Alhamisi, 11 Juni 2020
WAZIRI UMMY AZINDUA BARAZA JIPYA LA MADAKTARI TANGANYIKA
Na WAJMW-DODOMA
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu jana amezindua Baraza jipya la Madaktari Tanganyika katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dodoma.
Katika uzinduzi huo Waziri Ummy amelipongeza Baraza jipya linaloongozwa na Mwenyekiti Prof. David Ngassapa na wajumbe wake wanane walioteuliwa lakini pia hakusita kulishukuru na kutaja baadhi ya mafanikio ya baraza lililopita ambalo lilikua linaongozwa na Prof. Muhammad Kambi ambaye alikua Mwenyekiti.
“Katika kipindi chao cha uongozi, Baraza limepata mafanikio mengi ikiwemo Sheria za Madaktari, Madaktari wa meno wa wataalamu wa Afya shirikishi ya Mwaka 2017, na kuitengenezea kanuni zake tano ambazo ni ya Watarajali, Usajili wa mitihani, Ada na Tozo, pamoja na Uchunguzi wa mashauri ya mafunzo endelevu”. Amesema Waziri Ummy.
Waziri Ummy amesema mabadiliko hayo yameboresha sana muundo wa Baraza na hivyo usimamizi wa taaaluma ya udaktari na udaktari wa meno umeongeza wigo wa usimamizi wa taaluma kwa kuongeza kada za Afya shirikishi ambazo mwanzo zilikua hazina usimamizi.
Waziri Ummy amesema majukumu ya Baraza hilo ni pamoja na kuwatambua wanataaluma inaowasimamia kwa njia ya kuwasajili na kuwapa leseni zinazowaruhusu kufanya kazi hizo na kuwakagua mara kwa mara ili kujiridhisha kuwa wako hai kitaaluma.
Aidha, Waziri Ummy amesema kwa mujibu wa takwimu zilizopo ofisi ya Msajili wa Baraza la Madaktari inaonyesha kuwa jumla ya madaktari wa kada mbalimbali 13,973 wamesajiliwa nchi nzima, hata hivyo madaktari walipo kwenye ajira ni 5568.
Pamoja na hayo, Waziri Ummy amelitaka Baraza jipya chini Mwenyekiti Prof. David Ngassapa kuhakikisha kuwa: Wananchi wanahudumiwa na wanataaluma kwa namna ambayo ni salama, Kuhakikisha kuwa mahusiano kati ya mgonjwa na Daktari yanakuwa ya kuaminiana, Wanataaluma wanapata mafunzo na elimu ya kujiendeleza (CPD) ili waendane sanjari na maendeleo ya sayansi na teknolojia yanayotokea duniani pamoja na Baraza kuhakikisha lina kumbukumbu na taarifa sahihi za wanataaluma linaowasajili na ambazo zinaweza kupatikana kirahisi ili kuhakikisha jamii inapata taarifa sahihi ya wanataaluma wanaoruhusiwa kutoa huduma.
Mwisho, Waziri Ummy amelitaka Baraza hilo kuwa na wajibu wa kutangaza majina ya wanataaluma wenye usajili halali na unaoendana na wakati.
MWISHO
About Wizara ya Afya
Author Description here.. Nulla sagittis convallis. Curabitur consequat. Quisque metus enim, venenatis fermentum, mollis in, porta et, nibh. Duis vulputate elit in elit. Mauris dictum libero id justo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 on: "WAZIRI UMMY AZINDUA BARAZA JIPYA LA MADAKTARI TANGANYIKA"