Na Emmanuel Malegi-Dodoma
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Mhe. Ummy Mwalimu amesema Tanzania kama nchi nyingine za Kiafrika wavutaji wa
tumbaku wako hatarini kuyumba kiuchumi na kupata magonjwa yasiyoambukizwa kama
tahadhari hazitachukuliwa mapema.
Waziri Ummy amesema hayo leo wakati wa uzinduzi
wa ripoti ya utafiti wa matumizi ya tumbaku kwa watu wazima wa mwaka 2018
nchini uliofanyika mapema leo katika Ukumbi wa Takwimu jijini Dodoma.
Waziri Ummy amesema utafiti huo umeonesha kuwa kwa wastani matumizi ya tumbaku kwa mtu mmoja
kwa mwezi inagharimu Shilingi za Kitanzania 28,840/= fedha ambayo ingetosha
kupunguza kiwango cha umaskini wa mahitaji ya msingi kwa mtu mmoja mmoja kwa
mwezi kwa asilimia 58 na umaskini wa kupindukia (mahitaji ya chakula) kwa mtu
mmoja mmoja kwa mwezi kwa asilimia 85.
“Kwa kutumia taarifa za Matokeo ya Viashiria Muhimu vya Utafiti wa Mapato na
Matumizi ya Kaya binafsi kwa Tanzania Bara wa Mwaka 2017-18, fedha za kujikimu
kwa ajili ya mahitaji ya msingi kwa mwezi kwa mtu mmoja ni Shilingi za
Kitanzania 49,320/= na mahitaji ya chakula kwa mwezi kwa mtu mmoja ni Shilingi
za Kitanzania 33,748/=”. Amesema Waziri Ummy.
Kwa mujibu wa
utafiti huo, Matokeo yameonesha kuwa mtu mmoja kati ya 10 (8.7%), wenye umri wa miaka 15 au zaidi
nchini Tanzania wanatumia tumbaku ya aina yeyote na hivyo kuwa na watu milioni
2.6 kati ya watu zaidi ya milioni 55. Wanaume
ni asilimia 14.6 na wanawake ni asilimia 3.2.
Aidha, Waziri Ummy amesema watu 4 kati ya 10 (40.3%) nchini wamewahi kuona
onyo la matumizi ya tumbaku kupitia redio au runinga. Pia matokeo ya utafiti
yameonesha kuwa, watu 9 kati ya 10 (92.3%) wenye umri wa miaka 15 au zaidi
wanaamini uvutaji wa sigara husababisha magonjwa, wakati watu 8 kati ya 10
(84.4%) wanaamini kuvuta hewa ya mtu anaevuta sigara kunaweza kuwasababishia
magonjwa hata kama wao hawavuti sigara.
katika kipindi cha miezi 12 iliyopita.
Taarifa inaonesha kuwa watu 4 kati ya 10 (32.9%) wameathiriwa na moshi
wa tumbaku sehemu za kazi ikiongozwa na sehemu za mabaa na kumbi za starehe kwa
asilimia 77 (watu milioni 3), maeneo ya huduma za biashara za vyakula asilimia
31.1(watu milioni 3.5) na majumbani asilimia 13.8 (watu milioni 4.1).
Waziri Ummy amesema utafiti huo una umuhimu wa
kipekee katika Wizara, kwani matokeo yake yatasaidia katika kutathmini hatua
zilizofikiwa katika kupambana na magonjwa makuu manne yasiyoambukiza ambayo ni Saratani,
magonjwa ya moyo, magonjwa ya mfumo wa hewa na kisukari.
katika kuhakikisha
elimu dhidi ya athari ya tumbaku inaifikia jamii ipasavyo. Waziri Ummy ametoa
maelekezo kwa Watendaji wa Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu
na wadau wengine, kutengeneza au kupitia upya Sheria ya kudhibiti matumizi ya
Tumbaku ili iendane na Mkataba wa Kimataifa wa kudhibiti matumizi ya Tumbaku na
kuendelea kutoa Elimu kwa jamii kuhusu madhara yake; Wizara ya Elimu kuendelea
kuimarisha juhudi za kuwakinga wanafunzi dhidi ya tumbaku na bidhaa zake; Wizara
ya mambo ya ndani kuhakikisha wale wanaokiuka miongozo kama vile kuendelea
kuvuta sigara kwenye maeneo ya wazi wanachukuliwa hatua stahiki; Watengenezaji na wauzaji
wa sigara, kufuata miongozo iliyowekwa na Serikali ikiwemo kutokuweka mabango
au kutangaza na kuhamasisha matumizi ya sigara, kupitia bidhaa kama miamvuli,
T-Shirts, kofia, na kutowauzia watoto wenye umri chini ya miaka 18; jamii kuacha
kutumia tumbaku na bidhaa zake na Taasisi za Utafiti kufanya Tafiti za
kuangalia vifo vitokanavyo na matumizi ya tumbaku ilikuwe na takwimu za nchi na
siyo kutegemea za kutoka nje.
*MWISHO*
0 on: "UVUTAJI WA TUMBAKU UNA ATHARI UCHUMI WA MTU MMOJA MMOJA ANAYETUMIA"