Like us on Facebook

Inaendeshwa na Blogger.

Tafuta katika Blogu Hii

Instagram

visitors

display number of visitors

Popular Posts

Pages

Flickr Images

Jumatatu, 6 Agosti 2018

SERIKALI YATARAJIA KUDAHILI WANAFUNZI 380 WA KADA ZA AFYA.

- Hakuna maoni
Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu (MB) akisisitiza jambo mbele ya watumishi wa Serikali na wanafunzi wa Kada ya uuguzi leo wakati wa hafla ya makabidhiano ya Majengo ya chuo cha uuguzi Tanga.

Mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigela akiwasamia wanafunzi wa Kada ya uuguzi wakati alipomkaribisha mgeni rasmi, Waziri wa Áfya Mhe. Ummy Mwalimu katika hafla ya makabidhiano ya Majengo ya chuo cha uuguzi Tanga.

 Mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa chuo cha uuguzi Tanga  Felister Bulali  akitoa maelekezo ya namna ya kumuudumia Mtoto aliyetoka kuzaliwa , mbele ya Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wapili Kushoto),  Wakwanza ni mkuu wa chuo hicho Bi. Leah Makala na watatu ni Mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe Martine Shigela.

Waziri wa Áfya Mhe Ummy Mwalimu akiteta jambo juu ya kifaa cha kujifunzia chenye umbo la Mtoto,  wakati wa hafla ya makabidhiano ya Majengo ya chuo cha uuguzi Tanga. Wakwanza ni mkuu wa chuo hicho Bi Leah Makala.

Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akisakata ngoma na kikundi cha ngoma cha kinamama leo wakati wa hafla ya makabidhiano ya Majengo ya chuo cha uuguzi Tanga

Bweni la ghorofa nne la wanafunzi lenye uwezo wakulaza wanafunzi 380 kwa wakati mmoja likiwa ni baadhi ya majengo yaliyogharimu kiasi cha shilingi Bilion 3.5.

Picha ya pamoja ikiongonzwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Martine Shigela wakiwa na baadhi ya watumishi wa Serikali wakati wa Hafla ya makabidhiano ya Majengo ya chuo cha uuguzi Tanga.


SERIKALI YATARAJIA KUDAHILI WANAFUNZI 380 WA KADA ZA AFYA KATIKA CHUO CHA UUGUZI TANGA.

Na WAMJW - TANGA

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, inatarajia kufanya udahili wa wanafunzi kwa asilimia 100 kutoka wanafunzi Mia moja na Hamsini (150) hadi Mia tatu themanini wa kada za Afya nchini katika chuo cha Uuguzi Bombo Tanga.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) wakati wa hafla ya makabidhiano ya majengo ya chuo cha Uuguzi Tanga, yaliyojengwa kupitia ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kupambana na UKIMWI, KIFUA KIKUU (TB) na MALARIA (Global fund).

Waziri ummy aliendelea kusema kuwa  majengo yaliyokabidhiwa ni juhudi za Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo katika kuhakikisha wanazalisha wataalamu wa kada za Afya, hususani Wauguzi na Wakunga jambo litalowawezesha kuwa Wataalamu bora.

“Udahili wa wanafunzi umeongezeka kutoka 190 hadi 260, Huwa tunapata shida sana, wanafunzi wengi wanafaulu na tunakuwa hatuna nafasi ya wapi  pakuwapeleka, kwahiyo tunawashukuru Global fund , tunaweza kudahili hadi wanafunzi 368” Alisema Waziri Ummy Mwalimu.

Aidha, amemwagiza Mkurugenzi wa Mafunzo na Rasilimali watu  kutoka Wizara ya Afya kushirikiana na NACTE  kuwachukua wanafunzi wote waliosoma na kufaulu vizuri masomo nya Sayansi na wenye vigezo na wenye vigezo katika kada ya Afya.

