Mratibu wa ushirikiano wa Tanzania na China kwenye eneo la sekta ya afya Dkt. Ligile Vumilia akiongea mbele ya wajumbe wa kikao cha Menejimenti ya wizara ya afya mapema leo. |
Wajumbe wa kikao cha menejimenti ya wizara ya afya na wageni kutoka jimbo la Shadong nchini China wakiwa katika majadiliano ya mkakati wa kuimarisha uhusiano kati ya nchi mbili hizo. |
Katinu Mkuu wa Wizara ya Afya, ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakurugenzi na wajumbe kutoka jimbo la Shadong nchini China. |
Na WAJMW-Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula leo amekutana na kufanya mazungumzo na
wajumbe kutoka jimbo la Shadong la nchini China katika ofisi za Wizara zilizoko
Mtumba nje kidogo ya jiji la Dodoma.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika mbele ya wajumbe wa
kikao cha Menejimenti yalilenga kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na China,
Dkt. Chaula amesema wamekubaliana kushirikiana katika kubadilishana uzoefu na
kuzalisha wataalamu wa afya waliobobea katika sekta mbalimbali.
“Kimsingi tumekubaliana na wajumbe hawa toka jimbo la
Shadong lililopo China kuendelea kushirikiana katika kuboresha sekta ya afya
nchini na kwa kuanza tumesaini makubaliano ya kusomesha Watanzania madaktari
bingwa kwenda kusoma kozi mbalimbali kwa muda mrefu na muda mfupi”. Amesema
Dkt. Chaula.
Dkt. Chaula amesema lengo la makubaliano hayo ni kuhakikisha
Tanzania inapata wataalamu wa afya wabobezi watakaosaidia katika kuboresha
huduma za kibingwa nchini mara baada ya kusoma kozi mbalimbali za kada ya afya
chini China.
Nae Dkt. Ligile Vumilia ambaye ni mratibu wa ushirikiano wa
Tanzania na China kwenye eneo la Sekta afya ambayo chini ya idara ya tiba
amesema jimbo la Shadong limekua likileta wataalamu chini katika sekta ya afya
kuanzia miaka ya 1960 na wamekua wakihudumu katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili, Hospitali za mikoa ya Tabora, Dodoma na Mara.
Dkt. Vumilia amesema timu iliyokuja ni ya viongozi ambayo
itasaidia kuendeleza uhusiano kwa kuleta vifaa kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali
ya JKCI, kuleta madaktari wanaotoka China kwa ajili ya kutoa huduma nchini na
pia kutoa fursa kwa madaktari bingwa 50 nchini kwenda kusoma China na kuongeza
ujuzi zaidi.
Aidha, Dkt. Vumulia amesema ujumbe huo utasaidia kuleta
vifaa tiba ambavyo vitasaidia katika kutibu magonjwa ya moyo nchini, pia ugeni
huo utasaidia kujenga ukumbi mkubwa wa mikutano katika Mji wa Serikali eneo la
Wizara ya Afya utakaoitwa Shadong ambao
utatumika katika masuala mbalimbali ya elimu ya afya (tiba mtandao) ambapo Katibu
Mkuu na uongozi watakua na uwezo wa kuwasiliana na madaktari kutoka Hospitali mbalimbali
za Rufaa za mikoa na Kanda pasipo wao kufunga safari.
MWISHO
0 on: "SERIKALI YA CHINA YAAHIDI KUCHANGIA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI"