Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Video. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Video. Onyesha machapisho yote

Ijumaa, 20 Aprili 2018

HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA AFYA 2018/2019





Katika kipindi cha Mwaka 2017/2018, Wizara ilisimamia shughuli za utoaji wa chanjo kwa   watoto ili kuhakikisha kuwa malengo yaliyowekwa kitaifa na kimataifa yanafikiwa. Takwimu za Januari hadi Desemba 2017 zinaonyesha kuwa asilimia101.2 ya Watoto waliolengwa nchini walipatiwa chanjo zote muhimu ili kuwakinga na magonjwa.  Mnamo mwezi Desemba 2017, Serikali yaTanzania ilipongezwa Shirika la Afya Duniani na wadau wa Kimataifa wa Chanjo kwa kufikia kiwango cha juu chachanjo kwa asilimia 97 ya uchanjaji watoto kwa chanjo ya pentavalent kwa takwimu za mwaka 2016. Lengo la Mkakati wa Dunia kupitia Shirika la Afya
Duniani ni nchi kufikia kiwango cha uchanjaji wa asilimia 90. Mikakati ya Wizara imewezesha nchi yetu kufikia kiwango hicho ambapo inakuwa nchi ya Tatu barani Afrika ikitanguliwa na Zambia yenye kiwango cha asilimia 99 ikifuatiwa na Rwanda yenye asilimia 98

Hotuba nzima, bofya link ya chini hapa.
http://afyablog.moh.go.tz/2018/04/hotuba-ya-waziri-wa-afya-maendeleo-ya.html

Jumatano, 11 Aprili 2018

ALICHOSEMA MAKAMU WA RAIS KATIKA UZINDUZI WA CHANJO YA MLANGO WA KIZAZI

- Hakuna maoni


Katika ufunguzi huo uliofanyika jana jijini Dar es salaam Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan alisema kuwa chanjo hiyo imewalenga wasichana wote wanaotimiza umri wa miaka 14 ili kuanza kujikinga mapema na ugonjwa huo. 

"Ili kupata kinga kamili,  wasichana watahitajika kupata dozi mbili ambapo dozi ya kwanza itatolewa muda wowote binti anapofikisha umri wa miaka 14 na dozi ya pili itatolewa miezi site baada ya kupata dozi ya kwanza"alisema Mhe. Samiah Suluhu.

Ijumaa, 6 Aprili 2018

CHANJO YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI NI SALAMA, WAZIRI UMMY

- Hakuna maoni


Mhe. Ummy Mwalimu (MB) awatoa hofu viongozi wa dini pamoja na wananchi kwa ujumla kwamba chanjo hii haizuii binti kutopata watoto katika maisha yake ya baadae bali ni kinga dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi".  Kinga ni bora kuliko tiba, hivyo ni vyema tukashirikiana kuweza kuwaokoa mabint wetu na vifo".

Chanjo mpya ya kuwakinga wasichana wenye umri wa miaka 14 dhidi ya ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi itaanza kutolewa mara baada ya uzinduzi wa kitaifa tarehe 10 Aprili, 2018 na itahusisha mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar pia itatolewa kwenye vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya Serikali, binafsi na huduma mkoba kwenye shule na sehemu mbalimbali. Chanjo hii itatolewa mara mbili ili kupata kinga kamili(chanjo ya pili itatolewa baada ya miezi sita)

Alhamisi, 5 Aprili 2018

WAWEKEZAJI 38 WAONESHA UTAYARI UJENZI WA VIWANDA VYA DAWA NA VIFAA TIBA,...

- Hakuna maoni


Aliyoyasema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. UMMY MWALIMU katika kikao cha kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba hapa nchini, kilichokutanisha wadau mbalimbali wa Uwekezaji katika Sekta ya Dawa, Vifaa na Vifaa tiba

Alhamisi, 29 Machi 2018

HOSPITALI YA KANDA YA RUFAA MBEYA YAPIGA HATUA KATIKA KUMALIZA TATIZO LA WAGONJ...

- Hakuna maoni


Ameyasema hayo Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo Dkt. Godlove Mbwanji katika ofisi yake jijini Mbeya, 
Dkt. Mbwanji hakusita kuupongeza Uongozi na Wafanyakazi wa Hospitali hiyo kwa kujitoa kwa moyo katika kuwatumikia wananchi, pia aliwashukuru wananchi wa Mbeya hususani madereva wa Boda boda kwa moyo wakujitolea katika kuboresha Sekta ya Afya ikiwemo kutoa michango yakifedha.

Jumanne, 27 Machi 2018

DKT. MAGUFULI ATHIBITISHA UWEPO WA DAWA ZAKUTOSHA

- Hakuna maoni


ILI kufikia katika uchumi wa kati kwakutumia sekta ya viwanda Serikali inatak iw a kujikita katika kuimarisha sekta ya afya kwa watanzania ili kuwa na rasilimali watu wenye afya njema kwa ajili yakuleta mafanikio hayo kupitia viwanda.
Hayo yamesemwa na Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa uzinduzi wa magari 181ya kusambazia dawa uliofanyika leo katika Bohari Kuu ya Dawa ya Taifa (MSD) jijini Dar es salaam.
“Tunatakiwa kuwekeza kwenye uchumi wa Viwanda ili tufikie uchumi wa kati hivyo ni lazima tuwekeze kwenye sekta ya afya kwa kiwango kikubwa ili kuwa na wananchi wenye afya njema tayari kutumikia viwanda vyetu kwa muda wote” alisema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli amesema kuwa Tanzania inatakiwa kujijengea viwanda vya dawa na vifaa tiba hapa nchini ili fedha zinazotumika kununua bidhaa hizo nje ya nchi zirudi mikononi kwa watanzania wenyewe pamoja na kutoa ajira kupitia viwanda hivyo.
Mbali na hayo Rais Magufuli amesema kuwa katika kuimarisha Sekta ya afya Serikali imetenga shilingi Bilioni 269 za kununua dawa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 kutoka bilioni 31 katika bajeti ya fedha mwaka 2016/2017.
Kwa upande wake Waziri wa afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa katika kuimarisha Afya ya mama na Mtoto Serikali imepunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa asilimia 60 kutoka asilimia 20 ya upunguzaji wa vifo hivyo.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa fedha zilizotengwa kwa ajili ya dawa zina mawanyo ikiwemo asilimia 42 zahanati na vituo vya afya ,asilimia 16 zinatumika kwa chanjo za watoto ,asilimia 10.2 zianenda hospitali za wilaya ,asilimia  6.8 zinatumia hospitali za mikoa ,asilimia 3.4 zinaenda hospitali maalum na asilimia 3 zinatumika kwa ajili ya dawa za saratani.