwa ni moja ya njia ya kupambana dhidi ya ugonjwa wa Corona katika Mkoa wa Songwe.

Afisa kutoka makao makuu jeshi la polisi kitengo cha ushirikishaji Stafu Sajenti Valentino Ngowi akikagua moja ya daladala ili kujionea kama wanafuata maelekezo ya Serikali ya kuepuka msongamano ndani ya daladala (level sit) katika kituo cha mabasi Vwawa Mkoa wa Songwe.
 
Wafanyabiashara katika Soko la Ichenjezya Vwawa Songwe wakifuatilia Elimu juu ya njia za kupambana dhidi ya ugonjwa wa Corona kutoka timu ya uhamasishaji Wizara ya Afya ikiwemo kunawa mikono kwa maji safi yanayotiririka na sabuni, au kutumia vitakasa mikono (sanitizer) na kuepuka msongamano isiyo na ulazima. 



TUEPUKE MSONGAMANO KATIKA MAENEO YETU YA KAZI.

Na Rayson Mwaisemba, WAMJW-SONGWE

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Breg. Jen. Nicodemus Mwangela ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Songwe kuepuka misongamano katika maeneo yote, ikiwa ni moja ya njia ya kupambana na ugonjwa wa Corona usisambae endapo utaingia Mkoani hapo.

Ameyasema hayo, wakati akipokea vifaa vya kunawia mikono pamoja na vitakasa mikono kutoka Wizara ya Afya na Shirika la Project CLEAR, ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya uhamasishaji kwa wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona.

“Serikali imetoa maagizo mbali mbali, ambayo sisi kama Serikali ya Mkoa tunayasimamia na kuhakikisha yanatekelezwa, ikiwemo kusisitiza kuepuka msongamano na mikutano isiyokuwa yalazima katika maeneo mbali mbali na hili linatekelezwa vizuri kabisa” alisema.

Mbali na hayo, amesema kuwa, maambukizi ya ugonjwa wa Corona yameleta madhara makubwa kwa maisha ya binadamu hasa katika upande wa kiuchumi, huku akisisitiza kuwa nchi nyingi duniani zimeathirika kutokana na janga hili la Corona.

“Ni kweli kabisa huu ugonjwa sasahivi, umeleta madhara makubwa kwa Maisha ya binadamu, lakini pia kiuchumi, nan chi nyingi zenye uwezo mkubwa kiuchumi na kiafya zimeahirika kutokana na janga hili”alisema.

Aidha, Mhe. Alisema kuwa, Serikali inaendelea kutoa elimu na tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona kwa wananchi, hii inafuatia sababu kuwa, Mkoa wa Songwe upo mpakani mwa nchi za Malawi na nchi ya Zambia ambayo inapokea pia watu kutoka nchi ya DR Congo.

“Songwe ipo kwenye mlango, tusipotoa tahadhari ya kutosha kwa wananchi kuna hatari kubwa ya ugonjwa kuingia, Mkoa wa Songwe upo mpakani, tuna KM 135 tunapakana na Zambia, KM 45 tunapakana na Malawi, nchi zote hizo tayari zina maambukizi ya ugonjwa wa Homa kali ya mapafu, huku nchi ya DR Congo ikiongoza kuwa na wagonjwa wengi zaidi” alisema

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha maji na usafi wa mazingira kutoka Wizara ya Afya, Ndg. Anyitike Mwakitalima amesema kuwa katika kupambana na ugonjwa huo Serikali kupitia Wizara ya Afya inakabidhi vifaa vya kunawa mikono (sanitizer) lita 150 , Dispensa 30 na vifaa maalum vya kunawia mikono Mkoa  wa Songwe na mikoa yote ya mipakani kama sehemu ya kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu.

Nae, Msanii Mrisho Mpoto (Mjomba) amesema kuwa, vita dhidi ya ugonjwa huu ni vita inayohitaji ushirikiano na umoja baina ya watu wote katika jamii, huku akiweka wazi kuwa baadhi ya silaha za kupambana dhidi ya ugonjwa huu ni kunawa mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka na kuepuka msongamano isiyo na ulazima.

“Tupo katika kipindi ambacho tunahitajiana sana, kila mtu kwa nafasi yake anamuhitaji mwingine, kwahiyo tushirikiane kwa pamoja tunaweza kukabiliana na ugonjwa huu, janga hili haliitaji vifaru, janga hili haliitaji jeshi la anga, janga hili linatuhitaji sisi na utayari wet utu, na nguvu pekee tulionayo ni kunawa mikono, na kuepuka misongamano isiyo yalazima, na utamaduni huu uwe endelevu”, alisema

Uhamasishaji huu unafanywa kupitia kampeni hii ya “Mikono safi, Tanzania salama” inaratibiwa na Wizara ya Afya, kwa kushirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la Project CLEAR kwa kushirikiana na Msanii Mrisho Mpoto (Mjomba) kutoka Mjomba Theatre Gallery unaendelea katika Mkoa wa Songwe, kisha kuelekea Mkoa wa Rukwa.

MWISHO.

Jumanne, 14 Aprili 2020

MADEREVA CHUKUENI TAHADHARI DHIDI YA CORONA

- Hakuna maoni
Mratibu wa kampeni ya "Mikono safi, Tanzania salama" kutoka Wizara ya Afya Ndg. Anyitike Mwakitalima akitoa maelekezo kutoka kwa moja kati ya dereva boda boda katika eneo la kituo cha daladala cha Kabwe Jijini Mbeya ikiwa ni mwendelezo wa kampeni maalum ya uhamasishaji jamii kuchukua hatua za tahadhari dhidi ya maambukizi ugonjwa wa Corona Jijini Mbeya. 

Kondakta wa basi linalofanya safari ya Kyela akimsaidia abilia wake kutaka mikono kwa sanitizer kabla ya kuingia kwenye gari katika kituo cha mabasi Nanenane Jijini Mbeya, ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Corona yasisambae kwa abilia wengine endapo yatatokea.

Mkazi wa Mbalizi Jijini Mbeya akisafisha mikono kwa maji safi yanayotiririka na sabuni kabla yakuingia dukani kufanya manunuzi ikiwa ni sehemu ya kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona.

Mratibu wa kampeni ya "Mikono safi, Tanzania salama" kutoka Wizara ya Afya Ndg. Anyitike Mwakitalima akinawa mikono kwa sabuni na maji safi yanayotiririka katika chuo cha MUST Jijini Mbeya, ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona nchini.
Waratibu wa kampeni ya "Mikono safi, Tanzania salama" kutoka Wizara ya Afya Shirika lisilo Lakiserikali Project CLEAR na Mpoto Gallery wakitoa Elimu kwa madereva bodaboda wa Mbalizi Mbeya wakati wa kampeni maalum ya uhamasishaji jamii kuchukua hatua za tahadhari dhidi ya maambukizi ugonjwa wa Corona.

Kushoto ni Meneja wa Peter Hoteli Jijini iliyopo Jijini Mbeya, akikabidhiwa zawadi ya sabuni na vitakasa mikono (sanitizer) kutoka kwa mfanya kazi wa Shirika lisilo Lakiserikali Project CLEAR Bi Viola baada ya Waratibu wa Kampeni hiyo kutoka Wizara ya Afya kuridhishwa na hatua zinazochukuliwa na Hoteli hiyo kupambana dhidi ya ugonjwa wa Corona. 

Mkazi wa Mbalizi Jijini Mbeya aliyejishindia zawadi wa kitenge baada ya timu ya kampeni maalum ya uhamasishaji jamii kuchukua hatua za tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona kutoka Wizara ya Afya kumkuta akichukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo kwa kunawa mikono kwa maji safi yanayotiririka.

Timu ya kampeni maalum ya uhamasishaji jamii kuchukua hatua za tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona kutoka Wizara ya Afya ikiendelea na kazi ya uhamasishaji katika eneo la kituo kikuu cha mabasi ya Mkoani Jijini Mbeya ili wananchi waendelee kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona.


MADEREVA CHUKUENI TAHADHARI DHIDI YA CORONA

Na Rayson Mwaisemba, WAMJW- MBEYA

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeendelea kuwaasa madereva wa vyombo vya usafiri kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Kitengo cha Maji na Usafi wa Mazingira kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ndg. Anyitike Mwakitalima wakati wa uhamasishaji kwa wananchi wa kuchukua hatua za tahadhari dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona katika Mikoa ya Mbeya na Songwe.

Amesema kuwa, kila dereva na kondakta wake ni lazima wahakikishe gari linakuwa na vitakasa mikono (Sanitizer) kwa ajili ya matumizi yao na abiria. Aidha, vituo vyote vya mabasi viwe na sehemu za kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni kwa hii ni hatua muhimu sana ya kujikinga na virusi vya Corona. Aliyasema hayo alipotembelea Stendi Kuu ya mabasi katika Jiji la Mbeya iliyopo eneo la Nane Nane.

"Kondakta hakikisha kila anaepanda gari lako amenawa mikono kwa sabuni na maji safi yanayotiririka au ametakasa mikono yake kwa Sanitizer ndio aruhusiwe kuingia kwenye gari, huu ugonjwa jamani ni hatari na umeua watu wengi" alisema.

Aidha, amewaagiza madereva na makondakta wao kuhakikisha kila siku jioni wanapokuwa wamemaliza kazi zao wahakikishe wanasafisha magari yao kwa dawa maalum aina ya Jiki, ili kuua virusi vinavyoweza kuwepo na kupelekea maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

"Madereva na makondakta wote kila siku jioni, hakikisha mnasafisha magari yenu kwa dawa maalum, wote mnaifahamu Jiki hapa, dawa hii inatumika Kutakasa magari, bajaji au pikipiki. Changanya kipimo kimoja cha Jiki na vipimo Sita (6) vya maji ili kupata mchanganyiko unaotakiwa kisha osha chombo chako cha kusafirisha abiria, utajikinga wewe na abiria wako " alisema.

