Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumanne, 14 Aprili 2020

MADEREVA CHUKUENI TAHADHARI DHIDI YA CORONA

Mratibu wa kampeni ya "Mikono safi, Tanzania salama" kutoka Wizara ya Afya Ndg. Anyitike Mwakitalima akitoa maelekezo kutoka kwa moja kati ya dereva boda boda katika eneo la kituo cha daladala cha Kabwe Jijini Mbeya ikiwa ni mwendelezo wa kampeni maalum ya uhamasishaji jamii kuchukua hatua za tahadhari dhidi ya maambukizi ugonjwa wa Corona Jijini Mbeya. 

Kondakta wa basi linalofanya safari ya Kyela akimsaidia abilia wake kutaka mikono kwa sanitizer kabla ya kuingia kwenye gari katika kituo cha mabasi Nanenane Jijini Mbeya, ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Corona yasisambae kwa abilia wengine endapo yatatokea.

Mkazi wa Mbalizi Jijini Mbeya akisafisha mikono kwa maji safi yanayotiririka na sabuni kabla yakuingia dukani kufanya manunuzi ikiwa ni sehemu ya kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona.

Mratibu wa kampeni ya "Mikono safi, Tanzania salama" kutoka Wizara ya Afya Ndg. Anyitike Mwakitalima akinawa mikono kwa sabuni na maji safi yanayotiririka katika chuo cha MUST Jijini Mbeya, ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona nchini.
Waratibu wa kampeni ya "Mikono safi, Tanzania salama" kutoka Wizara ya Afya Shirika lisilo Lakiserikali Project CLEAR na Mpoto Gallery wakitoa Elimu kwa madereva bodaboda wa Mbalizi Mbeya wakati wa kampeni maalum ya uhamasishaji jamii kuchukua hatua za tahadhari dhidi ya maambukizi ugonjwa wa Corona.

Kushoto ni Meneja wa Peter Hoteli Jijini iliyopo Jijini Mbeya, akikabidhiwa zawadi ya sabuni na vitakasa mikono (sanitizer) kutoka kwa mfanya kazi wa Shirika lisilo Lakiserikali Project CLEAR Bi Viola baada ya Waratibu wa Kampeni hiyo kutoka Wizara ya Afya kuridhishwa na hatua zinazochukuliwa na Hoteli hiyo kupambana dhidi ya ugonjwa wa Corona. 

Mkazi wa Mbalizi Jijini Mbeya aliyejishindia zawadi wa kitenge baada ya timu ya kampeni maalum ya uhamasishaji jamii kuchukua hatua za tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona kutoka Wizara ya Afya kumkuta akichukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo kwa kunawa mikono kwa maji safi yanayotiririka.

Timu ya kampeni maalum ya uhamasishaji jamii kuchukua hatua za tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona kutoka Wizara ya Afya ikiendelea na kazi ya uhamasishaji katika eneo la kituo kikuu cha mabasi ya Mkoani Jijini Mbeya ili wananchi waendelee kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona.


MADEREVA CHUKUENI TAHADHARI DHIDI YA CORONA

Na Rayson Mwaisemba, WAMJW- MBEYA

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeendelea kuwaasa madereva wa vyombo vya usafiri kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Kitengo cha Maji na Usafi wa Mazingira kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ndg. Anyitike Mwakitalima wakati wa uhamasishaji kwa wananchi wa kuchukua hatua za tahadhari dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona katika Mikoa ya Mbeya na Songwe.

Amesema kuwa, kila dereva na kondakta wake ni lazima wahakikishe gari linakuwa na vitakasa mikono (Sanitizer) kwa ajili ya matumizi yao na abiria. Aidha, vituo vyote vya mabasi viwe na sehemu za kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni kwa hii ni hatua muhimu sana ya kujikinga na virusi vya Corona. Aliyasema hayo alipotembelea Stendi Kuu ya mabasi katika Jiji la Mbeya iliyopo eneo la Nane Nane.

"Kondakta hakikisha kila anaepanda gari lako amenawa mikono kwa sabuni na maji safi yanayotiririka au ametakasa mikono yake kwa Sanitizer ndio aruhusiwe kuingia kwenye gari, huu ugonjwa jamani ni hatari na umeua watu wengi" alisema.

Aidha, amewaagiza madereva na makondakta wao kuhakikisha kila siku jioni wanapokuwa wamemaliza kazi zao wahakikishe wanasafisha magari yao kwa dawa maalum aina ya Jiki, ili kuua virusi vinavyoweza kuwepo na kupelekea maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

"Madereva na makondakta wote kila siku jioni, hakikisha mnasafisha magari yenu kwa dawa maalum, wote mnaifahamu Jiki hapa, dawa hii inatumika Kutakasa magari, bajaji au pikipiki. Changanya kipimo kimoja cha Jiki na vipimo Sita (6) vya maji ili kupata mchanganyiko unaotakiwa kisha osha chombo chako cha kusafirisha abiria, utajikinga wewe na abiria wako " alisema.

Nae, Afisa kutoka Makao Makuu Jeshi la Polisi Kamisheni ya Ushirikishaji Jamii Stafu Sajenti Valentino Ngowi, amewataka madereva bodaboda kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi endapo watakutana na mtu alieingia nchini kwa njia za panya, ikiwa ni moja ya jitihada za kupambana na ugonjwa wa Corona, huku akiwataka wasiingie katika vishawishi vya kutaka pesa ya haraka ambayo inaweza kuwagharimu wao na taifa kwa jumla.

"Sasa hivi kuna abiria wengi ambao wanaingia mkoani Mbeya kwa kupita njia za panya, na njia rahisi wanayotumia ni watu wa Bodaboda, hivyo tunawata msiingie kwenye vishawishi vya kutafuta hela ya haraka kwa kuwapitisha watu hao, jambo ambalo ni kinyume na Sheria" alisema

Mbali na hayo, Stafu Sajenti Valentino Ngowi amewataka madereva wote wa vyombo vya moto kuhakikisha wanafuata Sheria bila shurti, ikiwemo kuhakikisha abiria hawasimami kwenye magari (level seat), huku kwa upande wa Bajaj wapande abiria watatu tu.

Kampeni hii ya "Mikono safi, Tanzania salama" inaratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana ya Shirika lisilo la kiserikali la Oroject CLEAR. Katika kuchagiza ufikishaji wa elimu ya tahadhari dhidi ya Corona, Wizara inashirikiana na Msanii Mrisho Mpoto (Mjomba) kutoka Mjomba Theatre Gallery, ambae aliwakumbusha wakazi wa Jiji la Mbeya hususani maeneo ya Uyole, Sae, Ilomba, Mwanjelwa, Stendi Kuu, Meta, Nzovwe na Mbalizi kuzingatia unawaji wa mikono kwa maji na sabuni na vile vile kuepuka kushikana mikono na misongamano isiyokuwa na lazima. Ziara hii ya utoaji wa elimu ya tahadhari dhidi ya Corona inaendelea katika Mkoa wa Songwe ambao unapakana na nchi ya Zambia.

Mwisho.

0 on: "MADEREVA CHUKUENI TAHADHARI DHIDI YA CORONA"