Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akitoa maelekezo juu ya matangazo yaliyo kwenye mbao mapema leo
wakati alipofanya ziara ya kukagua huduma za Afya zinazotolewa katika
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akimsikiliza moja kati ya wagonjwa waliofika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala wakati
alipofanya ziara mapema leo katika Hospitali hiyo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akimsikiliza kwa makini Bi Halima Said aliyefika kupata huduma
za matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala pindi
alipofanya ziara mapema leo katika Hospitali hiyo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akiongea na Bi. Angelina Erasto juu ya umuhimu wa kukata Bima ya
Afya ya TOTO AFYA KADI itakayomsaidia kupunguza gharama za matibabu kwa
mtoto wake,
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
akishangaa idadi kubwa ya wakina mama iliyozidi kiasi katika wodi ya
kupumzikia wakina mama baada ya kujifungua, akiwa katika ziara yake ya
kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala kukagua ubora wa
Huduma zitolewazo katika Hospitali hiyo.
NA
WAMJJW-DAR ES SALAAM
WIZARA ya afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imetangaza
rasmi kuanzia Juali 1 2018 imepokea
Hospitali 28 za Rufaa za Mikoa ambazo zilikuwa chini ya usimamizi wa
OR-TAMISEMI .
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipofanya ziara katika
Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala.
“Hospitali ambazo tumezipokea zina jumla
ya vitanda 7,474 na jumla ya watumishi 8,671 ambao, kati yao Wauguzi ni
3,960, Madaktari 536, Madaktari Bingwa wa fani mbalimbali ni 182, na waliobakia
ni watumishi wa kada zingine mbalimbali za Afya” alisema Waziri Ummy.
Waziri Ummy amesema kuwa Hospitali ambazo Wizara imezipokea ni Hospitali
ya Rufaa ya Mkoa ya Mount Meru (Arusha), Dodoma General (Dodoma), Kitete
(Tabora), Shinyanga, Geita, Singida, Mpanda (Katavi), Mawenzi (Kilimanjaro),
Bombo (Tanga), Morogoro, Ligula (Mtwara), Sokoine (Lindi), Maweni (Kigoma),
Sekou Toure (Mwanza), Mwananyamala, Amana, Temeke (Dar es Salaam), Songwe,
Kibena (Njombe), Iringa, Tumbi (Pwani), Sumbawanga (Rukwa), Bariadi (Simiyu),
Musoma (Mara), Songea (Ruvuma), Mbeya, Babati (Manyara) na Bukoba (Kagera).
Waziri Ummy alisema kuwa katika mwaka wa fedha 2018/19, Wizara imetenga
shilingi Bilioni 30 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya kipaumbele katika
Hospitali za Rufaa za Mikoa ambako tayari huduma zinatolewa ikiwemo Matibabu
kwa wagonjwa wa dharura ,Huduma za upasuaji wa dharura hususan wakati wa
ujauzito na uzazi pamoja na Huduma za tiba kwa wagonjwa mahututi zikiwemo za
watoto wachanga .
Mbali na hayo Waziri Ummy
amesikitishwa na upungufu wa wodi pamoja na vitanda kwa ajili ya wanawake wanaofika kujifungua katika
hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala na kuahidi kulifanyia kazi mara moja
iwezekanavo.
“Kama Mama,na nimeumia sana na lazima tulifanyie ufumbuzi mara moja
kwahiyo namuagiza katibu mkuu alete mtaalamu wa majengo na tupandishe fedha za
kujenga ghorofa mbili mara moja kwakweli halii hii haikubaliki” alisema Waziri
Ummy.
Mnamo Novemba 25, 2017 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizindua Hospitali ya Taaluma na
Tiba (MAMC) ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)
aliagiza kuwa Hospitali za Rufaa za Mikoa zihamishiwe kwenye usimamizi wa
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (WAMJW) kutoka
Ofisi ya Rais TAMISEMI.
0 on: " WIZARA YA AFYA YATANGAZA RASMI KUPOKEA HOSPITALI ZA RUFA ZA MIKOA."