Waziri Ummy aliongeza kuwa, kutokana na jitihada hizo kumekuwepo na ongezeko la wahitimu ngazi ya astashahada na Stashahada kwa mafunzo kutoka wahitimu 4473 mwaka 2012/2013 hadi 7561 kwa mwaka 2016/2017 , ongezeko hili ni sawa na Asilimia 69.

Wakati huo huo Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Otilia Gowelle amesema kwa mwaka huu wa fedha , Wizara imetenga shilingi Bilion 8 kwaajili ya ukarabati wa majengo chakavu katika chuo hicho.

Aliendelea kuwa Wakufunzi 143 wamepangiwa kufanya kazi katika vyuo vya Afya nchini, vikiwemo vyuo vya Wauguzi na Wakunga ambao ndio msingi wa kupunguza athari ya uzazi pamoja na vifo vya wakina mama wajawazito wakati wa kujifungua.

Nae Mwakilishi wa Global Fund Dkt. Hiltruda Temba amesema kuwa, Global fund  imeboresha miundombinu yakufundishia katika vyuo 14 na kuwezesha kufadhili zaidi ya wanafunzi 1500 wa kada za Uuguzi na Ukunga wa Technolojia dawa, Technolojia maabara na Tabibu katika kipindi cha Mwaka 2015/2016 hadi 2017/2018, pamoja na kutenga shilingi Billion 1.1 kwaajili yakuboresha mifumo ya Afya.

MWISHO.

Alhamisi, 2 Agosti 2018

MAAGIZO 12 YA DKT. NDUGULILE WAKATI WA ZIARA YAKE YA MIKOA 6 YA KANDA YA ZIWA

- Hakuna maoni

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza juu ya kuitambua Dawa ya Serikali iliyo na Nembo ya MSD GOT wakati akiwa katika ziara yake ya mikoa 6 ya kanda ya ziwa.

Msafara wa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile  akiwa katika ziara yake ya kukagua hali ya utoaji wa huduma za Afya katika mikoa 6 ya kanda ya ziwa.

MAAGIZO 12 YA DKT. NDUGULILE WAKATI WA ZIARA YAKE YA MIKOA 6 YA KANDA YA ZIWA

#Kusimamishwa kazi Mganga mkuu wa mji wa Bunda Dkt. Nikodemas Masosota 

#kusimamisha ujenzi wa jengo la upasuaji katika kituo chá Áfya chá Katoro Geita kutokana na kukosa misingi ya kitaalamu ya ujenzi

# Kupewa Ripoti ya ujenzi wa jengo la chuo chá Waganga wasaidizi Musoma kutokana na ubadhirifu wa pesa aliouona. 

# Waganga Wafawidhi wa hospitali kuhakikisha wanaagiza dawa  MSD na si mahala pengine. 

#Kamati za ulinzi za mikoa kulinda dawa za Serikali (Dawa zote za Serikali zina nembo ya MSD GOT) 

# Waganga wakuu wa mikoa kusimamia kikamilifu ujenzi wa hospitali mpya za Wilaya na Mikoa ili kuharakisha huduma za afya kwa wananchi.

# Watoa huduma za afya wote kuhakikisha wanaandika muda halisi wakati mgonjwa anapopokelewa hadi anatibiwa. Mfano wa muda ni saa 12: 06 jioni, saa 01: 01 asubuhi na siyo mazoea ya kuandika saa 12PM, saa 11AM 

# Wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya Afya na ule  wa afya ya jamii (CHF iliyoboreshwa) ili kuzishinda gharama za matibabu pindi wanapopata ugonjwa.

# Kuwekwa mikakati thabiti ili kukabiliana na tatizo la Lishe duni hususan kwa Watoto walio chini ya Miaka 5. 

#Akina mama wajawazito kuhudhuria kliniki walau mara nne ndani ya kipindi chá ujauzito na kuhakikisha wanajifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Áfya

#Wananchi kujitokeza kuwapa watoto wao chanjo, hususan chanjo mpya  Saratani ya mlango wa kizazi (HPV) kwa wasichana wenye umri wa miaka 9 - 14.
 