Nae, Afisa kutoka Makao Makuu Jeshi la Polisi Kamisheni ya Ushirikishaji Jamii Stafu Sajenti Valentino Ngowi, amewataka madereva bodaboda kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi endapo watakutana na mtu alieingia nchini kwa njia za panya, ikiwa ni moja ya jitihada za kupambana na ugonjwa wa Corona, huku akiwataka wasiingie katika vishawishi vya kutaka pesa ya haraka ambayo inaweza kuwagharimu wao na taifa kwa jumla.

"Sasa hivi kuna abiria wengi ambao wanaingia mkoani Mbeya kwa kupita njia za panya, na njia rahisi wanayotumia ni watu wa Bodaboda, hivyo tunawata msiingie kwenye vishawishi vya kutafuta hela ya haraka kwa kuwapitisha watu hao, jambo ambalo ni kinyume na Sheria" alisema

Mbali na hayo, Stafu Sajenti Valentino Ngowi amewataka madereva wote wa vyombo vya moto kuhakikisha wanafuata Sheria bila shurti, ikiwemo kuhakikisha abiria hawasimami kwenye magari (level seat), huku kwa upande wa Bajaj wapande abiria watatu tu.

Kampeni hii ya "Mikono safi, Tanzania salama" inaratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana ya Shirika lisilo la kiserikali la Oroject CLEAR. Katika kuchagiza ufikishaji wa elimu ya tahadhari dhidi ya Corona, Wizara inashirikiana na Msanii Mrisho Mpoto (Mjomba) kutoka Mjomba Theatre Gallery, ambae aliwakumbusha wakazi wa Jiji la Mbeya hususani maeneo ya Uyole, Sae, Ilomba, Mwanjelwa, Stendi Kuu, Meta, Nzovwe na Mbalizi kuzingatia unawaji wa mikono kwa maji na sabuni na vile vile kuepuka kushikana mikono na misongamano isiyokuwa na lazima. Ziara hii ya utoaji wa elimu ya tahadhari dhidi ya Corona inaendelea katika Mkoa wa Songwe ambao unapakana na nchi ya Zambia.

Mwisho.

Jumatano, 8 Aprili 2020

SERIKALI YAPOKEA MSAADA KUKABILIANA NA CORONA (COVID-19)



Na.WAMJW-Dar es Salaam

Ubalozi wa China nchini Tanzania umeipatia Serikali msaada wa vifaa kinga kwa ajili ya kuendelea kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Covid 19 (Corona), na kuahidi kuendelea kushirikian na Serikali ya Tanzania kukabiliana na ugonjwa huo, hadi hapo utakapomalizika.

Akipokea vifaa hivyo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema msaada huo utaenda kwa watumishi wa afya kote nchini kwani serikali imetoa kipaumbele cha kwanza kwao ili  kuweza kuwakinga na maambukizi ya Covid-19.

“kwa niaba ya serikali tunaishukuru sana Serikali ya China kwa mchango huu, na niendelee kuwathibitishia wale wote mnaoisaidia Serikali ya Tanzania,msaada huu tutaupeleka kwa watumishi wa afya,kipaumbele  ni kuwakinga watumishi wa afya wasipate maambukizi”

Ummy Mwalimu amesema msaada huo uliotolewa na ubalozi wa China nchini Tanzania ni pamoja na mavazi (PPE) 1,000 ya kujikinga wakati wa kuhudumia watu waliothibitika kuwa na ugonjwa wa corona, Barakoa (Mask) 100,000 pamoja na Vipima joto vya mkono(thermal scanner) 150.

Kwa upande wake balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Wang Ke amesema nchi yake na Tanzania ni marafiki kwa muda mrefu na ugonjwa huo ulipoikumba Nchi yao kwa mara ya kwanza, Tanzania ilikuwa mstari wa mbele kuwaunga mkono katika mapamabana dhidi ya  ugonjwa huo, hivyo na wenyewe wamejitoa kuisaidia kukabiliana nao.

Mhe.Wang Ke amesema Serikali ya China kwa sasa imechukua hatua na kujitoa rasmi kuwa nchi itakayoisaidia Tanzania katika misaada ya dharura ya vifaa kinga ambayo itasaidia kuweza kukabiliana na ugonjwa wa Corona.

Katika mwendelezo wa kuisadia vifaa kinga Serikali ya Tanzania, kwa mara nyingine tena  inatarajia kupokea msaada wa vifaa tiba vya kusaidia wagonjwa kupumua (Ventilator) 500 kutoka kwa mfanyabiashara raia wa China   Jack Ma.

MWISHO:

Jumatano, 1 Aprili 2020

"WATALAM WA AFYA ENDELEENI KUTOA ELIMU YA UGONJWA WA CORONA KWA WANANCHI" - DKT.NDUGULILE

- Hakuna maoni



Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo wakati akiongea na Wataalamu wa Sekta ya Afya ngazi ya Mkoa (hawapo kwenye picha) katika ofisi za mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na Wataalamu wa Sekta ya Afya ngazi ya Mkoa katika ofisi za mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akinawa mikono kwa maji safi tiririka na sabuni pindi alipowasiri katika kituo cha Afya Mkonze Jijini Dodoma kukagua jengo lililotengwa kwaajili ya washukiwa wa ugonjwa wa Corona endapo watatokea.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akikagua jengo la wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Muonekano wa chumba atakacholazwa mgonjwa wa Corona endapo atatokea, kilichopo katika jengo lililotengwa kwaajili ya wagonjwa hao katika kituo cha Afya Mkonze Jijini  Dodoma.

Jengo lililotengwa kwaajili ya matibabu ya ugonjwa wa Corona katika kituo cha Afya cha Mkonze Jijini Dodoma endapo mgonjwa atatokea.

Eneo lililotengwa kwaajili ya kuwatenga washukiwa wa ugonjwa wa Corona lililopo karibu na Chuo Kikuu cha Dodoma.

Na Rayson Mwaisemba, WAMJW-DOM

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewaasa Wataalamu wa Sekta ya Afya kuendelea kutoa Elimu kwa Wananchi kuhusu maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

Ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utayari wa kupambana dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona endapo utaingia Jijini Dodoma katika maeneo yote yaliyopangwa.

“Elimu bado haitoshi, kila siku ni lazima tuhakikishe tunatoa elimu kwenye jamii ili watu waweze kuelewa, watu waelewe ugonjwa huu maana yake ni nini, na kwanini tunasisitiza watu wanawe mikono, kwanini tunasisitiza maji tiririka na sabuni” alisema.

Amesema kuwa, ni muhimu kwa Wataalamu wa Sekta ya Afya kutoa Elimu ya kutosha kwa Wananchi, huku akisisitiza kuwa si kweli kwamba matumizi ya vitakasa mikono (sanitaizer) ni bora zaidi kuliko maji tiririka na sabuni.

“Si kweli kwamba Vitakasa mikono (Sanitaizer) ni bora zaidi kuliko kutumia maji tiririka na sabuni, tunahitaji tuwatoe hofu wanancni juu ya matumizi ya njia hizi mbili katika kujikinga dhidi ya ugonjwa huu.” Alisema.

Aliendelea kusisitiza kuwa, Wataalamu wa Sekta ya Afya kuongeza ubunifu katika kutoa elimu ili kuepuka upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu katika jamii juu ya kutibu maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Corona.

Aidha, Dkt. Ndugulile amewaagiza Wataalamu wa Sekta ya Afya kutumia njia nyepesi zaidi katika kutoa elimu ya ugonjwa wa Corona ili maambukizi haya yaweze kueleweka zaidi kwa Wananchi.

Mbali na hayo, Dkt. Ndugulile amesema kuwa, Serikali inaendelea kuleta mahitaji ya vifaa vyote vinavyohitajika katika maeneo yaliyotengwa kwa wagonjwa wa maambukizi ya virusi vya Corona endapo watatokea Jijini Dodoma.

“Niwahakikishieni vifaa vyote tutavileta, lakini pia niendelee kuwaomba tuwe imara muda wote, msisubiri ili kuweza kupambana na ugonjwa huu inabidi kuwa mbele muda wote” alisema.

Nae Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Best Magoma ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kuendelea kuboresha maeneo ya utayari na kuweka msisitizo katika maeneo yote ya muhimu ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa Corona endapo utatokea.

“Tunashukuru Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais TAMISEMI, kwa kutuunga mkono, wamekuwa karibu na sisi katika kutupa maelekezo na muelekeo wa nini chakufanya katika kuboresha Sekta ya Afya”alisema.

Dkt. Best Magoma, aliendelea kusema kuwa, katika ngazi ya Mkoa wataendelea kuboresha maeneo yote ambayo Wizara ya Afya kupitia Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndugulile ameelekeza katika zaira hiyo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Dkt. Faustine ndugulile amefanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Kituo cha Afya Mkonze na makazi ya chuo cha Dodoma, kukagua hali ya utayari wa kupambana dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona endapo utaingia.

MWISHO.

Jumatatu, 30 Machi 2020

ARUSHA YAZINDUA ZOAEZI LA KUPULIZA DAWA KUUWA VIJIDUDU NA KUWAKINGA ABIRIA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA CORONA

- Hakuna maoni
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akipuliza dawa ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa corona katika moja ya mabasi kwenye uzinduzi wa zoezi hilo uliofanyika stendi ya mabasi makubwa jijini humo.


Na Jusline Marco;ArushaMkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe.Gabriel Daqarro amezindua zoezi la upulizaji wa dawa ya kuuwa vijidudu kwa lengo la kuwakinga abiria na maambukizi ya virusi vya Corona pindi wanapotumia vyombo vya usafiri.

