Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatano, 16 Mei 2018

MOI SASA KUFANYA UPASUAJI KWA WAGONJWA 1000 KWA MWEZI ASEMA MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN.

- Hakuna maoni

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wa pili kulia akimkabidhi mguu wa bandia mzazi wa mtoto Daniela kwa ajili ya mwanae Daniela Palangyo (8) mkazi wa Kinyerezi wakati wa kuzindua na kupokea msaada wa chumba cha upasuaji MOI leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile na watatu kulia ni Balozi wa Kuwait Nchini Balozi Jasem Al Najem.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wa kwanza kushoto akikata utepe kuashiria kuzindua chumba cha upasuaji katika Taasisi ya Mifupa Moi wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile na katikati ni Balozi wa Kuwait Nchini Balozi Jasem Al Najem.




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wa pili kulia akipata maelezo juu ya vifaa vya upasuaji wakati wa kuzindua na kupokea msaada wa chumba cha upasuaji MOI leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile na aliyevaa kiremba ni Balozi wa Kuwait Nchini Balozi Jasem Al Najem.


Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikabidhi zawadi kwa baadhi ya wazazi weneye watoto wao katika Taasisi ya Mifupa MOI alipotembelea wagonjwa ha oleo jijini Dar es salaam, katikati ni Balozi wa Kuwait Nchini Balozi Jasem Al Najem.
NA WAMJW-DAR ES SALAAM

TAASISI ya Mifupa nchini MOI sasa itafanya upasuaji wa mifupa kwa wagonjwa wapatao 1000 kwa mwezi kutoka wagonjwa 500 mpaka 700 baada ya kupokea msaada wa chumba cha upasuaji na vifaa vyake kutoka kwa Serikali ya Kuwait .

Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa kuzindua na kupokea msaada wa chumba cha upasuaji na vifaa vyake vyenye thamani ya shilinigi milioni 186 leo katika Taasisi ya mifupa MOI leo jijini Dar es salaam.
“Hii ni faraja kubwa sana kwa Serikali kwani uboreshwaji wa huduma katika hospitali zetu za kibingwa kubwa kama MOI itaweza kuhudumia wagonjwa wengi Zaidi kutoka wagonjwa 700 kwa mwezi mpaka kufikia 1000 kwa mwezi” alisema Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Aidha Makamu wa Rais Samia Suluhu amesema kuwa anaishukuru Serikali ya Kuwait kupitia Balozi wake Jasem Al Najem kwa msaada huo kwani utaisaidia kwa kiasi kikubwa MOI katika kuboresha utoaji huduma hasa katika fani ya upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi hapa nchini.
Kwa uapnde wake Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa  kukamilika kwa vyumba hivi viwili vya upasuaji, kutaiwezesha Taasisi ya MOI kuwa na jumla ya vyumba vya upasuaji 8 kutoka 6 vilivyopo sasa na miongoni mwa vyumba hivi vya upasuaji kimoja kitakuwa maalumu kwa ajili ya  watoto tu.
“MOI imeshatoa matibabu ya upasuaji kwa wagonjwa 1,670 ikiwemo upasuaji mifupa (wagonjwa 1,228), kubadilisha nyonga (wagonjwa 84), kubadilisha goti (wagonjwa 72), upasuaji wa uti wa mgongo (wagonjwa 109), ubongo (wagonjwa 64), na watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi (wagonjwa 113” alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kuimarisha na kuboresha afya za Watanzania jengo hilo pia litakuwa na vitanda 16 vya ICU (Intensive Care Unit) na 16 vya HDU (High Dependency Unit), hivyo kuimarisha huduma za tiba kwa wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu.
Naye Balozi wa Kuwait Nchini Balozi Jasem Al Najem amesema kuwa Nchi ya Kuwait ipo mstari wa mbele katika kuhakikisha Hospitali na Vituo vya afya  nchini Tanzania vinatoa huduma bora za Afya kwa kutumia Taaluma na ujuzi wa kisasa ikiwemo vifaa na vifaa tiba .
“Serikali ya Kuwait itakuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuimarisha afya za wananchi kwa kuendelea kutoa misaada mbalimbali ikiwemo vifaa,vifaa tiba na wataalamu wa afya na kutochoka katika hilo” alisema Balozi Najem.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya MOI Bi. Zakia Mejhi amesema kuwa Taasisi yake imeokoa Bilioni 3 za kufanyia upasuaji kwani kwa sasa huduma hizo za kibingwa zinafanyika nchini kwa Shilingi Bilioni 12 kutoka Bilioni 15 za rufaa ya kwenda kutibiwa nje.