#Amepiga marufuku kwa vituo vyote vya kutolea huduma za Afya nchini zenye Runinga kuonesha muziki katika maeneo yote ya kutolea huduma bali kuweka jumbe zinazohusu Elimu ya Afya kwa umma.

WAZIRI UMMY AWAAGIZA WAGANGA WAKUU WA MIKOA KUTIMIZA WAJIBU WAO KATIKA KUPUNGUZA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI.

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na Wadau wa masuala ya Afya katika kikao cha tathimini  yakuokoa maisha ya mama na mtoto iliyofanywa mapema leo jijini Dar es salaam na shirika la Thamini Uhai.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Mstaafu Emmanuel Maganga akisisitiza jambo wakati wa kikao cha tathimini yakuokoa maisha ya mama na mtoto iliyofanywa mapema leo jijini Dar es salaam na shirika la Thamini Uhai.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya Dkt. Leonard Subi wakati wa kikao cha tathimini yakuokoa maisha ya mama na mtoto iliyofanywa mapema leo jijini Dar es salaam na shirika la Thamini Uhai.

Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu baada ya kikao cha tathimini  yakuokoa maisha ya mama na mtoto iliyofanywa mapema leo jijini Dar es salaam na shirika la Thamini Uhai.

 
WAZIRI UMMY AWAAGIZA WAGANGA WAKUU WA MIKOA KUTIMIZA WAJIBU WAO KATIKA KUPUNGUZA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI.

Na WAMJW-DSM

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa yote nchini kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kikamilifu katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

Amesema hayo mapema leo jijini Dar es salaam katika kikao cha tathmini ya miaka kumi (10) ya kuokoa maisha ya mama na mtoto katika maeneo ambayo ni magumu kufikika, iliyofanywa na Shirika la Thamini Uhai katika Mkoa wa Kigoma.

“Nawataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kutimiza wajibu wao katika kuondokana na tatizo la  vifo vitokanavyo na uzazi, kwa kuhakikisha vipaumbele vyao viwe na lengo moja kwa moja la kupunguza vifo vya watoto wachanga na mama wajawazito” alisema Mhe. Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy alisema kuwa kama kila mtu atatimiza wajibu wake, inawezekana kabisa ifikapo 2020 vifo vitokanavyo na uzazi vikapungua kwa zaidi ya Asilimia 50%, hivyo kuwaagiza Waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha vifaa muhimu vya huduma za uzazi vinakuwepo ili kumsaidia mama mjamzito .

Aidha,Waziri Ummy amewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa kufanyia uchunguzi juu ya Vifo vyote vya akina mama wajawazito  vinavyotokea katika vituo  vya kutolea huduma za Afya jambo litaloweza saidia kubaini tatizo lilipo.

“Tumetoa maelekezo  kwa Waganga Wakuu wa Mikoa, kuhakikisha vifo vyote vya akina mama wajawazito vinavyotokea katika vituo vya kutolea huduma na katika jamii, vitolewe taarifa” alisema Mhe. Ummy Mwalimu.

Sambamba na hayo Waziri Ummy alisema kuwa Serikali katika kuhakikisha inapunguza vifo  vya uzazi  kwa kuboresha vituo vya Afya ili kuviwezesha kutoa huduma za wa Dharura ikiwemo upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni,

Aliendelea kusema kuwa Wakati Serikali ya Awamu ya Tano inaingia madarakani kati ya vituo vya Afya vya Serikali takribani 473, ni vituo vya Afya 117 sawa na Asilimia 21% vilikuwa na uwezo wa kutoa Huduma za upasuaji wa Dharura, hivyo kuwashukuru Wadau kwa kushirikiana na Serikali kuboresha vituo vya Afya 208.

Hata hivyo, Waziri Ummy alisema kuwa katika kuimarisha Afya ya Mama, Uzazi na Mtoto, Serikali imeweka malengo kuwa  ifikapo mwaka  2020 angalau Asilimia 50% ya Vituo vya Afya nchini viweze kutoa huduma hizi kwa ubora unaotakiwa.

