Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatatu, 2 Machi 2020

TANZANIA INAFANYA VIZURI KWENYE KUPUNGUZA TB KWA ASILIMIA 75




Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula akiongea na wataalam kutoka ndani na nje ya nchi (hawapo pichani) wakati wa kupokea ripoti ya tathimini ya mapitio ya mpango mkakati wa TB na Ukoma

Kaimu Meneja Mpango wa Taifa wa kudhibiti na kutokomeza Kifua Kikuu na Ukoma Dkt. Zuweina Kondo akiongea kuhusu utekelezaji wa mpango mkakati wa kutokomeza magonjwa hayo ambapo tanzania imefanikiwa kwa asilimia 75

Baadhi ya washiriki wa tathimini kutoka nchini na nje ya nchi wakimsikiliza Katibu Mkuu

Na. Catherine Sungura-Dodoma.
Tanzania ni moja ya nchi mbili afrika zinazofanya vizuri katika kupunguza maambukizi,kutibu pamoja na kupona ugonjwa wa kifua kikuu “TB” na hivyo kufikia asilimia 75 ya malengo yaliyowekwa.
Hayo yameelezwa leo na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto-Idara kuu Afya Dkt. Zainabu Chaula wakati wa mkutano wa kupokea ripoti ya tathimini ya mapitio ya mpango mkakati wa kifua na ukoma uliofanyika jijini hapa.
“Shirika la Afya Duniani (WHO) limekuja kufanya tathimini kwa kushirikia na wataalam wengine kutoka nje na ndani ikiwa ni kuona jinsi gani  tumeyafikia malengo tuliyojiweke kwenye mpango mkakati wetu wa mwaka 2015  ikiwemo kuongeza kasi ya kuwafikia wagonjwa kwa asilimia 29 zaidi”.
Amesema kuwa tathimini hiyo ilikua ikiangalia  malengo ya kidunia ya kumaliza tatizo la Tb pamoja na ukoma,“asilimia nyingine tumepewa malezo na tutaenda kuyaweka kwenye mpango mkakati mwingine tunaoenda kuuandaa na kuweza  kushughulikia”.Aliongeza Dkt. Chaula
Hata hivyo Katibu Mkuu huyo alisema bado kuna changamoto ya uelewa kwa wananchi kwani ugonjwa wa TB unaenezwa kwa hewa hivyo alishauri wananchi kuepuka misongamano,kulala kwenye nyumba zenye madirisha yenye hewa , kuzingatia usafi wa mazingira na kwa watu wenye dalili ni vyema kuwahi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kupata matibabu kwani huduma za TB zinapatikana kuanzia ngazi za zahanati.
Naye Kaimu Meneja wa Mpango wa Taifa  wa kudhibiti na kutokomeza Kifua Kikuu na Ukoma (NTLP) Dkt. Zuweina Kondo amesema kuwa wamefanikiwa kugundua wagonjwa kutoka asilimia 37 mwaka 2015 hadi asilimia 53 hivi sasa.
“Tulikua tumeweka mkakati wa kuwafikia wagonjwa na tumefikia kwa asilimia 43 zaidi kwa mwaka 2018 tuliwafikia wagonjwa 75545 na mwaka 2019 tuliwafikia wagonjwa 82140 , kadri unavyogundua wagonjwa wengi ndio utastopisha yale  maambukizi”
Kwa upande wa watoto Dkt. Zuweina  amesema kuwa wameweza kufikia lengo la WHO kwa asilimia 15 ambalo ni lengo la juu lililotajwa kidunia ambapo Tanzania ni kati ya nchi saba ambazo zipo katika kufikia malengo ya kidunia ya mwaka  2020 ya kupunguza maambukizi mapya kwa kila mwaka kwa asilima nne (4) ukilinganisha na asilimia mbili (4) kwa nchi nyingine ambazo ni kiwango cha kawaida.
Dkt. Zuweina amesema kwa upande wa ukoma hivi sasa wameweza kuondoa ugonjwa huu kutoka halmashauri za wilaya  19 mwaka 2015  kubakiza  halmashauri 16 hivyo wanajipanga kuondoa kwenye halmashauri zilizobaki kwa kuendeleza kutoa elimu na kutafuta njia nyingine za kuwafikia wagonjwa.
-Mwisho-

0 on: "TANZANIA INAFANYA VIZURI KWENYE KUPUNGUZA TB KWA ASILIMIA 75"