Waziri Mkuu, Kaasim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wa tatu
kulia) wakati alipokagua hospitali ya wilaya ya kibaha iliyopo eneo la
Lulanzi ambayo imetengwa kwa ajili ya kuwahuduma kwa wagonjwa wa
Coroma, Machi 28, 2020. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi
Evarist Ndikilo na wa pili kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa
Muhammad Bakari.. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua wodi za hospitali ya
wilaya ya Kibaha iliyopo eneo la Lulanzi ambayo imetengwa kwa ajili
ya kuwahudumia wagonjwa wa Corona Mchi 28, 2020. Kushto ni Mkuu wa Mkoa
wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilio. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Na Mwandishi Wetu - Pwani
WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa ametembelea eneo lililotengwa kwa ajili kuwahudumia watu
watakaobainika kuwa na maambukizi ya homa kali ya mapafu
inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) na amesema ameridhishwa
na maandalizi.
Aliyasema hayo
jana (Jumamosi, Machi 28, 2020) wakati akizungumza na wananchi wilayani
Kibaha, Pwani baada ya kukagua hospitali ya wilaya ya Kibaha ambayo
imetengwa kwa ajili ya kuwahudumia watu watakaogundulika kuwa na
maambukizi ya virusi vya corona.
Alisema Serikali
imeendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kukabilia na COVID-19,
ambapo kwa sasa watu wote wanaoingia nchini kupitia viwanja vya ndege,
vituo vya mabasi na bandari lazima wapimwe na wakigundulika
wanamaambukizi wanawekwa kwenye maeneo maalumu kwa muda wa siku 14.
“Tunazingatia
sana wale wanaotoka kwenye nchi ambazo zimeathirika sana wakiingia hapa
Tanzania tunawazuia kwanza, tunawapima na tunafuatilia historia yake
anatoka wapi na tunaangalia katika siku 14 amepita kwenye nchi zipi.”
Waziri Mkuu
alisema wawaweka kwenye maeneo maalumu ili kuweza kuwapima kila siku na
kujirishika kama hawana maambukizi kwani mtu anaweza kupimwa leo
akaonekana yuko vizuri lakini ana maambukizi ambayo bado hayaonekani
kwenye vipimo. Kama katika kipindi cha siku 14 mtu atabainika hana
maambukizi anaruhusiwa kwenda kujiunga na familia.
Pia, alisisitiza
wananchi waendelee kufuata maelekezo yaliyotolewa na Serikali kwa ajili
ya kujikinga na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kuzuia mikusanyiko na kwa
wale wanaosafiri kwenye usafiri wa umma wasibanane kila mtu akae kwenye
kiti.
Waziri Mkuu
alisema wananchi wanapokwenda kufuata huduma kwenye masoko wahakikishe
wanapeana nafasi baina ya mtu mmoja na mwingine na kabla hawajaingia
katika maduka wanawe mikono kwa sabuni na maji tiririka ili kujikinga na
maambukizi ya corona.
Wakati huo huo,
Waziri Mkuu alisema Serikali imeanza kuwachukulia hatua watu wote
wanaopotosha kuhusu taarifa za ugonjwa wa homa kali ya mapafu
inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19). “Aliyetangaza kuwa
shule zinafunguliwa tumeshamkamata na atachukuliwa hatua.”
Hivyo aliwataka
wananchi wajihadhari na taarifa zinazotolewa na watu ambao si wasemaji
rasmi. Alisema taarifa kuhusu virusi vya corona itatolewa na Waziri
Mkuu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja
na Msemaji wa Serikali.
0 on: "MAJALIWA : NIMERIDHISHWA NA MAANDALIZI YA KITUO"