“Tunataka itapofika mwaka 2020, tunataka angalau Asilimia 50 ya Vituo vya Afya nchini viweze kutoa huduma hizi, hivyo nikiwa kama msimamizi wa Sera za Afya mpango wangu wa sasa ni kutaka kuhakikisha Ubora wa huduma hizi” alisema Mhe. Ummy Mwalimu

Nae Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Emmanuel Maganga  alisema kuwa Mkoa wa Kigoma umepiga hatua kubwa katika kusogeza huduma za dharura kwa wananchi na kufikia Asilimia 53 ya vituo vya Afya vyote vilivyopo huku wakitarajia kufikia Asilimia 83 ifikapo Desemba mwaka huu baada ya uboreshaji wa vituo vya Afya vingine 10 unaoendelea sasa.

 “Hadi sasa idadi ya vituo vya afya vinavyotoa huduma za Dharura za upasuaji ni Asilimia 53 ya vituo vya Afya vyote vilivyopo huku matarajio ni kufikia asilimia 83 ifikapo Desemba mwaka huu (2018) baada ya uboreshaji wa vituo vya Afya vingine 10 unaoendelea sasa” alisema Mhe. Maganga.

Aliendelea kusema kuwa Idadi ya akina mama wanaojifungulia katika vituo vya kutolea Huduma za Afya imeendelea  kuongezeka kwa kasi sana , mwaka 2015 wakina mama waliojifungua katika vituo vya kutolea huduma za Afya ilikuwa Asilimia 58 ya matarajio, Mwaka 2016 ilikuwa Asilimia 65 na Mwaka 2017 ni Asilimia 78, huku Idadi ya wanaohudhuria kliniki iliongezeka na kufikia Asilimia 113 ya matarajio.

Alhamisi, 26 Julai 2018

TANZANIA YAPONGEZWA NA CDC UFUATILIAJI, UTOAJI TAARIFA ZA MAGONJWA KIMAT...

- Hakuna maoni

TANZANIA YAPONGEZWA NA CDC UFUATILIAJI, UTOAJI TAARIFA ZA MAGONJWA KIMATAIFA

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akiongea na wadau wa Kituo cha Kimataifa cha kudhibiti magonjwa (CDC) kuhusu hali ya utekelezaji katika kufuatilia, kutoa taarifa na kudhibiti magonjwa nchini.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto   akimsikiliza kwa makini na Mkurugenzi Mkuu wa  Kituo cha Kimataifa cha kudhibiti magonjwa (CDC) Dkt. Robert Redfild kuhusu hali ya utekelezaji katika kufuatilia, kutoa taarifa na kudhibiti magonjwa nchini , katikati ni Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Balozi Inmi Petterson.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati chini akifuatilia takwimu zinazotolewa na mfumo wa ufatiliaji wa magonjwa nchini pamoja  na wadau wa Kituo cha Kimataifa cha kudhibiti magonjwa (CDC) wakati wa kikao  kuhusu hali ya utekelezaji katika kufuatilia, kutoa taarifa na kudhibiti magonjwa nchini.

Mtaalamu wa kitengo cha mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa nchini Dkt. Ally Nyangi akitoa maelezo kwa Wadau wa Kituo cha kimataifa cha kudhibiti magonjwa (CDC) hawapo pichani kuhusu jinsi mfumo huo unayofanya kazi nchini.

NA WAMJW- DAR ES SALAAM


TANZANIA imepata pongezi kutoka kwa Kituo cha Kimataifa cha kufuatilia , kutathimini , kutoa taarifa na kuchukua hatua (CDC) kwa kufanya vizuri katika utekelezaji huo hasa katika magonjwa ya mlipuko.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu  wakati wa kikao cha kuangalia hali ya utendaji katika sekta ya Afya nchini.

