Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Kumbukumbu la Blogu

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumamosi, 13 Aprili 2019

RAIS MAGUFULI AZINDUA MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMARais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua jiwe la msingi ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa ofisi za wizara mbalimbali ambazo zimejengwa katika kata ya Ntumba nje kidogo ya Jiji la Dodoma.

Rais Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan (Kushoto) na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (Kulia) wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la wizara ya Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora kama kiashirio cha uzinduzi wa Mji wa Serikali ambapo Majengo ya Wizara zote yamejengwa huko.

Rais Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan (Kushoto) na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (Kulia) na viongzi wengine waliokaa, wakiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri na Manaibu Waziri (Waliosimama) wakati wa uzinduzi wa Mji Mpya wa Serikali uliopo kata ya Ntumba Jijini Dodoma.

Rais Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan (Kushoto) na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (Kulia) na viongozi wengine waliokaa, wakiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Mji Mpya wa Seriakali Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akiongea na Watumishi wa Wizara hiyo wakati walipotembelea jengo jipya la Wizara lililopo kata ya Ntumba Jijini Dodoma mara baada ya Rais Magufuli kuzindua mji wa Serikali.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Taasisi mbalimbali za Afya, Wakurugenzi wa Vitengo mbalimbali pamoja Watumishi wa Wizara ya Afya wakati walipotembelea Jengo la ofisi za Wizara hiyo.

0 on: "RAIS MAGUFULI AZINDUA MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA"