Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Magonjwa Ambukizi Kibong'oto Dkt. Riziki Kisongo akisema jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na Kifua Kuu.
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya Dkt. Leonard Subi akisema jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na Kifua Kikuu (hawapo kwenye picha) mara baada ya kufanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Magonjwa Ambukizi (Kibong'oto)
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na Kifua Kikuu Mhe. Oscar Mukasa akisema jambo kwa wajumbe wa kamati na wataalam katika kikao mara baada ya kufanya ziara katika Hospitali ya Magonjwa Ambukizi ya Kibkng'oto. Aliye upande wa kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Siha, Onesmo Buselu.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na Kifua Kikuu Dkt. Mwigulu Nchemba (MB) akichangia hoja katika kikao na wataalam mara baada ya kufanya ziara katika Hospitali ya Magonjwa Ambukizi ya Kibong'oto.
Mkurugenzi,wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi (kushoto) akiwa pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya, na Kifua Kikuu wakizungumza na wagonjwa wa Kifua Kikuu sugu katika Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Magonjwa Ambukizi - Kibong'oto.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na Kifua Kikuu na wataalam wakiwa wamevalia barakoa (mask) kujilinda na maambukizi ya Kifua Kikuu sugu kabla ya kuelekea kwenye wodi za wagonjwa wa Kifua Kikuu sugu katika Hospitali ya Taifa ya Magonjwa ambukizi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Magonjwa Ambukizi (Kibong'oto) Dkt. Riziki Kisongo akiwaelekeza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na Kifua Kikuu namna ya kuvaa barakoa (mask) kabla ya kuelekea kwenye wodi za wagonjwa wa Kifua Kikuu sugu hospitalini hapo. Aliye upande wa kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Siha, Onesmo Buselu
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na Kifua Kikuu Dkt. Jasmine Tisekwa (kulia) akizungumza na mtoto Kidawa Baraza mwenye umri wa miaka 10 (kushoto) anayepata matibabu ya ugonjwa wa Kifua Kikuu Sugu katika Hospitali ya Kibong'oto
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na Kifua Kikuu (kushoto) akizungumza na watoto wagonjwa wa Kifua Kikuu sugu wanaopata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Magonjwa Ambukizi Kibong'oto, Kilimanjaro.
Na Englibert Kayombo WAMJW – Kilimanjaro.
Tafiti za magonjwa ambuzuki kutoka Hospitali
ya Rufaa ya Taifa ya Magonjwa Ambukizi (Kibong’oto) zimesaidia Shirika la Afya Duniani
(W.H.O) kubadilisha miongozo ya kutibu na kugundua vimelea vya ugonjwa wa Kifua
Kikuu.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Dkt. Riziki Kisongo wakati akiwasilisha
taarifa ya Hospitali hiyo kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania ya masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na Kifuaa
Kikuu.
"Tuna machapisho ya kisayansi 50
ambayo tumeyayachapisha kwenye majarida ya kimataifa, kati ya machapisho hayo;
mawili yamechangia kwenye kubadilisha miongozo ya kutibu na kugundua vimelea
vya ugonjwa wa Kifua Kikuu” amesema Dkt. Riziki
“Mwaka 2009 ilikuwa inachukua siku 392 ili mtu
kugundulika kuwa ana ugonjwa wa Kifua Kikuu toka aende hospitali’ anasema Dkt.
Riziki na kusema kuwa kupitia watafiti waliweza kutengeneza miongozo ambayo
ilitoa dira ya kuwa na haja ya kuwa na vipimo vipya ambavyo vingepunguza muda
wa kugundua mgonjwa wa Kifua Kikuu.
“Miongozo imesaidia kuja kwa vipimo
vya kisasa vya ugonjwa wa Kifua Kikuu “GeneXpert
Mashines” ambazo zinachukua masaa mawili na nusu kepee kufanya vipimo vya
ugonjwa wa Kifua Kikuu” Amesema Dkt. Riziki.
Andiko lingine lililobadili tiba ya
ugonjwa wa Kifua Kikuu amesema kuwa kupitia machapisho hayo, tiba ya ugonjwa wa
Kifua Kikuu imebadilika na sasa wagonjwa wanatibiwa kupitia dawa na sii sindano
kama ilivyokuwa awali.
“Tiba ya ugonjwa wa Kifua Kikuu
ilikuwa ni kwa njia ya sindano kwa muda wa miezi nane, utafiti ulivyofanyika hapa
ilionekana asilimia 47 ya wagonjwa walikuwa wanapata matatizo ya usikivu”
anasema Dkt. Riziki na kuendelea kusema kuwa kwa kuchapisha maandiko hayo
yalisaidia kubadili tiba ya ugonjwa huo ambapo hadi hivi sasa tiba inatolewa
kwa vidonge.
Naye Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi amesema kuwa Tanzania
ni mojawapo ya nchi inayofanya vizuri kwenye matibabu ya TB ambapo hadi hivi
sasa ina vituo 145 vya matibabu ya Kifua Kikuu sugu nchi nzima, tofauti na
awali ambapo ilikuwa na Hospitali ya Kibong’oto pekee.
“Lengo la kuwa na Hospitali ya
Kibong’oto sio kwa ajili ya kutoa tiba pekee bali wanatakiwa kubobea kwenye
tafiti, tiba na matokeo chanya kwa Taifa na Dunia kwa ujumla” amesema Dkt. Subi
na kuendelea kusema kuwa Wizara ya Afya imeongezewa uwezo Hospitali hiyo wa
kushughulikia magonjwa yote ambukizi, tafiti na ufuatiliaji.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi, Madawa ya Kulevya na Kifua Kikuu Mhe.
Oscar Mukasa amefurahi kusikia Hospitali hiyo inatoa mchango wa mabadiliko ya
sera za matibabu ya magonjwa kutokea Tanzania na kuwasihi waongeze juhudi zaidi
na kuja na tafiti nyingi zaidi zitakazo saidia katika kupata tiba ya ugonjwa
huo ambao bado ni tatizo kubwa kwa Watanzania.
Mwisho
Tafiti ni nzuri sana kufanyika, na pia matokeo yake tunaomba yawekwe pia katika lugha inayoeleweka na watu wote (Kiswahili sahili) ili kusaidia uelewa mpana wa wananchi.
JibuFutaTena kutokana na tabia ya kutosoma kwa maelezo marefu ingewezekana ziwekwe katika video na infographic mbalimbali. Ahsante