Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akisisitiza jambo mbele ya Wadau wa Masuala ya Uwekezaji na
masuala ya Afya wakati akiwa katika Kikao cha kujadili Uwekezaji wa
Kiwanda cha kutengenezea Dawa nchini na Kampuni ya Fosun Pharma kutoka
nchini China.
Picha ya Wadau wa Masuala ya Uwekezaji na Masuala ya Afya, ikiongozwa na
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage
katika Kikao cha kujadili Uwekezaji wa Kiwanda cha kutengenezea Dawa
nchini na Kampuni ya Fosun Pharma kutoka nchini China.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akijadili jambo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe.
Charles Mwijage katika Kikao cha kujadili Uwekezaji wa Kiwanda cha
kutengenezea Dawa nchini na Kampuni ya Fosun Pharma kutoka nchini China.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimuaga Rais wa Kampuni ya Fosun Pharma inayotarajia kufungua kiwanda cha uzalishaji wa Dawa hapa nchini hivi karibuni baada ya majadiliano yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Kituo cha uwekezaji yaliyomuhusisha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage.
Picha ya Pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na Waziri wa Viwanda, Biashara
na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage baada ya kikao cha kujadili Uwekezaji
wa Kiwanda cha kutengenezea Dawa nchini na Kampuni ya Fosun Pharma
kutoka nchini China.
NA WAMJW-DAR ES SALAAM
KIWANDA
kikubwa cha kutengeneza dawa kinatarajiwa kujengwa nchini ili kupunguza
adha na gharama zinazoikumba nchi wakati wa kuagiza dawa nje ya
Tanzania.
Hayo yamesemwa
na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.
Ummy Mwalimu wakati wa kujadili uwekezaji wa kiwanda cha dawa hapa
nchini leo jijini Dar es salaam.
"Leo
tumekutana kujadili jinsi ya kuwekeza na kiwanda cha kutengeneza dawa
cha FOSUN PHARMA kutoka nchini ili kupunguza changamoto za kuagiza dawa
nje ya nchi na kutokomeza tatizo la upatikanaji wa dawa nchini", alisema
Waziri Ummy .
Aidha
Waziri Ummy amesema kuwa kutokana na kujengwa kwa kiwanda hiko
kitapunguza asilimia kubwa ya fedha inayokwenda nje kwa ajili ya
manunuzi ya dawa kwani mpaka sasa asilimia 94 ya fedha zinakwenda
kununua dawa nje na asilimia 6 ndiyo inannua dawa nchini.
Waziri
Ummy amesema kuwa kutokana na uwekezaji huo kutapelekea kupunguza muda
wa kuagiza dawa kwani muda mwingine kunachukua miezi 9 mpaka miezi 11
kupata dawa kutoka nje ya nchi hivyo kuifanya Serikali kuagiza mzigo
mkubwa zaidi ili kukimbizana na mahitaji ya Watanzania.
"Tunatumia
mda mrefu sana kupata dawa tangu tunapoagiza na wakati mwingine
tunaweza kupata dawa zisizo na ubora kutokana na dawa hizo zinakaguliwa
na mdhibiti wa nje hivyo zinaweza zikaruhusiwa tu na zikija kukaguliwa
na mdhibiti wa ndani unaweza kukuta hazina ubora" alisema Waziri Ummy.
Mbali
na hayo Waziri Ummy amesema kuwa kampuni hiyo inayotengeza sindano za
kutibu Maralia kali ya ATESUNAT itaweza kutengeneza sindano nyingi zaidi
na kuweza kuwahudumia nchi jirani ikiwemo Kenya, Uganda na Burundi.
Kwa
upande wake Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles
Mwijage amesema kuwa hakuna kikwazo kwa Kampuni hiyo kuanzisha ujenzi wa
kiwanda cha dawa hapa nchini kwani kitasaidia upatikanaji wa dawa kwa
urahisi na kukua kwa uchumi kupitia viwanda.
"Tumejadili
na kuwakubalia bila ya kuweka kikwazo kwani tumeridhishwa na ubora wao
katika utengenezaji wa dawa na mafuta nchini kwao hivyo tunawakaribisha
kuja kufanya uwekezaji huo" alisema Waziri Mwijage.
Naye
Mkurugenzi wa Kituo Cha Uwekezaji Nchini Bw. Geofrey Mwambe amesema
kuwa wameupokea uwekezaji huo na wanaufanyia kazi haraka iwezekanavyo
ili kuipeleka Tanzania kuelekea uchumi wa Viwanda.
"Kutokana
na ahadi ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli la kuipeleka nchi kwenye
uchumi wa viwanda na kutokomeza kabisa tatizo la uhaba wa dawa hatuna
budi kushirikiana na wawekezaji hao kutimiza lengo hilo" alisema Bw.
Mwambe.
Kika hiko cha
kujadili uwekezaji wa kiwanda hiko cha kutengeneza dawa kimeudhuriwa na
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage,
Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA, Bohari kuu ya Dawa MSD, Kituo cha
Uwekezaji nchini TIC na wadau mbalimbali.
0 on: "KIWANDA CHA DAWA KIKUBWA KUJENGWA NCHINI. "