"Wenzetu wa CDC kutoka  Marekani wanatusaidia kujenga uwezo wa kufuatilia , kutoa taarifa na kuchukua hatua juu ya magonjwa ya mlipuko kama vile Ebora na Kipindupindu na wameridhika kwa utendaji wetu hapa nchini" alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa Tanzania imeimarika katika kufanya uchunguzi , kutathimini ,  kutoa taarifa na kuchukua hatua juu ya magonjwa mbalimbali.

Mbali na hayo Waziri Ummy amesema  kuwa magonjwa hayana mipaka hivyo ni lazima kuwa waangalifu na  kuchukua hatua mda wote kwa kujenga mifumo imara ya ufuatiliaji.

Kwa upande wake  Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Bi. Inmi Petterson amesema kuwa wamefurahishwa na kazi ya wataalamu wa afya waliowekwa hapa nchini katika kupambana na magonjwa na kuahidi kuongeza nguvu kubwa ikiwemo vitendea kazi.

Aidha Balozi Inmi amesesema kuwa Serikali ya Tanzania inatakiwa kushirikiana na wananchi wa Tanzania katika kupata taarifa sahihi za magonjwa na kujenga nchi yenye wananchi wenye afya bora.


Ijumaa, 20 Julai 2018

DKT. NDUGULILE AHAIDI KUZIWAJIBISHA MAMLAKA HUSIKA ENDAPO KITUO CHA AFYA KITAFUNGIWA.

- Hakuna maoni
Naibu Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akikagua cheti chá mmoja kati ya wagonjwa waliofika kupata huduma za Afya katika hospitali ya Mkoa wa Mwanza ya Sokotoure wakati akiendelea na Ziara yake Mkoani hapo.

Naibu Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile (katikati) akikagua chumba chá Dawa katika hospitali ya kanda ya Bugando pindi alipofanya ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya katika Mkoa wa Mwanza.

Naibu Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akikagua incubator katika Zahanati ya Nyamizeze wakati alipofanya ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya katika Mkoa wa Mwanza.

Mwakilishi kutoka Zahanati ya Ihayabuyaga iliyo katika Wilaya ya Magu Mkoa wa Mwanza akipokea zawadi ya cheti kutoka kwa Naibu Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (MB) baada ya kushinda nafasi ya tatu katika kutoa huduma bora za Afya.

DKT. NDUGULILE AHAIDI KUZIWAJIBISHA MAMLAKA HUSIKA ENDAPO KITUO CHA AFYA KITAFUNGIWA. 

Na WAMJW-Mwanza

NAIBU Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile amesema kuwa hatosita kuziwajibisha mamlaka husika endapo kituo chá kutolea Huduma za Afya kitafungwa kutokana na uzembe wa aina yoyote. 

Amesema hayo wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua hali ya utoaji wa huduma za Afya na kutoa vyeti na ngao kwa Halmashauri zilizofanya vizuri katika utoaji wa huduma za afya leo jijini Mwanza.

"Na Bahati nzuri tunapopita tunawapa na maelekezo wa nini chakufanya, tukishakamilisha hili zoezi letu lá kuweka mifumo ya usajili , ithibati, na utoaji wa leseni tutaanza kufungua visivyokidhi vigezo, Sasa tutapofungia kituo chá Afya Mamlaka husika,  iwe ni Rass, Mganga mkuu wa mkoa au wa Wilaya, Mkurugenzi utawajibika, Vingine ni uzembe wa baadhi ya mamlaka kutosimamia vizuri majukumu yake"Alisema Dkt Ndugulile. 

Aliendelea kusema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeendelea kuweka mikakati thabiti katika kuboresha hali ya utoaji huduma za Afya nchini ili wananchi wanufaike zaidi na hali hiyo. 

"Tunaongeza rasilimali watu, tumetangaza ajira mpya 8000 katika sekta ya Áfya,  ambapo na ninyi mtapata,  pia Vituo vyote tutavisajili, kiwe cha umma Au chá binafsi, kitu chá pili tutaweka ithibati kama usipofikisha kigezo katika ngazi husika tutakushusha kigezo unaenda kuanza hatua upya" Alisema Dkt Ndugulile

Aidha Dkt.  Ndugulile alimtaka Mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza Dkt. Thomas Rutachunzibwa kuyasimamia vizuri ili kuhakikisha huduma za afya zinatolewa kwa Ubora unaostahili kwa wananchi .

