Dkt. Erasmus Mndeme Mkurugenze Mtendaji Hospitali ya Magonjwa ya Akili - Milembe akiwasilisha taarifa yake kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya (hawapo pichani)
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya Mhe. Oscar Mukasa akisema jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) walipotembelea Kituo cha kutolea tiba ya madawa ya kulevya Itega, Jijini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya wakiwasilikiza waraibu wa madawa ya kulevya katika kituo cha kutolea tiba ya madawa ya kulevya Itega, Jijini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati ya Kuduma ya Bunge ya masuala ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya wakimsikiliza mtaalam katika kituo cha kutolea tiba ya madawa ya kulevya -Itega, Jijini Dodoma.
Picha ya pamoja ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya masuala ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya na wataala walipofanya ziara kwenye kituo cha tiba ya madawa ya kulevya - Itega Jijini Dodoma
Na Englibert Kayombo WAMJW – Dodoma.
Serikali kupitia
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto iko mbioni
kuanzisha huduma shikizi za tiba ya methadone kwa waathirika wa madawa ya
kulevya ya Heroine.
Hayo
yamesemwa na Dkt. Erasmus Mndeme Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Rufaa ya
Kitaifa ya Magonjwa ya Akili - Milembe alipokuwa akiwasilisha taarifa ya huduma
za tiba kwa waathirika wa madawa ya kulevya kupitia dawa ya methadone na
utekelezaji wa majukumu ya Kituo cha kuhudumia waathirika wa madwa ya kulevya
cha Itega Jijini Dodoma kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na
Madawa ya Kulevya walipofanya ziara ya ukaguzi wa huduma katika Kitui hicho.
“Kumekuwa
na msongamano mkubwa katika maeneo yanayotoa huduma za methadone kwenye Jiji la
Dar Es Salaam ambapo kwa sasa kwenye kliniki zote tatu idadi ya wagonja
imeongezeka maradufu” anabainisha Dkt. Mndeme
Amesema
kuwa hali hiyo imechagiza waratibu wa huduma hizo katika ngazi ya Taifa
kufikiria mbinu mbadala ya kuboresha huduma hizo nchini.
“Mojawapo
ya mbinu zilizokubalika katika kukabiliana na changamoto hii ni uanzishwaji wa
satellite kliniki nne kwenye ngazi ya Halmashauri na kituo kimoja kwenye gereza
la Seregea ifikapo 2020” amesema Dkt. Mndeme.
Dkt. Mndeme
amesema kuwa mkakati wa uanzishwaji wa Satellite kliniki unalenga kupunguza
msongamano kwenye kliniki na kutoa mwanya kwa watoa huduma kuwa na muda zaidi
wa kuwaona wagonjwa na kuwapa huduma stahiki.
Amesema
kuwa kupeleka huduma kwenye Halmashauri itasaida waathirika kupata huduma
karibu na makazi yao.
Hata hivyo
Dkt. Mndeme amesema kuwa Serikali imeandaa mkakati wa awamu ya pili ya
upatikanaji wa huduma za kutoa dawa kwa waathirika “Methadone” kwa mwaka
2019-2020 huku huduma zikisogezwa kwenye mikoa ya Tanga, Pwani, Morogoro,
Dodoma, Arusha na Kilimanjaro huku huduma zikiwa zimeanza kutolewa kwenye mikoa
ya Dodoma na Pwani.
Aidha kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kuduma ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na
Madawa ya Kulevya Mhe. Oscar Mukasa ameonyesha kufurahishwa na mkakati huo
ambao utasaidia upatikanaji wa huduma kwa waraibu wa madawa ya kulevya na kuwataka
wataalam kuongeza nguvu katika mapambano ya madwa ya kulevya na magonjwa ya
kuambukiza baina ya waathirika wa madawa ya kulevya yakiwemo maambukizi ya
Virusi vya Ukimwi na ugonjwa wa kifua kikuuna na homa ya ini miongoni mwa
waathirika wa madawa ya kulevya.
0 on: "SERIKALI KUANZISHA KLINIKI SHIKIZI NNE ZA KUTOLEA HUDUMA ZA METHADONE KWA WAATHIRIKA WA MADAWA YA KULEVYA."