Na
WAMJW – Dar es Salaam
Serikali
imepongezwa kwa jitihada inazozifanya katika kukabiliana na ugonjwa
unaosababishwa na Virusi vya Corona (COVID-19) hapa nchini.
Pongezi
hizo zimetolewa leo jijini Dar es Salaam na mwakilishi wa Ubalozi wa Pakistani
hapa nchini Muhammad Saleem wakati akikabidhi vifaa vya kujikinga na ugonjwa
huo kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Saleem
alisema tangu ugonjwa huo ulipoingia hapa nchini mwezi uliopita kasi
ya maambukizi ni ndogo ukilinganisha na nchi zingine, hiyo yote ni kutokana na
hatua thabiti zinazofanywa na Serikali katika kukabiliana na ugonjwa huo.
“Nchi
yetu ya Pakistani imekuwa na ushirikiano mzuri na Tanzania, hivyo
basi tumeona nasi tutoe msada wa vifaa kinga. Tunaomba mpokee
mchango wetu ambao ni kidogo ili watoa huduma wa afya waweze kutumia vifaa hivi
wakati wanawahudumia wagonjwa kwani ugonjwa huu ni janga la Dunia”, alisema
Saleem.
Mwakilishi
huyo wa Ubalozi wa Pakistani aliishauri Serikali kuendelea kutumia vyombo vya
habari na mitandao ya kijamii katika kutoa elimu ya ugonjwa wa
COVID-19 ili wananchi waendelee kupata elimu ya kutosha ambayo
itawasaidia kujikinga na ugonjwa huo.
Kwa
upande wake mganga mkuu wa Serikali Prof. Muhamad Bakari Kambi aliushukuru
Ubalozi wa Pakistani kwa msaada walioutoa na kusema kuwa utasaidia kwa kiasi
kikubwa katika kukabiliana na ugonjwa huo.
Prof.
Kambi alisema ugonjwa wa COVID -19 ni janga la Dunia, watu wengi
wamepata madhara kutokana ugonjwa huo hivyo basi hakuna msaada mdogo.
"Msaada wowote unaotolewa kwa Serikali utanasaidia kwa kiasi kukubwa
katika kukabiliana na ugonjwa".
Ubalozi
wa Pakistani umetoa msaada wa barakoa za upasuaji 1800, kofia ambazo zinavaliwa
na wahudumu wa afya wakati wanahudumia wagonjwa 1800, kava za viatu
za kuvaliwa wodini 800, barakoa za N95 zipatazo 500, magauni ya kuvaa watoa
huduma za afya 100, glovu 8000 pamoja na miwani ya kujikinga na virusi
vinavyosababisha ugonjwa wa Corona 60. Thamani ya vifaa hivyo ni
zaidi ya milioni 11.
Mwisho
0 on: "SERIKALI YAPONGEZWA KATIKA KUKABILIANA NA UGONJWA WA CORONA"