Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumapili, 7 Aprili 2019

WAZIRI UMMY AAHIDI NEEMA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (kushoto) akiongea jambo wakati alipofanya ziara ya kukagua jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (General). Kulia ni katibu wa Wizara ya hiyo Dkt. Zainab Chaula.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula wakiangalia kitu katika wodi ya akinamama waliojifungua wakati walipofanya ziara ya ukaguzi wa jengo jipya la mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu (Kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula wakifurahia jambo wakati wanasaini kitabu cha wageni katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakati walipofanya ziara ya kukagua jengo la mama na mtoto.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akimuonesha Waziri Ummy Mwalimu Dirisha katika moja ya Wodi za Jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wakati walipofanya ziara katika Hospitali hiyo leo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipokea hotuba kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Dkt. Ernest Benzi wakati walipofanya ziara ya kukagua jengo la mama na mtoto (Maternity Block). Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula na nyuma  viongozi wengine wa Wizara na Hospitali.

Jengo jipya la Mama na Mtoto (Maternity Block) lililopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Na WAMJW-Dodoma

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameahidi kutoa Tsh. Milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa jengo jipya la wagonjwa wa nje (OPD) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Waziri Ummy ametoa ahadi hiyo leo wakati alipofanya ziara ya kutembelea jengo jipya la mama na mtoto (Maternity Block) katika Hospitali hiyo ili kujionea hali ya utoaji huduma kwa akina mama wajawazito na watoto.

“Ninaahidi kutoa Milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa jengo jipya la OPD ya kisasa yenye uwezo wa kupokea wagonjwa wengi zaidi tofauti na OPD iliyopo sasa”. Amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy ameutaka uongozi wa Hospitali hiyo kurekebisha na kufanya maboresho katika baadhi ya maeneo yaliyoonekana kuwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuyapa majina majengo yote ya Hospitali hiyo ili kuepusha usumbufu kwa wagonjwa pindi wanapotaka kupata huduma katika majengo tofauti.

Aidha, Waziri Ummy ameutaka uongozi wa Hospitali hiyo kujenga ghorofa ambayo itakua maalum kwa ajili ya matibabu ya watoto pekee yenye uwezo wa kulaza watoto wengi sambamba na chumba cha uangalizi maalum kwa watoto waliozaliwa kabla ya muda (Intensive Neonatal Care Unit) na wale wanaohitaji uangalizi maalum (ICU).

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula amesema Wizara itaendelea kushirikiana na uongozi wa Hospitali hiyo katika kutatua changamoto mbalimbali zilizoonekana katika Hospitali hiyo ikiwa ni pamoja kuongeza watumishi wa kada mbalimbali ili kukidhi mahitaji.

“Naomba niwaahidi tutaongeza watumishi wa kada mbalimbali ili kuziba mapungufu yanayoonekana, lengo likiwa ni kuboresha huduma katika Hospitali hii inayotegemewa na watu wengi wa Dodoma na kutoka maeneo ya jirani”. Amesema Dkt. Chaula.

Hata hivyo Dkt. Chaula amewataka watumishi wa Hospitali hiyo kushirikiana ili waweze kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa wanaokwenda hospitalini hapo.

Katika ziara hiyo iliyoenda sambamba na siku ya Afya Duniani imejumuisha viongozi mbalimbali wa Wizara akiwemo Mkurugenzi wa Sera na Mipango Edward Mbaga wameondoka na azimio la kufanya maboresho katika Hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na kujengwa kwa jengo maalum la kupokea wageni mbalimbali wanaokuja Dodoma.

0 on: "WAZIRI UMMY AAHIDI NEEMA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA"