Na Emmanuel Malegi-Dodoma
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu kwa niaba ya Waziri Mkuu
Mhe. Kassim Majaliwa leo amepokea msaada wa hundi ya kiasi cha Tsh. Milioni 100
kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)uliokabidhiwa na
Kaimu Mkurugenzi Bw. Godfrey Chibulunje akiwa na Meneja Mawasiliano na uhusiano
wa mamlaka hiyo Bw. Titus Kaguo.
Aidha, Waziri Ummy amepokea msaada wa ndoo 480 sawa na Lita
9600 za vitakasa mikono (Hand Sanitizer) zenye thamani ya Tsh. Milioni 11 zilizotolewa
na kampuni ya Mafuta ya Mount Meru ambazo zitatumika katika kudhibiti ugonjwa
wa Corona nchini. Vitakasa mikono hivyo vimekabidhiwa na Meneja Mkuu wa Kampuni
hiyo Bw. Prabhat Yadau.
Katika makabidhiano hayo yaliyofanyika katika ofisi ya
Waziri Mkuu Mlimwa jijini Dodoma, Waziri Ummy kwa niaba ya Waziri Mkuu ameshukuru
kupata misaada hiyo ambayo itasaidia katika kudhibiti ugonjwa wa Corona nchini
na pia amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari licha ya maambukizi ya ugonjwa
huo kupungua nchini.
0 on: "EWURA NA MOUNT MERU ZATOA MSAADA KWA AJILI YA UDHIBITI WA CORONA NCHINI"