Zoezi hilo limezinduliwa leo rasmi kwa mabasi yanayotoka Jiji la Arusha kuelekea mikoa mingine , pamoja na vyombo vingine vya usafiri wa umma vinavyotumika katika safari za ndani ya Jiji la Arusha.

Mhe.Gabriel Daqaro amesema kuwa operesheni hiyo ya upulizaji wa dawa utakuwa endelevu na utashirikisha wadau ambao tayari wameanza kutoa michago yao kuwezesha zoezi hilo.

Aidha Daqarro amewataka wananchi kutokuwa na taharuki na hofu pamoja kuzusha maneno ya upotoshaji juu ya ugonjwa huo bali waachie mamlaka husika kutoa taarifa pamoja na elimu.

"Kuna watu wana dhana potofu wanasema Corona haiwezi kuwapata watu weusi hayo ni mawazo potofu kikubwa ni kuchukua tahadhari na kufata maagizo ya wataalamu wetu wa afya" amesema mkuu huyo wa wilaya.

Naye mganga mkuu wa jiji la Arusha Dr. kheri Kyaga amesema kuwa ni vyema wasafirishaji wote wakahakikisha abiria wanatumia vitakasa mikono au kusafisha mikono kwa maji tiririka kabla ya kupanda chombo cha usafiri ili wafike salama bila maambukizi ya ugonjwa huo.

Amesema kuwa maeneo ya stendi yanauwezekano mkubwa wa kuambukizana hivyo jukumu kuu ni kunawa mikono na kuepuka misongamano isiyo ya lazima kwani itasaidia kuepukana na janga hilo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha usafirishaji mkoa wa Arusha na Kilimanjaro (AKIBOA) Locken Adolf Massawe amesema zoezi la upuliziaji dawa vyombo vya usafirishaji ni endelevu na litahusisha vyombo vya usafiri wa jumuia ambapo bodaboda, magari makubwa na madogo.

" AKIBOA tutaendelea kushirikiana na Serikali katika vita dhidi ya ugonjwa huu"amesema.

Sambamba na mpango huo,Chama cha wasafirishaji abiria (AKIBOA) na wadau wa usafirishaji wametoa vifaa kinga vikiwemo vitakasa mikono pamoja na dawa za kupulizia vyombo vya usafiri vyenye gharama ya Shilingi milioni 7 ili kusaidia wananchi kujikinga dhidi ya virusi vya Corona.

WAZIRI MKUU APOKEA MISAADA YA SH. BILIONI 1.185 KUKABILIANA NA COVID-19

- Hakuna maoni
Waziri Mkuu,   Kassim Majaliwa akipokea hundi ya sh. milioni 230  ukiwa ni mchango wa Benki ya UBA wakati alipopokea michango kutoka kwa wadau mbalimbali  kwa ajili ya mapambano dhidi ya  ugonjwa wa CORONA, Machi 28, 2020. Kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, kushoto ni  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Usman Isaka na wa nne kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, Farhiya Warsama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  wakikagua jenereta lilitolewa na familia ya Karimjee  Jivanji ya jijini Dar es salam lenye thamani ya sh. milioni 75 wakati alipopokea michango kutoka kwa wadau mbalimbali  kwa ajili  ya mapambano dhidi ya  ugonjwa wa CORONA, Machi 28, 2020. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mussa Azan Zungu.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipima joto la mwili wakati alipowasili ofisini kwake  Magogoni jijini Dar es salaam kupokea michango kutoka kwa wadau mbalimbali  kwa ajili ya mapambano dhidi ya  ugonjwa wa CORONA, Machi 28, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisafisha mikono wakati alipowasili ofisini kwake  Magogoni jijini Dar es salaam kupokea michango kutoka kwa wadau mbalimbali  kwa ajil ya mapambano dhidi ya  ugonjwa wa CORONA, Machi 28, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa fedha pamoja na vitu mbali mbali kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) wenye thamani ya sh. bilioni 1.185 kutoka kwa wadau.

Amewataka Watanzania wote waendelee kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo ili kuzuia usisambae zaidi nchini. “Hii ni vita kubwa inahitaji tupigane kwa lengo la kuzuia janga hili lisisambae zaidi nchini, hivyo tuzingatie maagizo ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kumtaka kila Mtanzania ashiriki kwenye vita hii”

Amepokea msaada huo leo (Jumamosi, Machi 28, 2020) katika ofisi ndogo ya Waziri Mkuu iliyoko Magogoni, jijini Dar Es Salaam. Waziri Mkuu amewashukuru wadau hao na kuwataka Watanzania waendelee kushirikiana na Serikali katika hatua zinazochukuliwa kukabiliana na ugonjwa huo.

Miongoni mwa wadau waliotoa msaada huo ni taasisi za kifedha ikiwemo benki ya UBA Tanzania  iliyotoa sh. milioni 230, CRDB sh milioni 150 na  NMB sh milioni 100. Wadau wengine ni  Karimjee Jivanjee Ltd na kampuni zake tanzu waliotoa sh. milioni 200 pamoja na kuhaidi kufanyia matengenezo kinga ya magari yote ya Toyota yanayotumika katika kukabiliana na COVID-19 kwa muda ya siku saba bure, Familia ya Karimjee imetoa jenereta la KVA 180 lenye thamani ya sh. milioni 75.

Wengine ni Watoa Huduma ya Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) ambao wametoa bidhaa mbalimbali zikiwemo magari ya matangazo yatakayotumika kutoa elimu kwa muda wa miezi minne kupitia kampuni ya Advent Construction, maji ya kunywa (Bakhressa Group), Billboard (Ashton Media) vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya sh. milioni 150.

Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) walitoa matanki 1,000 yenye thamani ya sh. milioni 25, huku kila moja likiwa na ujazo wa lita 250, matanki hayo yametengenezwa maalumu kwa ajili ya kunawia mikono, pia Kampuni ya GS1 Tanzania Limited imetoa vitakasa mikono chupa 1,600 zenye thamani ya sh. milioni nne.

Kadhalika, Tanzania Oxygen ltd imetoa msaada wa sh. milioni 158 ambapo wamehaidi kufanyia ukarabati kiwanda kikubwa cha kuzalisha oxygen, Mount Meru imetoa vitakasa mikono vyenye thamani ya sh. milioni mbili, Hospitali ya Aga Khan imetoa dawa, sabuni, vitakasa mikono na vifaa tiba vyenye thamani ya sh. milioni 10.220.

Pia, kampuni ya gesi ya Oryx imehaidi kutoa msaada wa kusambaza gesi kwa ajili ya kupikia na matumizi mengine katika hospitali kama kufulia na kwenye vituo vya kuwahifadhi watu wanaohisiwa kuwa pamoja wagonjwa wa COVID-19. Gesi hiyo ina thamani ya sh. milioni 25, Tredea Cosmetics Ltd wametoa vitakasa mikono vyenye thamani ya sh.  milioni 1.6.

Umoja wa Mama lishe-Ilala na Machinga  wa Kariakoo wametoa sabuni na vitakasa mikono vyenye thamani ya sh. milioni mbili. Wakati huohuo, Chemba ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Wakulima (TCCIA) wametoa shuka 50, magodoro10, sabuni za maji chupa 170 na vitakasa mikono chupa 400 vyote vikiwa na thamani ya sh milioni tano.

Baada ya kupokea misaada hiyo, Waziri Mkuu kwa niaba ya Rais Dkt. Magufuli aliwashukuru wadau hao kwa vitu mbalimbali walivyovitoa kwa ajili ya kupambana na COVID-19 kwani vifaa pamoja na fedha walizozitoa zitaisadia Serikali katika kukabiliana na ugonjwa huo.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema Serikali kwa upande wake inaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kupambana na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha hausambai zaidi nchini. Alitumia fursa hiyo kuwashukuru madaktari, wauguzi pamoja na wataalamu wengine kwa huduma wanazozitoa.

Kuhusu wadau wengine wanaohitaji kutoa misaada, Waziri Mkuu amesema Ofisi yake iko wazi pia wanaweza kupeleka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na kwa wanalio nje ya nchi au sehemu yoyote wanaweza kutuma fedha kupitia akaunti  yenye Jina la: National Relief Fund Electronic  Akaunti Na: 9921159801

MAJALIWA : NIMERIDHISHWA NA MAANDALIZI YA KITUO

- Hakuna maoni

Waziri Mkuu, Kaasim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  (wa tatu kulia) wakati alipokagua hospitali ya wilaya ya kibaha iliyopo eneo la Lulanzi  ambayo imetengwa kwa ajili ya kuwahuduma kwa wagonjwa wa Coroma, Machi 28, 2020.  Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo  na wa pili kushoto ni  Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Muhammad Bakari.. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua wodi za hospitali ya wilaya ya Kibaha  iliyopo eneo la Lulanzi  ambayo imetengwa  kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wa Corona Mchi 28, 2020. Kushto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilio. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu 

Na Mwandishi Wetu - Pwani
 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea eneo lililotengwa kwa ajili kuwahudumia watu watakaobainika kuwa na maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) na amesema ameridhishwa na maandalizi.

Aliyasema hayo jana (Jumamosi, Machi 28, 2020) wakati akizungumza na wananchi wilayani Kibaha, Pwani baada ya kukagua hospitali ya wilaya ya Kibaha ambayo imetengwa kwa ajili ya kuwahudumia watu watakaogundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Alisema Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kukabilia na COVID-19, ambapo kwa sasa watu wote wanaoingia nchini kupitia viwanja vya ndege, vituo vya mabasi na bandari lazima wapimwe na wakigundulika wanamaambukizi wanawekwa kwenye maeneo maalumu kwa muda wa siku 14.