Nae Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza Dkt. Thomas Rutachunzibwa alisema kuwa Mkoa unatarajia kuanza uboreshaji wa miundombinu ya huduma za afya hususani eneo lá uzazi na Mtoto kupitia mradi wa "Improving access to maternal and Newborn health (IMPACT)  umaotekelezwa na Aga Khan Development Network  (AKDN)  chini ya Ufadhili wa Serikali ya Canadá pamoja na Agriteam kupitia mradi wa Mama na Mtoto ambapo zaidi ya Bilioni 2.8 zinatarajiwa kutolewa na kutumika katika vituo 30

Dkt. Thomas Rutachunzibwa aliendelea kusema kuwa mkoa wa Mwanza Unaendelea kuimarishwa ambapo madirisha maalum 35 yameanzishwa katika hospitali zote 7 za Serikali, vituo vya Áfya 11 na Zahanati 17 ili kuhakikisha wazee wanapata huduma kwa haraka na Ubora unaotakiwa, jumla ya wazee 43,046 wamepatiwa vitambulisho na mabaraza ya wazee 172 yameundwa 

SERIKALI YAIPATIA MKOA WA MARA BILION 5.9 KATIKA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA YA MAMA NA MTOTO.

- Hakuna maoni
Naibu Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akitoa maelekezo kwa mhandisi wa Majengo wakati alipofanya ziara ya kutembelea ujenzi wa hospitali ya Mkoa wa Mara.

Naibu Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akisikiliza kero kutoka kwa mgonjwa aliyefika kupata huduma za afya katika kituo chá Afya Nyasho Mkoani Mara.

Naibu Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akisikiliza maoni ya mama alipofanya ziara katika wodi ya kujifungulia katika kituo chá Afya chá Nyasho Mkoani Mara.

Naibu Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akimjulia hali Mtoto aliyefika na mama yake katika kituo chá Áfya chá Nyasho

Naibu Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akimsalimia moja kati ya wazee aliyefika kupata huduma za afya katika kituo chá Áfya chá Nyasho Mkoani Mara huku akimsisitiza kuwa matibabu ni bure kwa wazee wote wasio na uwezo wakuchangia.

Dkt. Faustine Ndugulile (wakatikati) akiendelea na ziara yake ya kutembelea ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Serengeti.


SERIKALI YAIPATIA MKOA WA MARA BILION 5.9 KATIKA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA YA MAMA NA MTOTO.

Na WAMJW-MARA

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto imeupatia Mkoa wa Mara kiasi cha shilingi Bilion 5.9 ikiwaq ni moja ya jitihada za kuboresha hali ya utoaji huduma za Afya kwa wananchi katika mkoa huo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile mapema leo wakati akiwa katika ziara yake ya Kukagua hali ya utoaji huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara.

“Mkoa wa Mara umepokea Bilion 5.9 kwaajili ya kuboresha vituo vya kutolea huduma za Afya 13, ikiwa ni jitihada za Serikali katika kuboresha hali nya utoaji huduma kwa wananchi wake “ alisema Dkt Ndugulile.

Pia Dkt. Ndugulile aliagiza kamati ya ulinzi ya Wilaya ya Tarime ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya Mhe. Vicent Naano kusimamia vizuri manunuzi ya Dawa, huku akiagizi Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Mwanisi kuhakikisha  dawa zote zinunuliwe kutoka Bohari ya Dawa (MSD).

“Hutaratibu wa kuagiza Dawa kwa  mawakala sitaki kuusikia, MSD tuna dawa karibia zote za msingi,  utaratibu wa mawakala tuliuweka kama mbadala endapo MSD watakosa aina Fulani ya dawa” Alisema Dkt. Ndugulile.

Aidha, Dkt. Ndugulile alisema kuwa  mimba na ndoa za utotoni bado ni tatizo kubwa ambapo mkoa wa Mara ni wa tano kitaifa kwa kuwa na asilimia 37.

“Serikali imeandaa Mpango wa kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa mwaka 2017/18-2021/22 na moja kati ya msisitizo katika mpango huu ni kutokomeza ukatili wa kijinsia shuleni” alisisitiza Dkt. Ndugulile

Aidha Dkt. Ndugulile amekemea mahusiano ya kingono yaliyopo baina ya walimu na wanafunzi na kuwataka wanafunzi kuacha kufanyiana vitendo vya ukatili na kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt. Mwanisi alisema kuwa Idara ya Afya ina upungufu mkubwa wa watumishi mkoani hapo ambao ni 3477 sawa na Asilimia 60.9 ikilinganishwa na watumishi 2237 sawa na Asilimia 39.1 waliopo sasa kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya hadi kufikia mwezi Juni 2018.

Dkt. Mwanisi aliendelea kusema kuwa hali ya maambukizi ya VVU yamepungua kutoka Asilimia 4.5 mwaka 2011 hadi Asilimia 3.6 mwaka 2016/2017 kulingana na utafiti wa kitaifa uliofanyika mwaka  2011-2012 na 2016-2017 huku akisema kuwa wanaendelea kufanya juhudi mbali mbali za kupambana na UKIMWI ili kuhakikisha maambukiz mapya yanaendelea kupungua.

Kwa upande mwingine Mganga Mkuu wa Mkoa alisema hali ya chanjo hadi kufikia Disemba 2017 kwa watoto chini ya mwaka mmoja waliomaliza chanjo zote kimkoa ilikuwa Asilimia 143 ambayo ipo juu ya lengo la kitaifa ambalo ni Asilimia 90.

DKT. NDUGULILE AUGIZA UONGOZI WA MKOA WA MWANZA KUHAKIKISHA 80% YA VITUO VYA AFYA HAVISHUKI CHINI YA NYOTA 3.

- Hakuna maoni
 Naibu Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akikagua list ya vituo vilivyofanya vizuri kupitia utaratibu wa ugawaji wa nyota katika vituo hivyo  wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya katika Mkoa wa Mwanza.

 Naibu Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile  akikagua Fiji ya kuhifadhia damu salama pindi alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya katika Mkoa wa Mwanza, kulia kwake ni mtaalamu wa maabara katika Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe.

Naibu Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile  akiongea na wagonjwa waliofika katika Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe pindi alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya katika Mkoa wa Mwanza.


