Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatano, 22 Aprili 2020

WAZAZI TUWAKINGE WATOTO WETU DHIDI YA VIRUSI VYA CORONA

Wakazi wa eneo la Keko Jijini Dar es Salaam wakisikiliza elimu kuhusu mbinu za kujikinga wao na Watoto wao kupata maambukizi ya virusi vya Corona kutoka kwa timu ya uhamasishaji kutoka Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wadau kutoka Shirika lisilo Lakiserikali la Project CLEAR.

Dereva boda boda wa eneo la Kariakoo Jijini Dar es Salaam wakisikiliza elimu kuhusu mbinu za kujikinga kupata maambukizi ya virusi vya Corona.

Mkuu wa Kitengo cha maji na usafi wa mazingira, Wizara ya Afya, Ndg. Anyitike Mwakitalima akikabidhi vitakasa mikono kwa askari wa jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani ili viwasaidie kujilinda dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona wakati wa kutoa huduma kwa wananchi, katika eneo la Kariakoo Jijini Dar es Salaam.

Balozi wa kampeni ya Mikoni safi, Tanzania salama, Msanii Mrisho Mpoto (Mjomba), akikabidhi boksi la vitakasa mikono (sanitizer) Mrakibu msaidizi wa polisi (ASP) Angelica, makao makao makuu ndogo ya jeshi la polisi, Posta Jijini Dar es Salaam.

Afisa kutoka jeshi polisi kitengo chaushrikishaji jamii Stafu Sajenti Valentino Ngowi akiongea na Dereva boda boda na Bajaji, kuhusu elimu ya kujikinga kupata maambukizi ya virusi vya Corona.

Mkurugenzi wa Lemutuz Brand, vyombo vya utoaji habari za kwa njia ya mtandao, Ndg. Lemutuz akinawa mikono yake kwa sabuni na maji safi yanayotiririka ikiwa ni sehemu ya uhamasishaji kwa wananchi juu ya kunawa mikono, kama moja ya njia ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Timu ya uhamasishaji kutoka Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Wadau kutoka Shirika lisilo Lakiserikali la Project CLEAR na kampuni ya Mjomba Gallery ikiendelea na utoaji elimu kwa wafanyabiashara wa Kariakoo Jiji la Dar es Salaam kuhusu kuchukua tahadhari za kujikinga dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona.WAZAZI TUWAKINGE WATOTO WETU DHIDI YA VIRUSI VYA CORONA

Na WAMJW- DSM

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa wito kwa wazazi na walezi nchini kuwalinda Watoto wao dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona kwa kuhakikisha wanajikinga vizuri na kuwakinga watoto wao dhidi ya virusi hivyo,

Wito huo ameutoa, Mkuu wa Kitengo cha maji na usafi wa mazingira, Wizara ya Afya, Ndg. Anyitike Mwakitalima wakati akitoa elimu kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kuhusu kuchukua tahadhari za kujikinga dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona

Ndg. Anyitike Mwakitalima amesema kuwa, Watoto wanaweza kuwa chanzo cha kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya Corona katika jamii na familia, hivyo amesisitiza wazazi na walezi kuhakikisha wanawadhibiti watoto kuzulula mitaani katika kipindi hiki cha mlipuko wa virusi hivyo.

"Serikali kupitia Wizara ya Afya inatoa wito ambao inautoa ni kwamba wazazi na walezi tukumbuke kuwalinda watoto wetu, wakae na watulie majumbani kwa kipindi hiki shule zimefunga, msiwaruhusu waende kuzulula maeneo mbali mbali, kwani wanaweza kupata maambukizi huko wanakoenda kucheza" alisema.

Mbali na hayo, alisisitiza kuwa, wazazi watoe elimu kwa watoto kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona kwa kuhakikisha wananawa mikono kwa sabuni na maji safi yanayotiririka, huku akisisitiza waepuke kushika macho, pua na mdomo ili kuzuia kupata maambukizi hayo.

"Wazazi na walezi tuwakumbushe Watoto kunawa mikono kwa sabuni na maji safi yanayotiririka, tuwakumbushe Watoto kuepuka kushika pua, mdomo na macho kwa mikono kwa kufanya hivyo tutakuwa tumewalinda watoto watoto wetu na tutajilinda sisi wenyewe kupata maambukizi ya virusi vya Corona " alisema

Kwa upande wake, Afisa kutoka jeshi polisi kitengo chaushrikishaji jamii Stafu Sajenti Valentino Ngowi amewaagiza madereva na makondakta wao kuhakikisha kila siku jioni wanapokuwa wamemaliza kazi zao Kutakasa magari yao kwa dawa maalum aina ya jiki, ili kuua virusi vinavyoweza kuwepo na kupelekea maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

Nae Balozi wa kampeni ya Mikoni safi, Tanzania salama, Msanii Mrisho Mpoto (Mjomba), amewakumbusha Watanzania kufuata maelekezo ya Wataalamu wa Afya ikiwemo kuepuka msongamano katika maeneo yote, huku akisisitiza kama hakuna sababu yakutoka nje ni watulie majumbani.

“Nitumie fursa hii kuwakumbusha Watanzania kuendelee kufuata maelekezo ya wataalam wa afya, ikiwemo kuepuka misongamano isiyo na ulazima, na kama huna sababu ya kutoka nyumbani ni vyema ukabaki nyumbani" alisema

Mwisho.

3 on: "WAZAZI TUWAKINGE WATOTO WETU DHIDI YA VIRUSI VYA CORONA"
 1. Hongera wizara kwa hatua hii.
  Ila nilikuwa naomba pia mikoani wapate elimu pia kuhusu janga hili. Maana bado kuna mizaha ipo inaendelea. Ni vizuri wakuu wa mikoa wahakikishe elimu inatolewa pia kwa wananchi waliopo mikoani mwao.

  JibuFuta
 2. Hongera sana waziri na wasaidizi wako, nilitamani wadau wa afya wa kila wilaya wangeandaa semina za watu wachache kuwaelimisha kuhusu corona ili nao wakatoe Elimu nyumba kwa nyumba.

  JibuFuta
 3. Tunaipongeza Serikali kwa hatua inazizichukua.

  JibuFuta