Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi (kushoto) akizungumza na wananchi waliofika katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma kupata huduma ambapo amezungumza nao kuendelae kujilinda na ugonjwa wa corona kwa mbinu zinatotolewa na Wizara ya Afya ikiwemo tiba asili ya kujifukiza.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi (kulia) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika wakielekea kwenye kituo kilichotengwa kuhudumia wagonjwa wa corona ambacho hakina mgonjwa yeyote.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi akizunguma na watumishi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa alipotembelea hospitlai hiyo, Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika.
WITO WATOLEWA WANANCHI KUENDELEA KIJIKINGA NA
CORONA ILI PIA KUJIKINGA NA MAGONJWA MENGINE.
Na WAMJW-DOM
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi
ametoa wito kwa wananchi kuendelea kujikinga dhidi ya ugonjwa wa corona na
kudhibiti magonjwa mengineyo ya kuambukiza.
Prof. Makubi ametoa wito huo leo alipofanya
ziara ya kuona hali ya utoaji huduma katika Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo
Jijini Dodoma.
“Katika kudhibiti ugonjwa wa corona wananchi
walipokea kwa mikono miwili mbinu za kuepuka kuambukizwa ugonjwa wa corona
ikiwemo unawaji mikono kwa maji yanayotirika na sabuni, uvaaji wa barakoa,
kuepuka mikusanyiko na misongamano pamoja na mbinu za tiba asilia/tiba mbadala
ili kutibu ugonjwa wa corona”. Amesema Prof. Makubi
Pamoja na kupungua kwa ugonjwa wa corona
nchini, Prof. Makubi amesema kuwa bado Watanzania tunatakiwa kuendelea kuchukua
tahadhari za kinga ili hatimae tuweze kutokomeza kabisa ugonjwa wa corona au
pale ambapo bado utaendelea kuwepo tuweze kuishi nao bila madhara makubwa.
Prof Makubi amesema kuwa Serikali inawapongeza
wananchi kwa kuipokea na kutumia njia zote zilizotelewa kukabiliana na ugonjwa
wa corona pamoja na magonjwa mengine ya kuambukiza na kuwataka wananchi
kuendelea na mbinu walizoelimishwa kujikinga na magonjwa ya kuambukiza.
“Mwamko tulio nao sasa hivi wananchi juu ya
mbinu hizi tusiziache, tukiendelea nazo zitatusaidia kujikinga na magonjwa
mengine” amesisitiza Prof. Makubi.
Hatukuwa na utamaduni wa kunawa mikono mara kwa
mara, lakini tuelewe pia usafi wa mikono unatusaidia pia kupunguza hatari ya
kupata magonjwa mengine yanayotokana na uchafu yakiwemo magonjwa ya kuhara, au
hata kipindupindu.
Prof.
Abel Makubi amesema kuwa kufanya mazoezi ya mwili na
kula lishe bora yanasaidia
pia kujenga afya ya mwili uimara na pia kujikinga na magonjwa yasiyo ya
kuambukiza kama shinikizo la damu, kisukari na moyo.
“Ni vema wanachi
wakaendelea na utamaduni huu huku wakiendelea kupata lishe bora aili kujenga
kinga zao dhidi ya mgonjwa mengine” Amesisitiza Prof.
Makubi
Kuhusu
mbinu ya tibaasili, Prof. Makubi amewapongeza wananchi kwa kuipokea na
kuikubali mbinu hiyo katika kusaidia kutibu ugonjwa wa corona na kutumia fursa
hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzana
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuelekeza bajeti ya tiba asili/mbadala na
tafiti za dawa asilia iweze kuongezwa ili kuwawezesha wataalam wanaotengeneza
dawa hizo zinazosaidia kutibu magonjwa mbalimbali na kupambana na maambukizi ya
virusi vya corona nchini.
Aidha Prof Makubi amewaagiza wataalam wa afya hasa Wakurugenzi, Waganga wa
Mikoa, Wilaya, Maafisa wa afya ngazi za jamii, viongozi wa mashule, vyuo,
michezo, na mamlaka za mitaa kuendelea kutoa elimu ya kupambana ugonjwa wa
corona na kuendelea kuhamasisha mbinu za kuthibiti CORONA ambazo
zikiendelezwa zitapunguza uwezekano wa kuibuka magonjwa mengine hivyo kuokoa
afya za wanachi na fedha nyingi ambazo zingetumika kutibu wagonjwa.
Mwisho.
0 on: "WITO WATOLEWA WANANCHI KUENDELEA KIJIKINGA NA CORONA ILI PIA KUJIKINGA NA MAGONJWA MENGINE."