“Tunazingatia sana wale wanaotoka kwenye nchi ambazo zimeathirika sana wakiingia hapa Tanzania tunawazuia kwanza, tunawapima na tunafuatilia historia yake anatoka wapi na tunaangalia katika siku 14 amepita kwenye nchi zipi.”

Waziri Mkuu alisema wawaweka kwenye maeneo maalumu ili kuweza kuwapima kila siku na kujirishika kama hawana maambukizi kwani mtu anaweza kupimwa leo akaonekana yuko vizuri lakini ana maambukizi ambayo bado hayaonekani kwenye vipimo. Kama katika kipindi cha siku 14 mtu atabainika hana maambukizi anaruhusiwa kwenda kujiunga na familia.

Pia, alisisitiza wananchi waendelee kufuata maelekezo yaliyotolewa na Serikali kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kuzuia mikusanyiko na kwa wale wanaosafiri kwenye usafiri wa umma wasibanane kila mtu akae kwenye kiti.

Waziri Mkuu alisema wananchi wanapokwenda kufuata huduma kwenye masoko wahakikishe wanapeana nafasi baina ya mtu mmoja na mwingine na kabla hawajaingia katika maduka wanawe mikono kwa sabuni na maji tiririka ili kujikinga na maambukizi ya corona.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu alisema Serikali imeanza kuwachukulia hatua watu wote wanaopotosha kuhusu taarifa za ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19). “Aliyetangaza kuwa shule zinafunguliwa tumeshamkamata na atachukuliwa hatua.”

Hivyo aliwataka wananchi wajihadhari na taarifa zinazotolewa na watu ambao si wasemaji rasmi. Alisema taarifa kuhusu virusi vya corona itatolewa na Waziri Mkuu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Msemaji wa Serikali.

Alhamisi, 26 Machi 2020

HADI SASA TUMEWEZA KUDHIBITI MAAMBUKIZI YA NDANI KWA NDANI YA CORONA-WAZIRI UMMY

- Hakuna maoni
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto, Ummy Mwalimu, akieleza jambo, wakati akiongea na Waandishi wa Habari juu ya mwenendo wa ugonjwa wa Corona (COVID-19) Jijini Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto, Ummy Mwalimu, akiwa na Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid na Naibu Katibu Mkuu wake wakati akiongea na Waandishi wa Habari juu ya mwenendo wa ugonjwa wa Corona (COVID-19) Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula wakifuatilia neno kutoka kwa Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu (hayupo kwenye picha, wakati akiongea na Waandishi wa Habari juu ya mwenendo wa ugonjwa wa Corona (COVID-19) Jijini Dodoma.



HADI SASA TUMEWEZA KUDHIBITI MAAMBUKIZI YA NDANI KWA NDANI YA CORONA-WAZIRI UMMY
Na WAMJW-DOM

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto, Ummy Mwalimu, amebainisha kuwa, hadi sasa Tanzania imeweza kudhibiti maambukizi ya ndani kwa ndani ya ugonjwa (COVID-19) na kuwasisitiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zote za kujikinga.
 
Amesema, wasafiri 245 walioingia Tanzania Bara na Zanzibar tangu Machi 23, mwaka huu, wametengwa kwenye hoteli na maeneo yaliyoandaliwa na Serikali kwa gharama zao.
 
Waziri Ummy ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa Corona nchini.
 
Amesema hadi sasa hakuna maambukizi ya ndani (Local transmission) na wagonjwa 13 waliothibitika kuwa na virusi vya ugonjwa huo wanaendelea vizuri.
 
“Hatua mbalimbali zimechukuliwa kwa lengo lakutimiza dhamira nzuri ya serikali ya kupunguza hatari ya kusambaa kwa haraka maradhi haya nchini, tunashukuru Mungu bado hatuna ‘Local transmission,”amesema.
 
Aidha, amesema mgonjwa wa kwanza wa Arusha, amepona Corona na taratibu za kumruhusu kurudi nyumbani zinaendelea.
 
“Mgonjwa wetu amepona COVID19 na amepimwa mara tatu hana, tumeanza utaratibu wa kumrudisha nyumbani, kazi ambayo nimemuelekeza Katibu Mkuu aifanye sasa hivi suala la kutoa elimu ili kuondoa unyanyapaa, kulaumiana na kunyoshewa vidole Isabela,” amesema.
 
Kadhalika, amesema wasafiri hao 245 wamewekwa karantini kwa siku 14 kwenye maeneo maalum ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais, Dkt.John Pombe Magufuli.
 
“Tangu agizo la Rais wasafiri 111 kwa Tanzania barana 134 kwa Zanzibar wametengwa kwenye hayo maeneo, na tunasisitiza mikoa yote nchini kuendelea na zoezi la kubainisha sehemu zitakazo tumika kuweka wasafiri bila kuleta usumbufu usio wa lazima,”amesema. 
 
Pamoja na hayo, Waziri huyo amesema Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wizara ya Afya ya Zanzibar imeendelea kufanya ukaguzi kwa kupima joto lamwili kwa wasafiri wote wanaoingia nchini.
 
