Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akikagua list ya vituo vilivyofanya vizuri
kupitia utaratibu wa ugawaji wa nyota katika vituo hivyo wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya
utoaji huduma za afya katika Mkoa wa Mwanza.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akikagua
Fiji ya kuhifadhia damu salama pindi alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji
huduma za afya katika Mkoa wa Mwanza, kulia kwake ni mtaalamu wa maabara katika
Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akiongea
na wagonjwa waliofika katika Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe pindi alipofanya ziara
ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya katika Mkoa wa Mwanza.
DKT. NDUGULILE AUGIZA UONGOZI
WA MKOA WA MWANZA KUHAKIKISHA 80% YA VITUO VYA AFYA HAVISHUKI CHINI YA NYOTA 3.
Na WAMJW – UKEREWE, MWANZA
Serikali kupitia Wizara ya
Afya imeuagiza uongozi wa Mkoa wa Mwanza kuhakikisha kwamba vituo vyote vya
Afya vya Serikali na vya binafsi hazishuki chini ya nyota 3, hii ikiwa moja ya
jitihada za kuboresha hali ya utoaji wa huduma Afya nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua hali ya utaji huduma leo
katika Wilaya ya Ukerewe Mkoa wa Mwanza.
“Tuhakikishe kwamba Asilimia
80 ya vituo vyetu vyote vya kutolea huduma za Afya vyote kuwa na nyota 3 hicho
kiwe ni kiwango cha chini sana,” Alisema Dkt. Faustine Ndugulile.
Dkt. Ndugulile aliendelea
kusisitiza kwa watoa huduma za Afya juu ya nidhamu na matumizi ya lugha nzuri
pindi wanapokuwa wanawahudumia wagonjwa ili kupunguza malalamiko kutoka kwa
wananchi yasiyo na lazima,
Aidha, Dkt. Ndugulile alisema
kwamba Serikali imeweka utaratibu wa kuzitambua dawa zake kwa kuziwekea rebo ya MSD GOT katika dawa zote inazizitoa
na kusisitiza kwamba dawa hizo zinastahili kupatikana katika vituo vya Afya vya Serikali au kwa mgonjwa tu.
“Sisi kama Serikali tumeanza
kuweka utaratibu wa kuziwekea rebo dawa zote za Serikali lebo ya MSD GOT,
tumeziweka kwenye boksi na kwenye dawa , anaepaswa kuwa nazo ni hospitali zetu
na mgonjwa tu, mtu yoyote wa katikati akiwa na hizo dawa basi huyo ametuibia,
msimfumbie macho” Alisema Dkt Ndugulile.
Pia, Dkt Ndugulile ameahidi
kuwapelekea huduma za dharura katika Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe jambo
linalopelekea kupoteza maisha kwa wahitaji wa huduma hizo kutokana hali ya
ugumu wa usafiri kutoka kisiwani Ukerewe mpaka kufika katika hospitali ya Rufaa
ya Mkoa wa Mwanza SoukeToure
Kwa upande wake Mbunge wa
jimbo la Ukerewe Mhe. Joseph Mkundi amefarijika juu ya ujio wa Naibu Waziri Dkt.
Faustine Ndugulile jambo lililompa fursa ya kuona mazingira halisi na kuziona
changamoto ambazo wananchi kutoka Ukerewe wanakumbana nazo.
Kisha Mhe. Joseph Mkundi
alimuomba Dkt. Faustine Ndugulile (MB) kuwasaidia kuboresha huduma za hospitali hiyo ya Wilaya
ya Ukerewe kwa kuwajengea chumba cha upasuaji , chumba cha wagonjwa mahututi na
boti kwaajili ya kubebea wagonjwa ili kuwavusha kwenda hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Mwanza .
“Mambo ambayo nimekuwa
nikiyapigania ni juu ya kuboresha hospitali yetu ya Wilaya ili iweze kutoa
huduma kamilifu, kwa maana kwa mazingira yetu tunaichukulia kuwa ndio Hospitali
ya Rufaa, ikitokea mgonjwa kakosa usafiri inakuwa ni vigumu sana kuweza
kusaidia hali yake,” alisema Mhe. Mkundi.
0 on: "DKT. NDUGULILE AUGIZA UONGOZI WA MKOA WA MWANZA KUHAKIKISHA 80% YA VITUO VYA AFYA HAVISHUKI CHINI YA NYOTA 3."