Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel akiongea na madereva malori mpaka wa Tanzania na Kenya Namanga Jijini Arusha, lengo kuwasikiliza changamoto zao.
Baadhi ya madereva wa malori waliokwama katika mpaka wa Tanzania na Kenya Namanga Jijini Arusha wakimsikiliza Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel.
DKT.
MOLLEL ATETA NA MADEREVA WA MALORI, NAMANGA
Na WAMJW-
Arusha.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel
amefanya ziara katika mpaka wa Tanzania na Kenya Namanga Jijini Arusha na
kuzungumza na madereva wa malori yanayokwenda Kenya ili kusikiliza changamoto
zinazowakumba.
Dkt.
Mollel amefanya ziara hiyo leo, ikiwa ni sehemu ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto
zinazowakumba madereva hao, katika kipindi hiki ambacho Dunia imekumbwa na
maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona.
Dkt.
Mollel amesema kuwa, Serikali imeliona tatizo hilo na kuweka wazi kuwa
itaongeza kasi katika kuhakikisha inapata suluhu ya changamoto wanazokumbana
nazo madereva hao katika eneo la mpaka wa Namanga.
"Nimekuja
kuwaambia poleni, lakini Serikali yetu itaenda kwa kasi ya ajabu kuhakikisha
kwamba hili tatizo lenu katika mpaka huu linatatuliwa " alisema.
Aidha,
Dkt. Mollel amewataka madereva hao kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho,
Serikali inatafuta utatuzi wa changamoto yao, huku akiwapa salamu kutoka kwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli na kusema
anawapenda sana.
Mbali na
hayo Dkt. Mollel alisema kuwa changamoto hii iliyojitokeza katika mpaka wa
Namanga ni suala mtambuka ambalo linahusisha Wizara zaidi ya moja, huku akiweka
wazi kuwa suala hili lina uhusiano wa kibiashara na uchumi baina ya nchi hizo.
Nae,
dereva wa malori yanayokwenda nchini Kenya Bw. Abdullah Hassan amesema kuwa,
kama madereva hawakubaliani na majibu ya vipimo wanavyopewa kutoka Kenya
kutokana na vipimo hivyo kuonesha idadi kubwa ya madereva kuwa na ugonjwa wa
Corona jambo ambalo sio kweli.
"Tunaishi
maisha magumu sana kutokana na hali iliyojitokeza, na kunachosikitisha zaidi,
sisi hatukubaliani na vipimo ambavyo tunapimwa upande wa pili.
Kwa
upande wake, Japhet Jeremiah alisema kuwa, wamekuwa wakiombwa kiasi cha
shilingi 2000 za Kenya ili kuandikiwa kuwa hawana Corona, hali aliyeweka wazi
kuwa ni uonevu kwa madereva kutoka Tanzania.
"Sisi
kero yetu, tumekuwa tukipima Kenya tumeambiwa tuna Corona, na mimi wiki mbili
nilipima nikapewa cheti nina Corona lakini ukweli ni kwamba sina Corona na
sijawai tumia dawa yoyote mpaka sasahivi" alisema
Mwisho.
0 on: "DKT. MOLLEL ATETA NA MADEREVA WA MALORI, NAMANGA"