“Kuanzia Januari mosi mwaka huu hadi sasa wasafiri 1,890,532 wamefanyiwa ukaguzi wa kupimwa joto kwenye vituo 27 vya mipakani ikiwemo viwanja vya ndege na bandarini na kwa saa 24 zilizopita jumla yawasafiri 3,471 wamefanyiwa ‘screening’,”amesema.
 
Amefafanua kuwa watu 273 wamepimwa sampuli za kupima virusi vya Corona katika Maabara Kuu ya Taifa ya Afya ya Jamii hadi Machi 26,2020.
 
“Kati ya sampuli hizo zilizopimwa 260 hazikuonesha uwepo wa virusi hivyo na sampuli 13 zilithibitika kuwa na virusi, wagonjwa hawa ni kutoka Mkoa wa Arusha (2), Dar es salaam(8), Zanzibar (2) na Kagera (1),”amesema.
 
Katika hatua nyingine, Waziri huyo ameshukuru msaada wa vifaa mbali mbali ikiwemo vya kupima virusi haraka (Rapid test kits) kutoka kwa Taasisi zilizopo Jamhuri ya watu wa China za Jack Ma na Alibaba na vitasambazwa kwenye hospitali zilizotengwa maalum kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa hao.
 
Waziri Ummy amesema maabara iliyopo haijazidiwa na utaratibu mzuri umeandaliwa wa upimaji wa sampuli kutoka mikoani.
 
Aidha, amesema serikali inatarajia kuongeza maabara sita na Zanzibar moja.
 
“Tumeona pia kuna haja ya kuongeza maabara, tayari maabara ya Chuo Kikuu Sokoine (Sua) inaweza kupima sampuli, pia maabara za NIMR Mbeya, Tanga, Mwanza na Arusha ile maabara ya St.Nelson Mandela, hili tumeliona lakini tumeona kuna haja ya kuwa na ‘rapid test’, tupo vizuri hatujazidiwa na sampuli zinafika kwa wakati kwenye maabara yetu,”amesema.
 
Waziri huyo amesema vipimo vya kupima virusi kwa haraka vitawekwa kwenye Hospitali za Mikoa, Kanda na kwenye mipaka.
 
“Jumuia ya ya Afrika Mashariki pia jana tumepata msaada wa maabara zinazotembea, na tuta pata mbili kwa Tanzania ambazo zitapelekwa Arusha na Zanzibar,”amesema.
 
Naye, Waziri wa Afya Zanzibar, Hamad RashidMohammed, amewataka Watanzania kujikinga na ugonjwa huo huku akisisitiza kuwa Serikali haina nia ya kumuweka mtu kambini kumtesa.
 
Mwisho.

Jumatano, 25 Machi 2020

SERIKALI YAPOKEA MSAADA WA VIFAA VYA KUKABILIANA NA CORONA (COVID-

- Hakuna maoni
Mganga Mkuu wa  Serikali, Prof. Muhammed Bakari Kambi
akipokea msaada wa vifaa kinga kutoka China kwaajili ya kusaidia kukabiliana na Corona.
 
SERIKALI imepokea msaada wa vifaa kinga kutoka China kwa ajili ya kusaidia kukabiliana na mlipuko wa maambukizi ya homa kali ya mapafu inayoambukizwa na virusi vya Corona (COVID-19) kutoka taasisi ya Jack Ma na Alibaba.

Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Serikali, Mganga Mkuu wa  Serikali, Prof. Muhammed Bakari Kambi amesema msaada huo ambao umetolewa na Taasisi ya Jack Ma na Alibaba ni pamoja na mavazi (PPE) 1,000 ya kujikinga wakati wa kuhudumia watu waliobainika kuwa na ugonjwa huo ni pamoja na vitendanishi (Rapid Tests) 20,000 na Barakoa (Masks) 100,000.

Prof. Muhammed amesema msaada huo utawasaidia wataalamu wa afya nchini wakati wa kuwahudumia waliobainika na watakaobainika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona. 

Vifaa kinga vya msaada kutoka China kwa ajili ya kusaidia kukabiliana na mlipuko wa maambukizi ya homa kali ya mapafu inayoambukizwa na virusi vya Corona (COVID-19).


“Tunashukuru kwa msaada huo kama serikali,tumekuja hapa kushuhudia sehemu ya shehena ya tani tatu ya vifaa-tiba vilivyotolewa na Taasisi ya Jack Ma na Alibaba ambavyo vimewasili usiku wa leo na ndege ya mizigo ya Jamhuri ya Shirikisho la Kidemokrasia Ethiopia,” amesema Prof. Muhammed.

Katika hatua nyingine, Prof. Muhammed amemshukuru Afisa Ubalozi wa Jamhuri ya Shirikisho la Kidemokrasia Ethiopia Ndg. Tewodros Girma ambaye amekabidhi msaada huo kwa niaba ya Balozi wa nchi hiyo, Mhe. Yonas Yosef. 

MWISHO.