 

Ijumaa, 4 Mei 2018

TANZANIA KUPATA DOLA MILIONI 512 KWA AJILI YA KUKINGA NA KUDHIBITI UKIMWI

- Hakuna maoni



Na.WAMJW - DAR ES SALAAM
Serikali inatarajia kupata dola ya kimarekani milioni 512 kwa ajili ya mapambano dhidi ya UKIMWI kutoka Serikali ya Marekani kupitia fungu la mradi wa dharura wa Rais  wa kupambana na UKIMWI Duniani.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile wakati wa akipokea rasmi taarifa ya kutolewa fedha za UKIMWI kwenye hafla iliyofanyika kwenye hospitali ya Mnazi Mmoja jijini hapa.
Dkt.Ndugulile alisema fedha hizo ambazo serikali itapatiwa zitatumika kwa ajili ya kununulia dawa za kufubaza makali ya Virus vya UKIMWI pia zitagawiwa kwa afua mbalimbali za kupambana na  kuzuia maambukizi ya UKIMWI pamoja na uhamasishaji wa upimaji wa Virus vya UKIMWI nchini.
Aidha ,alisema kiasi hicho cha fedha zinatakiwa kutumika ndani ya mwaka mmoja kwa kwa kujikita kwenye malengo ya Dunia ya  tisini tatu(90,90,90) kwa kuhakikisha kwamba asilimia 90 ya watanzania wote wanaohisiwa kuwa na Virusi vya UKIMWi wanafikiwa,asilimia 90 ya wenye Virusi baada ya kupima wana pata tiba na asilimia 90 wanaopata tiba kuweza kufumbaza Virusi vya UKIMWI.
Alisema kama nchi imekuwa na changamoto kubwa sana  na asilimia 90 ya kwanza ya upimaji kutokana na Takwimu za mwaka jana za hali ya maambukizi nchini zinaonyesha bado kuna changamoto kubwa hususan kwenye makundi ya vijana bado maambukizi yanaongezeka hasa kwa wasichana”vilevile kwa upande wa wanaume ambao ni wagumu kwenda kupima na wengine wanapima ila wanachelewa kuanza dawa na kutofuata misingi ya umezaji dawa na hivyo kufa zaidi”.
“Mkakati ambao tunautafakari na kuja nao ni ule wa mwananchi kuweza kujipima wenyewe kwa kutumia mate(Self-Test) hivyo kila mtu aweze kujijpima mwenyewe kwa kwenda kununua kipimo duka la dawa kama ilivyo kwa wanawake kujipima ujauzito”alisema Dkt.Ndugulile
Hata hivyo Naibu Waziri huyo aliwatoa hofu wananchi kwamba Serikali  haitawapima wanaume kwa nguvu kwenye ma bar bali itatumika utaratibu ule ule katika makundi yao kwa kuwapatia ushauri nasaha na kupima kwa hiari “hatusemi wanaume watapimwa kwa nguvu hapana utaratibu utakua ule ule hivyo wananchi msipate hofu” alisema dkt.Ndugulile
Alitaja mikakati mingine ni kwenda kuwafikia makundi mahususi ambayo inaonekana yana maambukizi makubwa  ikiwemo ya wavuvi pamoja na migodini hivyo alitoa rai kwa watanzania kujitokeza ili kuweza kufikia asilimia 90 kutoka 52 ya upimaji wa Virus vya UKIMWI.
Naye Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Inm alisema nchi yake ipo tayari kufanya kazi na Serikali ya Tanzania kujenga Tanzania yenye afya nzuri.

TAARIFA KWA UMMA

- Hakuna maoni
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA,MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WAZEE NA WATOTO