DKT. NDUGULILE AUGIZA UONGOZI WA MKOA WA MWANZA KUHAKIKISHA 80% YA VITUO VYA AFYA HAVISHUKI CHINI YA NYOTA 3.
Na WAMJW – UKEREWE, MWANZA
Serikali kupitia Wizara ya Afya imeuagiza uongozi wa Mkoa wa Mwanza kuhakikisha kwamba vituo vyote vya Afya vya Serikali na vya binafsi hazishuki chini ya nyota 3, hii ikiwa moja ya jitihada za kuboresha hali ya utoaji wa huduma Afya nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua hali ya utaji huduma leo katika Wilaya ya Ukerewe Mkoa wa Mwanza.
“Tuhakikishe kwamba Asilimia 80 ya vituo vyetu vyote vya kutolea huduma za Afya vyote kuwa na nyota 3 hicho kiwe ni kiwango cha chini sana,” Alisema Dkt. Faustine Ndugulile.
Dkt. Ndugulile aliendelea kusisitiza kwa watoa huduma za Afya juu ya nidhamu na matumizi ya lugha nzuri pindi wanapokuwa wanawahudumia wagonjwa ili kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi  yasiyo na lazima,
Aidha, Dkt. Ndugulile alisema kwamba Serikali imeweka utaratibu wa kuzitambua dawa zake kwa  kuziwekea rebo ya MSD GOT katika dawa zote inazizitoa na kusisitiza kwamba dawa hizo zinastahili kupatikana katika  vituo vya Afya vya Serikali au kwa mgonjwa tu.
“Sisi kama Serikali tumeanza kuweka utaratibu wa kuziwekea rebo dawa zote za Serikali lebo ya MSD GOT, tumeziweka kwenye boksi na kwenye dawa , anaepaswa kuwa nazo ni hospitali zetu na mgonjwa tu, mtu yoyote wa katikati akiwa na hizo dawa basi huyo ametuibia, msimfumbie macho” Alisema Dkt Ndugulile.
Pia, Dkt Ndugulile ameahidi kuwapelekea huduma za dharura katika Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe jambo linalopelekea kupoteza maisha kwa wahitaji wa huduma hizo kutokana hali ya ugumu wa usafiri kutoka kisiwani Ukerewe mpaka kufika katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza SoukeToure
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Ukerewe Mhe. Joseph Mkundi  amefarijika juu ya ujio wa Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndugulile jambo lililompa fursa ya kuona mazingira halisi na kuziona changamoto ambazo wananchi kutoka Ukerewe wanakumbana nazo.
Kisha Mhe. Joseph Mkundi alimuomba Dkt. Faustine Ndugulile (MB) kuwasaidia  kuboresha huduma za hospitali hiyo ya Wilaya ya Ukerewe kwa kuwajengea chumba cha upasuaji , chumba cha wagonjwa mahututi na boti kwaajili ya kubebea wagonjwa ili kuwavusha kwenda hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza .

“Mambo ambayo nimekuwa nikiyapigania ni juu ya kuboresha hospitali yetu ya Wilaya ili iweze kutoa huduma kamilifu, kwa maana kwa mazingira yetu tunaichukulia kuwa ndio Hospitali ya Rufaa, ikitokea mgonjwa kakosa usafiri inakuwa ni vigumu sana kuweza kusaidia hali yake,” alisema Mhe. Mkundi.


ZIARA YA WAZIRI UMMY KUJUA HALI YA UTOAJI HUDUMA ZA AFYA URAMBO TABORA

- Hakuna maoni
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa pili kulia akikata utepe kuashiria kuweka jiwe la msingi kwenye jengo la wodi ya wazazi lilitokana na mpango wa malipo kwa ufanisi katika Zahanati ya Itebulanda wilayani Urambo Mkoani Tabora wakati wa ziara yake mkoani humo,wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Urambo Bi. Magreth Sitta.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikakati akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi kitabu cha mpango wa malipo kwa ufanisi katika Zahanati ya Vumilia Wilayani Urambo Mkoa wa Tabora wakati wa ziara yake mkoani humo

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikakati akionesha kitabu cha mpango wa malipo kwa ufanisi pamoja na watumishi wengine wa sekta ya afya  katika vituo vya fya mara baada ya uzinduzi huo uliofanyika  katika Zahanati ya Vumilia Wilayani Urambo Mkoa wa Tabora wakati wa ziara yake mkoani humo wa tatu kushoto ni mkuu wa Wilaya ya Urambo Bi. Angelina Kwinga,.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Urambo Bi. Angelina Kwinga kushoto kitabu cha muongozo wa mpango wa malipo kwa ufanisi  mara baada ya uzinduzi huo uliofanyika  katika Zahanati ya Vumilia Wilayani Urambo Mkoa wa Tabora wakati wa ziara yake mkoani humo.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kulia akifunua pazia kuashiria  kuashiria kuweka jiwe la msingi kwenye jengo la upasuaji katika Zahanati ya Uyogo wilayani Urambo Mkoani Tabora wakati wa ziara yake mkoani humo,kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Urambo Bi. Magreth Sitta.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitembelea maeneo ya Zahanati ya Uyogo wilayani Urambo Mkoani Tabora wakati wa ziara yake mkoani humo.

PICHA NA WAMJW-TABORA