TANGAZO LA WATUMISHI WALIOPATA UFADHILI KWA AWAMU YA PILI KWA MASOMO YA UZAMILI KWA MWAKA 2017/2018
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, anawatangazia watumishi walioomba ufadhili wa masomo ya Uzamili kwa mwaka wa masomo 2017/2018 kuwa zoezi la uchambuzi wa maombi ya ufadhili kwa awamu ya pili umekamilika. Jumla ya watumishi 17 wamechaguliwa kwa awamu hii ya pili hivyo kukamilisha idadi ya watumishi 90 ambao wamepata ufadhili kwa mwaka wa masomo 2017/2018, ufadhili huu unahusisha kulipiwa gharama za ada kwa kipindi chote cha masomo pamoja na posho ya utafiti.
Watumishi hawa waliochaguliwa wanatakiwa kuandika barua ya kukubali ufadhili huu pamoja na kujaza mkataba wa makubaliano ya ufadhili (Bonding Agreement) na Wizara. Wizara inasisitiza kuwa haitahusika kugharamia mafunzo ya mtumishi yeyote ambaye hayuko kwenye orodha hii au ambaye yuko kwenye orodha hii lakini hatojaza mkataba wa  makubaliano ya ufadhili.
Kila mtumishi aliyepata ufadhili atalazimika kuingia kwenye tovuti ya Wizara ya afya ili kupata nakala ya mkataba ambao atatakiwa kujaza nakala tatu katika sehemu zinazomhusu na sehemu ya “First guarantor” atajaza mwajiri wake au yeyote mwenye mamlaka ya kusaini kwa niaba ya mwajiri wake kisha agonge muhuri wa mwajiri na “guarantor” wa pili anapaswa kuwa mtu yeyote mwenye sifa za kuingia mkataba kwa mujibu sheria za nchi. Mikataba hiyo (nakala tatu) ikikamilika kujazwa itawasilishwa wizarani kwa kuambatishwa na picha 3 (passport size) ili Wizara iweze kukamilisha kusaini mikataba hiyo. Kwa watumishi waliopo Dar es Salaam wawasilishe mikataba hiyo ofisi ndogo ya Wizara iliyopo Dar es Salaam, na wengine wawasilishe Makao Makuu ya Wizara yaliyopo Dodoma
Mwisho wa kuwasilisha mikataba hiyo ni tarehe 25/05/2018. Mkataba wa makubaliano ya Ufadhili (Bonding Agreement) unapatikana kwenye tovuti ya Wizara www.moh.go.tz.

Imetolewa na;

Katibu Mkuu (Afya),
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Maendeleoya Jamii,
Jengo 11,
S.L.P 743.
40478 DODOMA
04/05/2018.

Alhamisi, 3 Mei 2018

MAABARA YA AFYA YA JAMII YA TAIFA KUKAMILIKA JULAI 2018

- Hakuna maoni
Naibu wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katikati akipata maelekezo kuhusu ujenzi wa Maabara ya afya ya jamii ya Taifa  kutoka kwa Mkandarasi Alex Musumi wa kwanza kulia  kutoka kampuni ya Ukandarasi WCEC wakati alipotembelea kuangalia ujenzi huo leo jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile katikati akikagua michoro ya jengo la Maabara ya Taifa  ya Afya ya Jamii wakati alipotembelea ujenzi wa maabara hiyo unaoendelea jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kulia akikagua jengo la Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii wakati aliootembelea kukagua ujenzi huo leo jijini Dar es salaam , kushoto ni Mkurugenzi wa Ugavi na Manunuzi Wizara ya Afya Bw. Castro Simba.

 Ukaguzi wa jengo hilo ukiendelea.





Muonekano wa jengo la Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii liliopo jijini Dar es salaam likiwa bado linaendelea na ujenzi.

Sambamba na hilo Dkt. Ndugulile ametembelea Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua kitabu cha usajili wa dawa wakati alipotembelea Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA leo jijini Dar es salaam, kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bi.  Agness Kijo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia mitambo iliyo katika maabara ya chakula, wakati alipofanya ziara katika mamlaka hiyo jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katikati akipata maelezo kutoka kwa Mchunguzi wa Dawa na vipodozi Gerald Sambu kulia wakati alipitembelea TFDA leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi TFDA Bi. Agness Kijo

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katikati akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA wakati alipotembelea mamlaka hiyo leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bi.  Agness Kijo.



Na WAMJW- DAR ES SALAAM. 

UJENZI wa Maabara ya  Afya ya Jamii ya Taifa inayohusiana na magonjwa ya mlipuko unatarajia kukamilika ifikapo Julai mwaka huu. 

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa ziara yake ya kuangalia hali  ya ujenzi wa maabara hiyo jijini Dar es salaam. 

"Mpaka hivi sasa asilimia 60 ya ujenzi imekamilika hivyo namsisitiza  Mkandarasi kwamba Serikali haitaongeza muda wa ziada mpaka kufikia Julali 9 mwaka huu tuwe tumeshakabidhiwa jengo hili" alisema Dkt. Ndugulile 

Aidha, Dkt. Ndugulile alisema kuwa Maabara hiyo ya Afya ya Jamii ya Taifa ni kwa ajili ya kupima sampuli ya magonjwa ya mlipuko na itakuwa ni maabara kubwa Afrika yenye kiwango cha ubora wa  BS3 ambayo imegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 7. 6. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya ukandarasi ya WCEC Injinia Edwins Shittindi amesema kuwa ujenzi huo ulitakiwa uwe umekamilika Oktoba mwaka jana badala ya Julai 2018.

"Tulitakiwa kukabidhi hiki jengo Oktoba 2017 lakini kutokana na vifaa ya kazi  tulivyoviagiza kuchelewa kuwasili tutajitahidi mpaka kufikia Julai 9 mwaka huu tuwe tumekabidhi jengo" alisema Eng. Shittindi.

Sambamba na hilo Dkt. Ndugulile ametembelea Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA na kuwataka waangalie sana watu wanaotangaza vipodozi vyao kwenye mitandao ya jamii na kuandaa utaratibu husika kuhusu bidhaa hizo. 

"Kila kukicha kuna matangazo mengi sana kwenye mitandao ya jamii yanayohusiana na vipodozi hivyo mnatakiwa kuchukua tahadhari na kufuatilia kwa ukaribu kuhusu ubora wa bidhaa zao" alisema Dkt.  Ndugulile. 

Dkt. Ndugulile amesema kuwa TFDA wanatakiwa kuhakikisha ubora wa dawa ,  chakula pamoja na vipodozi unastahili ili watanzania waweze kutumia bidhaa zenye usalama zaidi. 

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile leo ametembelea maeneo mbalimbali ya TFDA ikiwemo sehemu ya usajili wa Dawa, maabara na kuweza kuongea na Uongozi wa Mamlaka hiyo. 

Jumatano, 2 Mei 2018

MAJI YANAYOTIRIRIKA MITAANI KUTOKA VIWANDANI YAPIMWE KEMIKALI.

- Hakuna maoni
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndegulile akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mafunzo na Rasilimali watu ambae alimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Otilie Gowelle.kulia ni Mwenyekiti wa bodi hiyo Dkt Esther Jason.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndegulile akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi Dkt. Esther Jason mwongozo wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Mafunzo na Rasilimali watu ambae alimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Otilie Gowelle.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndegulile akimkabidhi vitendea kazi Mkemia Mkuu wa Serikali Fidelice Mafumiko wakati wa uzinduzi wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali leo jijini Dar es salaam. 

Mwenyekiti wa Bodi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Esther akiongea akitoa neno mbele ya viongozi wa Serikali na Waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndegulileakisisitiza jambo mbele ya Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mku na viongozi wengine wa Srikali wakati wa uzinduzi wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu.


Picha ya pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndegulile wakati wa uzinduzi wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali leo jijini Dar es salaam. 

Na WAMJW-DAR ES SALAAM. 

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeitaka  Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuchukua hatua ya kupima maji yanayotiririka mitaani kutoka viwandani kubaini kama yana kemikali ambazo zinaathiri wananchi au hazina madhara yoyote. 

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afy, Maendeleo ys Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa uzinduzi wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali leo jijini Dar es salaam. 

"Bodi hii ninayoizindua leo inatakiwa kuhakikisha  majibu ya watu wanaokuja kuleta vipimo vyao yatoke mapema na haraka iwezekanavyo ili kupunguza msongamano wa wateja wenu" alisema Dkt. Ndugulile. 

Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa Mamlaka hiyo inatakiwa kushirikiana na kufanya  mazungumzo na Taasisi ya Chakula na Dawa TFDA na TBS ili kutoingiliana katika majukumu kwani kuna kuna kipengele cha majukumu yao kinafanana katika kusimamia ubora wa chakula. 

Aidha Dkt. Ndugulile ameitaka Mamlaka hiyo kuisimamia kikamilifu sheria ya uchafuzi wa Mazingira ili kuepusha wananchi na magonjwa ya kuambukiza na yasioambukiza. 

Kwa upande wake Mkemia Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Katibu wa Bodi hiyo Dkt. Fidelis Mafumiko amesema kuwa wanaiomba Serikali kutatua changamoto ya upungufu wa mitambo ya kufanyia kazi katika mamlaka hiyo. 

Aidha Dkt. Mafumiko amesema kuwa Bodi hiyo iliyozinduliwa leo ipo tayari kufanya kazi kwa manufaa ya  Watanzania japo mamlka hiyo ina upungufu wa Watumishi kutoka watumishi 400 mpaka kufikia watumishi 220. 

Bodi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imezinduliwa leo ikiwa na Wajumbe saba ambao ni Mwenyrkiti wa bodi hiyo Prof. Esther Hellen, Katibu Dkt. Fidelis Mafumiko,  Dkt. Eliud Eliakimu,  Dkt. Samwel Gwamaka, Dcp. Hussein Laiser, Bi. Irene Leisure na Bw. Pius Mponzi.